Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nedy Music: Mapenzi hayana adabu

KAMERA Pict


KINACHOWEZA kuwatofautisha binadamu ni levo za kimaisha, urefu, ufupi, unene, wembamba, imani, lakini linapokuja suala la mapenzi halijawahi kuchagua mtu, kumfurahisha ama kumuumiza.


Mfano mzuri ni supastaa wa zamani wa Brazil, Ricardo Kaka licha ya upole, uamini na upendo wa kweli aliyokuwa nao kwa aliyekuwa mke wake Caroline Celico haikusaidia chochote kuachwa.


Mwanamke huyo aliweka wazi kuachana kwao mwaka 2015  licha ya kudumu katika ndoa hiyo miaka 10 tangu walipofunga 2005 na kujaaliwa watoto wawili, hakuhusiani na usaliti wala migogoro ya kifamilia kama anavyosema: “Alikuwa mume mzuri anayenijali kwa kila hali ila nahisi nilikuwa nakosa kitu, sikuwa na furaha.”

Jambo ambalo msanii wa Bongo Fleva, Said Seif Ally ‘Nedy Music’ anaiambia Nyuma ya Kamera yeye ni nani hadi akoswe kwenye matukio ya kuteswa na mapenzi kama ilivyo kwa mastaa wengine duniani.

KAME 01

Nedy Music aliyezaliwa Februari 24, 1995 anasimulia tukio la mwanamke aliyewahi kumpenda sana hadi ilifikia hatua ya kupelekana kwa wazazi, lakini mwishowe alijikuta akiambulia aibu na machozi.

“Mapenzi yanamliza kila mtu kwa wakati wake, hayana levo za kimaisha wala umaarufu, binafsi nimewahi kulia mara nyingi kutokana na kuachwa, tukio ambalo limesalia kwenye kumbukumbu zangu licha ya kufanyika muda mrefu ila bado nikilikumbuka na sipendi kuliongelea, nilika taliwa na wazazi wa mw anamke niliyempenda kisa naimba muziki,” anasema Nedy Music na kuongeza;

KAME 02

“Sitalitaja jina la huyo mwanamke wala wazazi wake, maana kuna maisha mengine yameendelea, nakumbuka nilipotambulishwa mimi na wakajua kazi yangu ni muziki hawakuhitaji mtu kama mimi katika familia yao, walihitaji kusikia mtu wa aina fulani kama meneja wa kampuni hivi, ilitoka kauli moja ya aniniache kwa haraka sana.

“Ni kitu kilichoniumiza sana, maana nilihukumiwa kwa kazi yangu, lakini kitu pekee ambacho wazazi wengi wanaishi na watato wao kwa tabia feki na siyo uhalisia, mimi niliyechukuliwa siyo mtulivu ama hadhi yangu ya kazi haikuwafurahisha ndiye nilikuwa nabadilisha tabia mbovu ya binti, kwani alikuwa huru kunieleza kila kitu, halafu mapenzi hayapo kwenye vitu, mtu anaweza akawa ana vitu anakupa lakini hajawahi kukupenda.”

KAME 03

Neddy Music anasema kipawa cha muziki ndicho kinachomtofautisha na wengine ila ubinadamu na mapito ni yale yale: “Binadamu tunapitia stresi tofauti mfano Mohammed Dewji anaweza akawa anawaza kiwanda fulani hakijakamilika, ikawa inamnyima usingizi, ila mimi stresi zangu ikawa kodi ya nyumba, mwingine ikawa pesa ya kununua chakula, huo ndio ubinadamu, kila mtu anateswa na levo ya maisha yake. Anaongeza:

“Kwa hiyo stresi za mapenzi zinanitesa kama kawaida, mimi nina moyo wa kupenda, unaweza ukapenda usipopendwa au mkapendana na wazazi ndio wakawa kikwazo na mtu akibahatika kupatana na mtu sahihi amheshimu sana, ndiyo maana katika wimbo wangu wa Amen, nimeelezea uhalisia wa maisha yangu niliyoyapitia kwa asilimia kubwa, nasisitiza watu maarufu wanaonyesha maisha ambayo wanayataka jamii ijue hasa kuhusu kazi zao, ila yapo ambayo hawayajui kabisa, wakati mwingine lile tabasamu tunaloonyesha majukwaani linaficha maumivu makali tukiwa wenyewe, tunaumwa, tunatunza familia, tunakopa na kudaiwa kama wengine.”