Prime
Siri nzito ya usajili wa Shalulile Yanga
WAKATI mashabiki wa Yanga wakisubiri kumuona mshambuliaji mpya Peter Shalu-lile akianza kazi ndani ya kikosi chao, sasa imefahamika kwa nini klabu hiyo ilifanya kila linalowezekana kumsajili staa huyo mkubwa kwenye ukanda huu.
Yanga imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo raia wa Namibia kwa mkataba wa miaka miwili, ikiwa ni moja ya hatua kubwa zaidi kwenye dirisha la usajili la msimu wa 2026/27, huku ikionyesha wazi kuwa safari ya kutafuta mafan-ikio makubwa Afrika imeanza rasmi.
Shalulile ambaye kabla alikuwa ametumika Mamelodi kwa misimu sita, ametua Jangwani akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza kipindi chake cha mafanikio kati-ka soka la Afrika Kusini ambako alijijengea heshima kubwa kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao, kushambulia na ni tishio kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na kasi na uwezo alionao wa kuficha mpira.
Staa huyo ambaye alikuwa akivaa jezi namba 38 ndani ya kikosi cha Mamelodi, ndiye mchezaji mwenye mafanikio makubwa zaidi kwenye Ligi ya Tanzania kati ya wale ambao wamesajiliwa kwenye dirisha hili, ikiwa ni miezi michache tu imepita tangu aliposhiriki kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa FAR Rabat ya Morocco.
Mshambuliaji huyo wa kati ambaye hakuwa na nafasi sana kwenye timu yake msi-mu uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha amesajiliwa na Yanga akiwa ni mchezaji huru lakini akitajwa kuwa mmoja kati ya mastaa wakubwa kwenye soka la Afrika kwa sasa.
Staa huyo mzaliwa wa Namibia mwenye umri wa miaka 32 ambaye Mwanaspoti lilikuwa la kwanza kuripoti ujio wake nchini anapewa nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha Yanga mbele ya washambuliaji wengine, Clement Mzize, Dilson Maria Aurélio ‘Depu’ pamoja na mshambuliaji mpya Cheikh Ibrahim Toure kutokana na uwezo na uzoefu wake kwenye soka la Afrika.
Lakini nyuma ya usajili huo kuna mambo makubwa yaliyofanya Yanga iamue kuvunja benki kwa mshambuliaji huyo.
DOLA 700,000 ZATAJWA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja kati ya mameneja wa staa huyo, imes-ema kuwa Yanga imefanikiwa kuzipiku baada ya timu kubwa Afrika baada ya kufikia kitita cha dola 700,000 sawa na shilingi 1.8 bilioni ambacho kilikuwa kinatakiwa ili nyota huyo asaini mkataba wa miaka miwili, hata hivyo amesema kuwa fedha hizo zinalipwa kwa awamu nne.
“Awali haikufahamika kama Tanzania kuna timu inaweza kufanya hivyo, lakini baada ya mazungumzo ya muda mrefu Yanga waliweza kufikia mahitaji hayo na hivyo hakuna aliyekuwa na kipingamizi kwa kuwa mchezaji mwenyewe alitaka kubaki Afri-ka pamoja na kwamba alikuwa na ofa kadhaa za nje na ndani zikiwemo timu kutoka Morocco,” kilisema chanzo hicho ambacho kwa sasa kipo nchini Rwanda kwenye michuano ya Kagame
MNGQITHI NDIYE KICHOCHEO
Hata hivyo, Moja ya sababu kubwa zilizofanya dili hilo litimie ni uwepo wa kocha mpya wa Yanga, Manqoba Mngqithi, ambaye anamfahamu vizuri Shalulile kutokana na kufanya naye kazi katika klabu ya Mamelodi Sundowns na kabla mchezaji huyo alimuuliza kocha huyo kuhusu nafasi yake kikosini na mipango ya Yanga kuelekea msimu ujao, alipopewa projekti nzima alikubalianana dili hilo baada ya mambo yote kuwa sawa.
