Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

China ilivyomfungulia Rany Kida mlango wa dili

RANY Pict

Muktasari:

  • Mikataba imekuja baada ya shoo aliyoifanya kwenye sherehe za sikukuu katikati ya msimu zilizofanyika katika nchi mbalimbali, ikiwemo Tanzania na jamii ya Wachina. Baada ya sikukuu hiyo, shoo aliyoifanya dansa huyo ilipostiwa na kituo cha China Culture Center, ambapo amepata fursa za kutakiwa kufanya kazi na kampuni za China zilizopo nchini.

KUNA milango ikifunguka, msanii hatakiwi kusubiri mtu amsukumie, bali kuingia. Hilo linaonekana sasa kwa dansa Rany Kida, ambaye safari yake ya burudani imeanza kugusa upande mwingine wa biashara kupitia kampuni za China zilizopo Tanzania.

Mikataba imekuja baada ya shoo aliyoifanya kwenye sherehe za sikukuu katikati ya msimu zilizofanyika katika nchi mbalimbali, ikiwemo Tanzania na jamii ya Wachina. Baada ya sikukuu hiyo, shoo aliyoifanya dansa huyo ilipostiwa na kituo cha China Culture Center, ambapo amepata fursa za kutakiwa kufanya kazi na kampuni za China zilizopo nchini.

Rany Kida, ambaye amekuwa akijijenga taratibu katika ulimwengu wa dansi, sasa yupo kwenye mazungumzo na kampuni hizo kuhusu mikataba na fursa za kibiashara.

Dansa huyo anasema baadhi ya kampuni zimeonyesha nia ya kufanya kazi naye katika miradi yao, ingawa mazungumzo bado yanaendelea na hakuna makubaliano ya mwisho yaliyowekwa wazi.

Akizungumzia hatua hiyo, Rany Kida anasema: “Kingine ni kwamba kuna baadhi ya mikataba na kampuni za China ambazo zipo hapa Tanzania, na kampuni hizo zinataka tufanye kazi pamoja pia. Kwa hiyo, kwa sasa hivi ni vitu hivyo viwili tu.”

Hii ni hatua nyingine katika safari yake ya kupanua jina lake, akitoka kwenye jukwaa la dansi na kuanza kuangalia namna kipaji chake kinavyoweza kuwa daraja la kufikia fursa kubwa zaidi.


RAN 01

DILI ZIKO MEZANI

Kwa mujibu wa Rany Kida, mazungumzo yake na kampuni za China yanahusu mikataba na shughuli mbalimbali za kibiashara.

Kwa sasa, bado hajafunguka kuhusu thamani ya dili hizo wala muda wa utekelezaji wake, kwa kuwa mazungumzo bado hayajafikia mwisho.

Lakini jambo moja ni kwamba kampuni hizo zimeona nafasi ya kufanya kazi naye na hilo linampa dansa huyo fursa nyingine ya kuonyesha kuwa dansi inaweza kuwa zaidi ya kupanda jukwaani na kucheza.

Katika tasnia ambayo wasanii sasa wanatafuta njia mbalimbali za kugeuza umaarufu na vipaji kuwa biashara, Rany Kida anaonekana kuanza kuucheza mchezo huo kwa upande wake.


RAN 02

SHOO YA CHINA

Na siyo dili pekee zinazomweka Rany Kida kwenye ramani hiyo. Dansa huyo pia amesema anaendelea na maandalizi ya shoo mbalimbali, huku moja kati ya fursa hizo ikiwa inahusisha China.

Hata hivyo, shoo hiyo bado haijafikia hatua ya mwisho kwa sababu baadhi ya taratibu na mipango yake bado inaendelea kufanyiwa kazi.

Kwa hiyo, mashabiki bado wanasubiri kuona kama safari hiyo ya China itageuka kuwa shoo halisi baada ya mazungumzo kukamilika.

Wakati huo, Rany Kida anaendelea na shoo zake nyingine ndani ya Tanzania, akitengeneza nafasi zaidi za kuendelea kuonekana kwenye jukwaa.


RAN 03

CHINO KID

Katika safari hiyo, Rany Kida pia amepata sapoti kutoka kwa mwenzake kwenye sanaa, Isaya Michael, maarufu kama Chino Kidd.

Rany Kida anasema Chino Kidd alimpongeza baada ya kuona hatua ambazo amekuwa akizipiga pamoja na fursa mpya zinazoanza kujitokeza kwenye kazi yake.

Kwa dansa huyo, pongezi kama hizo zinaongeza hamasa kuendelea kusaka nafasi zaidi na kutokomea kwenye mafanikio ya jukwaani. Anataka safari iwe pana zaidi.


RAN 04

SASA NI KUINGIA

Kwa sasa, macho ya Rany Kida yako kwenye mazungumzo hayo pamoja na shoo inayohusisha China.

Iwapo makubaliano yatafikiwa, fursa hizo zinaweza kuwa hatua nyingine katika safari ya kuunganisha dansi na biashara. Hii ni kwa sababu dunia ya burudani imebadilika; kipaji pekee hakitoshi, bali namna msanii anavyoweza kukitumia kujenga fursa nyingine nayo imekuwa sehemu ya mchezo.

Rany Kida sasa anagonga mlango huo. Na kama China itafunguka kweli, huenda akaanza sura mpya ya safari yake ambayo jukwaa linaweza kuwa mwanzo tu, huku biashara ikiwa hatua inayofuata.