Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Napoli bado inamtaka Mainoo, Man United yamzuia ikitaja sababu

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Napoli ilikuwa miongoni mwa timu zilizotaka kumsajili dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini dili hilo lilifeli kwa kile kinachoelezwa Amorin alizuia kuondoka kwake hadi atakapopatikana mbadala wake.

KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim anadaiwa kuzuia mpango wa kuondoka kwa kiungo wao, Kobbie Mainoo dirisha lijalo la majira ya baridi licha ya kuhusishwa kuondoka.

Inaelezwa Amorim anataka kwanza Man United isajili mbadala wa Mainoo kabla ya kumwachia fundi huyo mwenye umri wa miaka 20.

Napoli ilikuwa miongoni mwa timu zilizotaka kumsajili dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini dili hilo lilifeli kwa kile kinachoelezwa Amorin alizuia kuondoka kwake hadi atakapopatikana mbadala wake.

Licha ya kufeli kwa wakati huo, Napoli bado imeendelea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili staa huyu kwa mkopo ifikapo Januari mwakani.

Mainoo kwa sasa anasumbuliwa na majeraha ambayo yanadaiwa yatamweka nje kwa wiki kadhaa kabla ya kurejea Januari mwakani sawa na Bruno Fernandes ambaye majeraha yake yanaonekana yatamweka nje kwa muda mrefu zaidi.

Mkataba wa sasa wa Mainoo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na licha ya kutompa nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza na mara zote Amorim amekuwa akisisitiza bado ana mipango ya kumtumia fundi huyu.


Davide Bartesaghi

ARSENAL imeanza mazungumzo na AC Milan ili kumsajili beki wa pembeni wa timu hiyo, Davide Bartesaghi, 19, ambaye inamwona kama sehemu ya mipango yao ya kuimarisha safu ya ulinzi.

Bartesaghi bado ana mkataba wa muda mrefu na Milan hadi mwaka 2030, hivyo timu hiyo inadaiwa kutaka kiasi kinachokadiriwa kufikia Pauni 45 milioni ili kumuuza.

Hadi sasa Arsenal haijawasilisha ofa rasmi ya kumsajili fundi huyu.


Youri Tielemans

ASTON VILLA imeanza rasmi mazungumzo na kiungo wao wa kimataifa wa Ubelgiji, Youri Tielemans ili kumsainisha mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi chao.

Mkataba wa sasa wa Tielemans unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 lakini Villa inataka kumsainisha mkataba mpya mapema baada ya kuona baadhi ya  vigogo barani Ulaya wameanza kumnyemelea.

Kwa sasa Villa haina mpango wa kumuuza lakini inaamini ikimsainisha mkataba mpya inaweza ikapata ofa nono zaidi.


Yan Diomande

LIVERPOOL na Chelsea zimenza mchakato wa kumsajili winga wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yan Diomande, 19,  dirisha lijalo la majira ya baridi.

Ripoti zinaeleza mabosi wa Leipzig wapo tayari kumwachia lakini kwa kiasi kisichopungua Pauni 69  milioni.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2030, msimu uliopita alicheza mechi 15 za michuano yote na kufunga mabao sab.


Lorenzo Torriani

ARSENAL inataka kumsajili kipa wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia, Lorenzo Torriani, 20. Maskauti wa washika mitutu hao wa Jiji la London wanadaiwa kumwangalia staa huyo kwa muda sasa na wameandika ripoti inayopendekeza asajiliwe baada ya kuridhishwa na kiwango bora alichoonyesha.

Awali kinda huyu alionekana kama mbadala sahihi wa Mike Maignan anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu lakini sasa mambo yamebadilika na Milan itatakiwa kutafuta mbadala wake ikiwa itakubali kumuuza kwenda Arsenal.


Matt Targett

NEWCASTLE United imeanza mchakato wa kumrejesha mapema beki wao wa kushoto raia wa England, Matt Targett, 30, ambaye anacheza kwa mkopo Middlesbrough inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mpango wa Newcastle kutaka kumrudisha Targett ambaye alisaini mkataba wa mkopo wa msimu mmoja kuitumikia Middlesbrough umechochewa na majeraha ya beki wao Dan Burn, 33 ambaye atakosekana kwa muda  hali inayomlazimu kocha kutafuta chaguo mbadala haraka.


Elliot Anderson

Manchester United bado ina mpango wa kumsajili kiungo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, Elliot Anderson, 23, ili akaongeze chachu zaidi katika eneo lao kiungo.

Hata hivyo, fundi huyu  pia anawindwa na Liverpool na Newcastle ambazo zinahitaji huduma yake. Ripoti zinaeleza mabosi wa Forest wanahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza staa huyu katika dirisha lijalo au mwisho wa msimu.


Ousmane Diomande

CRYSTAL Palace inataka kuanza tena mazungumzo na wawakilishi wa beki kisiki wa Sporting Lisbon, Ousmane Diomande ili kumsajili dirisha lijalo la majira ya baridi.

Mabosi wa Palace wanamwangalia fundi huyu kama mbadala wa beki wao Marc Guehi, 25, ambaye anatarajiwa kuondoka katika dirisha lijalo au mwisho wa msimu.

Diomande ambaye ni miongoni mwa mabeki tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Lisbon na timu ya taifa ya Ivory Coast, amewahi pia kuhitajika na Chelsea na baadhi ya timu nyingine za England.