Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasaudia waanza kumnyemelea Lewandowski

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa Lewandowski bado ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Barca, lakini timu hiyo imekuwa ikipanga kuachana naye mwisho wa msimu kutokana na umri wake kwani wanahitaji kujenga kikosi chao kutokana na wachezaji vijana zaidi.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski, 37, anaweza kushawishika kuhamia Ligi ya Saudi Arabia ikiwa Barca itaendelea kushikilia msimamo wa kuachana naye mwisho wa msimu.

Kwa sasa Lewandowski bado ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Barca, lakini timu hiyo imekuwa ikipanga kuachana naye mwisho wa msimu kutokana na umri wake kwani wanahitaji kujenga kikosi chao kutokana na wachezaji vijana zaidi.

Vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vinaeleza tayari kuna ofa nono kutoka Saudi Arabia amazo zimewekwa mezani kwa ajili ya kumshawishi atimkie huko baada ya kuondoka Barca.

Awali ilidaiwa huenda akaendelea kusalia Ulaya kwa kujiunga na AC Milan au kurudi Poland kumaliza soka nyumbani kwao.

Hadi sasa Barcelona haijatoa msimamo rasmi iwapo ipo tayari kumwachia staa huyo au itaendelea kuwa naye ingawa taarifa za ndani zimeshaeleza imepanga kuachana naye.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote, amefunga mabao nane na kutoa asisti mbili.



Casemiro

KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, bado hajafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatima ya kiungo wa Brazil Casemiro, 33, na beki wa England Harry Maguire, 32, kuelekea dirisha lijalo.

Wachezaji hao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na kutofanyika kwa mazungumzo ya kuwaongeza hadi sasa kumeibua uwezekano mkubwa wa kuondoka.

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, Casemiro alikuwa alikuwa akihusishwa kuondoka lakini mpango huo ulifeli baada ya kocha kudai anaridhishwa na kiwango chake.


James Garner

MANCHESTER United inafikiria kufanya usajili wa kushtukiza wa aliyekuwa kiungo wao wa zamani, James Garner, 24, dirisha la Januari.

Garner ambaye kwa sasa anakipigaEverton, mkataba wake unatarajiwa kumalizika katika dirisha la majira ya kiangazi, jambo linaloipa Man United tamaa zaidi kwani itampata kwa bei nafuu.

Kiungo huyo wa zamani wa timu ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 21, amekuwa katika kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu.


Jeremy Jacquet

CHELSEA inaendelea kumfuatilia kwa karibu beki wa Rennes Jeremy Jacquet, 20, pamoja na mshambuliaji chipukizi wa Saint-Etienne Djylian N’Guessan, 17, kama sehemu ya mipango yao ya usajili wa dirisha lijalo la majira ya baridi na kiangazi.

Hata hivyo, kipaumbele kikubwa cha klabu hiyo katika dirisha la Januari ni kuwaondoa baadhi ya wachezaji waliopo ili kupunguza mzigo wa mishahara na idadi.

Miongoni mwa waliopo kwenye orodha ya kuuzwa ni beki wa kimataifa wa Ufaransa Axel Disasi, 27, pamoja na winga raia wa England Raheem Sterling, 31, na Tyrique George, 19.


Sandro Tonali

JUVENTUS imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali, 25, dirisha lijalo la usajili.

Tonali, ambaye aliwahi kung’ara Serie A akiwa na AC Milan, anatajwa kuwa tayari kurejea Italia iwapo makubaliano yatafikiwa kati ya klabu hizo mbili.

Mbali ya Tonali, Juventus pia inamfuatilia beki wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Romania, Radu Dragusin, ambaye anawindwa na AS Roma pia.


Oscar Bobb

FULHAM na Crystal Palace zinaendelea kumfuatilia kwa karibu kiungo mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Norway, Oscar Bobb, 22.

Klabu hizo zinasubiri kuona kama Man City itaruhusu mchezaji huyo kuondoka kwa mkopo au uhamisho wa moja kwa moja dirisha la Januari.

Mbali ya klabu hizo za England, pia Sevilla ya Hispania inatajwa kutaka kumsajili.


Luis Guilherme

SPORTING CP imewapiku wapinzani wao wa jadi FC Porto katika mbio za kumsajili winga wa West Ham United, Luis Guilherme, 19.

Klabu hiyo ya Lisbon iko karibu kukamilisha makubaliano ya uhamisho wa kudumu wa mchezaji huyo raia wa Brazil, ambaye anaonekana kuvutiwa na mpango wa  kurejea Ureno.

Guilherme alijiunga na West Ham 2024, lakini ameshindwa kufikia matarajio na ameomba kuondoka mwenyewe ili kupata muda mwingi wa kucheza.


Joelinton

KIUNGO wa Newcastle United na timu ya taifa ya Brazil, Joelinton, 29, ni miongoni mwa wachezaji wanaofuatiliwa kwa karibu na klabu za Ligi ya Saudi Arabia.

Newcastle inatajwa kuwa tayari kufanya majadiliano ya kumuuza ikiwa itawasilishwa ofa nzuri mezani. Joelinton amekuwa nguzo muhimu katika safu ya kiungo ya Newcastle.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.