Wawili hao walikuwa sehemu ya kipindi cha mafanikio cha Sundowns, wakitwaa mataji mbalimbali ya ligi na kujenga moja ya mifumo bora ya ushambuliaji Afrika Kusini.
Mngqithi anaamini Shalulile bado ana uwezo wa kuongoza safu yake ya ushambuliaji kutokana na vitu ambavyo amekuwa akivipenda kwake, uwezo wa kukimbia nyuma ya mabeki, presha anapopoteza mpira, uelewa wa nafasi na umaliziaji.
MASHINE YA MABAO
Kabla ya kuja Tanzania, Shalulile alijenga jina kubwa kutokana na uwezo wake wa kufunga mabao na kufanya kazi kwa bidii ndani ya uwanja, akiwa na Mamelodi kwa kipindi cha misimu sita staa huyo alifunga jumla ya mabao 104 katika michezo 219 akiwa ni mchezaji mwenye kiwango bora zaidi cha mabao kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara.
Mbali na kufanya hivyo akiwa na Mamelodi awali Shalulile alifanikiwa kufanya mam-bo makubwa akiwa na Highlands Park ambapo alitumika kwa misimu mitano, aki-funga mabao 49 kwenye michezo 134.
Ndani ya timu ya taifa ya Namibia, mshambuliaji huyo mrefu anayependa ku-chomekea muda wote ametumika kwa miaka 12 akicheza michezo 66 na kufunga mabao 20.
MBELGIJI ASHTUKA
Kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael, ameshindwa kujizuia kutoa maoni yake kuhusu usajili huo mkubwa uliofanywa na mabingwa hao wa Tanzania, akisema Wananchi wamefanya jambo kubwa kwa kumpata mmoja wa washambuliaji bora Afrika ambaye atawafanya waendelee kuwa tishio kwenye michuano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Eymael, ambaye amewahi kufanya kazi katika klabu mbalimbali za Afrika Kusini iki-wemo Chippa United, Polokwane City na Black Leopards wakati Shalulile akiwe kwenye ligi hiyo, alisema uzoefu wa mshambuliaji huyo anayeshangilia mabao yake kwa madaha unamfanya kuwa usajili wa kiwango cha juu kwa Yanga na timu yoyote ya Tanzania kuelekea msimu mpya.
“Yanga wamepata mchezaji mkubwa sana, Shalulile sio mshambuliaji wa kawaida, ni mchezaji ambaye amethibitisha uwezo wake katika mazingira magumu ya soka la Afrika Kusini. Wamepata mchezaji mwenye ubora na uzoefu mkubwa,” alisema Eymael.
Kocha huyo anaamini ujio wake Yanga unaweza kuwa silaha kubwa katika harakati za klabu hiyo kutafuta mafanikio kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuliko kufikiri ku-husu ligi ya ndani.
‘’Huyu ni silaha muhimu sana kwa Yanga hasa kwenye michuano ya CAF, ana kila kitu kwenye kikosi, ana uzoefu wa kutosha, ana uwezo uwanjani na anaweza pia kuwaongoza wenzake wakati wa mechi ngumu.’’
SASA BADO WAWILI
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema kuwa bado watasajili wachezaji wawili wa kimataifa, tofauti na ilivyokuwa inaelezwa na rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said kuwa sasa wamebakiza usajili mmoja tu.
Hersi wakati anatangaza mastaa watatu ambao ni Chekh Ibrahima Toure, Houssein Zakouani na Albert Kangwanda alisema bado wachezaji wawili.
Hata hivyo juzi usiku Yanga ilimtangaza Shalulile na kubaki mchezaji mmoja, lakini bosi huyo wa kitengo cha habari alidai bado wawili.
“Yanga bado tunasajili msianze kupanga kikosi vinakuja vyuma vingine viwili am-bavyo vitawastaajabisha,” alisema.
Mbali na hilo aliwatuliza Wanayanga kwamba wanakwenda kusajili top namba sita Afrika ambaye usajili wake utatangaza hivi karibuni.
“Yanga haijafanya mazungumzo yoyote na kiungo Morice Chukwu, ni mchezaji mzuri, lakini hajazungumza chochote na klabu yetu.”