Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafyekwa! Ripoti ya kocha Man United ipo hivi

FYEKA Pict

Muktasari:

  • Casemiro ambaye ni raia wa Brazil, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu lakini una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim ameshawasilisha baadhi ya sehemu za ripoti yake ya usajili wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambayo inaonyesha beki Harry Maguire ataongeza mkataba mpya, Casemiro ataachwa mwisho wa msimu na wachezaji kibao watakatwa.

Casemiro ambaye ni raia wa Brazil, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu lakini una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Hata hivyo, ripoti ya kocha inaonyesha kuwa hana mpango wa kuendelea naye na badala yake anamtaka kiungo wa Brighton, Carlos Baleba kama mbadala wake.

Casemiro, ambaye atatimiza miaka 34 Februari mwakani, ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi Man United, akipokea Pauni 300,000 kwa wiki tangu alipojiunga kwa ada ya Pauni 70 milioni mwaka 2022.

Kocha amependekeza Maguire kupewa mkataba mpya ifikapo Januari mwakani kabla ya ule wa sasa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Amorim pia ndiye aliyependekeza Man United kutumia kipengele cha kuongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wa beki huyo Januari mwaka jana.

Maguire, aliyekuwa beki ghali zaidi duniani alipojiunga na United kutoka Leicester kwa ada ya Pauni 80 milioni mwaka 2019, analipwa Pauni 190,000 kwa wiki na katika mkataba wake mpya atatakiwa kukubali kupokea chini ya hapo.

FYE 01

Man United pia inatarajia kuachana rasmi na Jadon Sancho, ambaye kwa sasa yupo Aston Villa kwa mkopo wa msimu mzima.

Sancho, aliyenunuliwa kwa ada ya Pauni 73 milioni katika dirisha la majira ya baridi mwaka 2023, hajacheza mechi yoyote ya ligi akiwa na Man United kwa zaidi ya miaka miwili sasa baada ya kuingia katika mgogoro na kocha Erik ten Hag hali iliyosababisha atolewe kwa mkopo kwenda Borussia Dortmund na baadaye Chelsea kabla ya kupelekwa Aston Villa katika dirisha lililopita.

Licha ya kwamba Man United ina kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi kwenye mkataba wa Sancho, kocha Amorim hahitaji huduma yake na ametoa ruhusa ya kuuzwa Januari ili timu ipate pesa itakazotumia kusajili wachezaji wengine kwa wakati huo.

Beki Tyrell Malacia ndiye mchezaji pekee katika kundi la mastaa walioondolewa katika timu na Amorim aliyebaki baada ya kukosa timu ya kujiunga nayo katika dirisha lililopita.

Malacia alisajiliwa wakati Ten Hag anaingia Man United lakini alipoteza siku takribani siku 550 bila kucheza United kutokana na majeraha ya goti yaliyohitaji afanyiwe upasuaji mara mbili.

Baada ya kurejea msimu uliopita, Amorim alimchezesha katika mechi tano lakini kiwango chake hakijaonekana kumshawishi, hivyo naye amemweka katika orodha ya wachezaji wanaopaswa kuuzwa.


Kipa namba tatu, Tom Heaton ambaye atakuwa na miaka 40 ifikapo mwisho wa msimu huu, naye anaweza kuachwa Januari kwa maelekezo ya Amorim.

Heaton kwa sasa anadaiwa kusoma kozi ya ukocha na kuna uwezekano pia akastaafu mwanzoni mwa mwaka ujao.

Kuachwa kwa wachezaji hawa pia kutasaidia kusajiliwa kwa wachezaji wapya kwani kuondokwa kwao kutawapa pesa watakazotumia kufanya sajili mbalimbali mwisho wa msimu.