Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walker: Nitafuta tatoo ya mataji Man City

WALKER Pict

Muktasari:

  • Walker, mwenye umri wa miaka 36, ndiye mchezaji wa kwanza wa zamani wa City kuzungumzia hadharani sakata hilo, huku klabu hiyo ikikabiliwa na tuhuma zinazohusisha zaidi ya ukiukaji 100 wa kanuni za kifedha na ikiendelea kupinga uamuzi huo kupitia rufaa.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa zamani wa Manchester City, Kyle Walker amesema atalazimika kuondoa tattoo yake inayoadhimisha mataji manne mfululizo ya Ligi Kuu England iwapo klabu hiyo itanyang’anywa mafanikio hayo kutokana na sakata la ukiukaji wa kanuni za kifedha.

Walker, mwenye umri wa miaka 36, ndiye mchezaji wa kwanza wa zamani wa City kuzungumzia hadharani sakata hilo, huku klabu hiyo ikikabiliwa na tuhuma zinazohusisha zaidi ya ukiukaji 100 wa kanuni za kifedha na ikiendelea kupinga uamuzi huo kupitia rufaa.

Akizungumzia uwezekano wa kufuta tattoo hiyo, beki huyo wa kulia, ambaye kwa sasa anakipiga Burnley katika Championship, amesema: “Huenda ikabidi nifanye hivyo.”

Walker, aliyekuwa nahodha wa City, amesema hawezi kupuuza ukweli kwamba klabu hiyo imepatikana na hatia, ingawa mchakato wa rufaa unaendelea.

WALK 01

“Tusifiche ukweli kwamba wamepatikana na hatia, lakini wanaendelea na rufaa. Kama mchezaji, ninachoweza kusema ni kwamba tulichofanya ni kwenda uwanjani na kucheza soka letu bora kama timu. Nitatetea wachezaji kwa maisha yangu yote,” amesema.

Ameongeza kuwa mafanikio waliyoyapata katika kipindi hicho yalikuwa ya kipekee na huenda yasiwe rahisi kurudiwa tena.

“Ninahisi kwamba tulichofanya na tulichofanikiwa katika kipindi hicho kilikuwa cha kushangaza na huenda kisirudiwe tena. Lakini ukiangalia kwa mtazamo wa mtu aliye nje ya klabu, mambo hayaonekani vizuri na tunapaswa kuyazungumzia,” amesema Walker.

WALK 02

Manchester City inakabiliwa na uwezekano wa kuchukuliwa hatua kali, ikiwamo kufukuzwa kwenye Ligi Kuu England, kutokana na madai ya kuongeza mapato kwa zaidi ya pauni milioni 900 kupitia mikataba ya udhamini inayodaiwa kuhusishwa na ufadhili wa serikali kinyume cha kanuni.

Ingawa uamuzi yanayohusiana na tuhuma hizo yanahusu kipindi cha mwaka 2009 hadi 2018, adhabu zinazoweza kutolewa zinaweza kuathiri pia mafanikio ya City ya kutwaa mataji manne mfululizo ya ligi kati ya mwaka 2020 na 2024.

Walker, aliyekuwa akishiriki kipindi cha talkSPORT Drive! pamoja na Andy Goldstein, amesema anatumaini hatalazimika kufuta tattoo hiyo.

“Ni wachache tu kati yetu tunaoweza kusema tulishinda mataji manne mfululizo. Nitajaribu kuihifadhi, lakini natumaini hatutanyang’anywa mafanikio hayo,” amesema.

WALK 03

Katika pigo jingine kwa klabu hiyo, ombi la kupata taarifa chini ya sheria ya uhuru wa kupata habari limeibua maelezo kuhusu mkataba wa haki za kutumia jina la uwanja wa City.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa wamiliki wa klabu kutoka Abu Dhabi walipata mkataba wa pauni milioni 10 kwa mwaka kutoka Etihad Airways, shirika la ndege linalofadhiliwa na serikali, kwa haki za kutumia jina la uwanja wa timu hiyo.