Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watkins atua anga za Man United, dau latajwa

Muktasari:

  • Licha ya nia ya kutaka kumsajili Watkins taarifa zinaeleza kwamba huenda dili hilo likawa gumu kwa Manchester United, kwani kiasi cha pesa zinazohitajika na Villa ni nyingi.

MSHAMBULIAJI wa Aston Villa, Ollie Watkins, mwenye umri wa miaka 29, yupo kwenye orodha ya mastaa ambao Manchester United imepanga   kuwasajiliwa katika dirisha hili ikiwa mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark, Rasmus Hojlund, 22, ataondoka katika viunga vya Old Trafford.

Licha ya nia ya kutaka kumsajili Watkins taarifa zinaeleza kwamba huenda dili hilo likawa gumu kwa Manchester United, kwani kiasi cha pesa zinazohitajika na Villa ni nyingi.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Athletic, Villa inahitaji zaidi ya Pauni 60 milioni kama ada ya uhamisho ya Watkins kwenda timu inayomtaka.

Mbali ya Hojlund, Man United pia imepanga kuachana na washambuliaji wengine kadhaa akiwemo Marcus Rashford na Antony ambao wote walicheza kwa mkopo kwa msimu uliopita wakionyesha viwango bora.


Luis Diaz

BAYERN Munich imeongeza jina la mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Colombia, Luis Diaz, 28, kwenye orodha ya wachezaji inaotaka kuwasajili dirisha hili. Taarifa zinaeleza, Bayern inatafuta winga wa kushoto wa kiwango cha juu na Diaz anaonekana kuwa mmoja wa malengo yao. Hata hivyo, anaripotiwa kutamani zaidi kutimkia Barcelona akiondoka Liverpool.


Eberechi Eze

ARSENAL imefanya mazungumzo na wawakilishi wa Crystal Palace pamoja na wakala wa kiungo wa timu hiyo na England, Eberechi Eze, 27, ambaye ana kifungu cha kuondoka ikiwa timu inayomtaka italipa Pauni 67.5 milioni. Eze anahitajika Arsenal ili kusuka upya eneo la kiungo ambalo limeondokewa na kiungo mwandamizi akiwamo Thomas Partey.


Tolu Arokadare

FULHAM inataka kupimana ubavu na AC Milan na Manchester United kuwania saini ya mshambuliaji wa Genk na timu ya taifa ya Nigeria, Tolu Arokodare, 24, katika dirisha hili. Maskauti wa timu zote tatu wamekuwa Ubelgiji mara kadhaa kumtazama akicheza, lakini Fulham ndio inaonekana mstari wa mbele kutaka kuwasilisha ofa.


Mohammed Kudus

TOTTENHAM Hotspur ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa West Ham United na timu ya taifa ya Ghana, Mohammed Kudus, 24, na ina matumaini ya kufanikisha dili hilo kwa kiasi kidogo sana cha fedha tofauti na kifungu kilichopo katika mkataba wake kinachotaka kulipa Pauni 85 milioni. Kudus mwenyewe ameonyesha nia ya kuwa tayari kujiunga na Spurs ambao watashiriki Ligi ya Mabingwa.


Richarlison

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Richarlison de Andrade, 28, ameruhusiwa kuondoka Tottenham Hotspur katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi ambapo taarifa zinaeleza anakwenda kujiunga na Galatasaray ya Uturuki. Richarlison amekuwa akihusishwa kuondoka tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu, lakini ilishindikana baada ya Spurs kuzuia dili lake.


Christopher Nkunku

CHELSEA inahitaji kupata karibu Pauni 35 milioni kama ada ya uhamisho ya kuipata saini ya  mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Christopher Nkunku, 27, katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Nkuku anadaiwa kuomba mwenyewe kuondoka katika dirisha hili ili kujiunga na timu itakayompa nafasi kubwa ya kucheza tofauti na ilivyo sasa.


Rav van den Berg

CRYSTAL Palace imepanga kutumia ya Pauni 27 milioni kwa ajili ya kusajili wachezaji wawili kutoka Middlesbrough ambao ni  kiungo raia wa England, Hayden Hackney, 23, na beki raia wa Uholanzi, Rav van den Berg, 20, wote katika dirisha hili. Mastaa hao ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Middlesbrough lakini timu yao ipo tayari kuwauza.