Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wavuta nywele wapunguziwa adhabu EPL

Muktasari:

  • Maafisa wa mchezo pia wataagizwa kuweka mkazo zaidi katika kupambana na kushikana na kuvutana ndani ya eneo la hatari, jambo ambalo limekuwa la kawaida wakati wa kona na mipira ya adhabu.

LONDON, ENGLAND: WAAMUZI wa Ligi Kuu England watabadilisha namna wanavyotafsiri matukio ya kuvuta nywele kuanzia msimu ujao wa 2026/27, baada ya wachezaji watatu kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa hilo katika msimu uliopita.

Maafisa wa mchezo pia wataagizwa kuweka mkazo zaidi katika kupambana na kushikana na kuvutana ndani ya eneo la hatari, jambo ambalo limekuwa la kawaida wakati wa kona na mipira ya adhabu.

Aidha, hatua mpya zinatarajiwa kuanzishwa ili kudhibiti tabia ya makipa kutumia majeraha au kuchelewesha mchezo kwa makusudi kama mbinu ya kupunguza kasi ya mchezo.

Mabadiliko hayo yalipitishwa katika mkutano mkuu wa kila mwaka wa Ligi Kuu mapema mwezi huu baada ya mashauriano na kikundi cha ushauri wa kuboresha mchezo. Yatakuwa sehemu ya mwongozo mpya wa "kanuni za soka" na "maeneo ya mkazo kwa waamuzi" kwa msimu wa 2026/27.


Kadi Nyekundu za Kuvuta Nywele zilizozua Mjadala

Katika msimu uliopita, kadi zote tatu nyekundu za kuvuta nywele zilitolewa baada ya mapitio ya VAR.

Wachezaji walioadhibiwa ni Michael Keane wa Everton FC, Lisandro Martinez wa Manchester United na Dan Ballard wa Sunderland AFC.

Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, aliwahi kuelezea moja ya uamuzi hayo kama:"Mojawapo ya uamuzi mbaya zaidi ambayo nimewahi kuona."

Hata hivyo, rufaa ya klabu hiyo ya kuondoa adhabu ya kufungiwa mechi tatu ilikataliwa.

Pia, beki wa Stockport County, Josh Dacres-Cogley, alitolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa kama hilo katika fainali ya mtoano ya League One.


Nini Kitabadilika?

Kuanzia msimu ujao, si kila tukio la kuvuta nywele litakalosababisha kadi nyekundu.

Badala yake, waamuzi watazingatia zaidi:Nguvu iliyotumika.

Nia ya mchezaji aliyefanya kitendo hicho.Ikiwa kitendo hicho kilikuwa cha makusudi au cha bahati mbaya.

Mwongozo mpya unasema waamuzi wanapaswa kutafuta:"Kitendo cha wazi na cha makusudi" ambacho kinaonyesha "matumizi ya nguvu kupita kiasi na/au ukatili."

Wachezaji wangeadhibiwaje Chini ya Sheria Mpya?

Michael Keane huenda bado angepewa kadi nyekundu kwa sababu alivuta nywele za Tolu Arokodare wa Wolverhampton Wanderers kwa namna iliyotafsiriwa kama kitendo cha vurugu.

Dan Ballard na Josh Dacres-Cogley huenda wangepata kadi ya njano badala ya nyekundu.

Tukio la Lisandro Martinez lingekuwa katika eneo la tafsiri tofauti na lingeachwa zaidi kwa uamuzi wa mwamuzi.

Kwa kuwa VAR haiwezi kuingilia kati kutoa kadi ya njano, baadhi ya matukio kama hayo yangeweza kuishia kuadhibiwa kwa onyo pekee.


Lengo la Mabadiliko

Mabadiliko haya yanalenga kuwapa waamuzi nafasi kubwa zaidi ya kutofautisha kati ya kuvuta nywele kwa makusudi na matukio ambayo mchezaji ameshika nywele za mpinzani kwa bahati mbaya wakati wa mapambano ya kawaida ya mchezo.

Kwa hivyo, kuvuta nywele hakutaruhusiwa, lakini si kila tukio la aina hiyo litachukuliwa moja kwa moja kama kosa la kadi nyekundu kuanzia msimu wa 2026/27.