Simba yaifanyia mauaji 15 de Agosto, Doumbia atupia mbili
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, wakati akishangilia moja ya bao alilofunga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili ya awali dhidi ya 15 de Agosto.
Muktasari:
- Kabla ya mchezo dhidi ya 15 de Agosto, mara ya mwisho kwa Doumbia kuifungia Simba ilikuwa ni Julai 31, 2026 alipofunga dhidi ya Singida Black Stars katika Kombe la Kagame.
Baada ya kucheza mechi 11 mfululizo za Simba bila kufunga bao, mshambuliaji Ibrahim Doumbia amemaliza ukame wa mabao baada ya kuifungia mabao mawili timu hiyo leo Jumatano, Oktoba 21, 2026 katika mechi ya raundi ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwenye mechi hiyo, Simba imeibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1.
Doumbia amefunga bao hilo katika dakika ya 64 akimalizia pasi ya Anicet Oura.
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, wakati akifunga bao la kwanza kati ya mawili katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili ya awali dhidi ya 15 de Agosto.
Mara baada ya Doumbia kupokea pasi hiyo, aliwapiga chenga beki na kipa wa 15 de Agosto na kujaza mpira wavuni.
Mshambuliaji hiyo alifunga tena bao la pili katika dakika ya 87 akimalizia pasi ya Morice Abraham.
Kabla ya mechi ya leo, Doumbia aliifungia Simba bao Julai 31, 2026 katika mechi ya Kombe la Kagame dhidi ya Singida Black Stars.
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, wakati akifunga bao la kwanza kati ya mawili katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili ya awali dhidi ya 15 de Agosto.
Katika mchezo wa leo, Doumbia ameingia kutokea benchi katika dakika ya 60 akichukua nafasi ya Elie Mpanzu.
Mabao mengine ya Simba leo yamefungwa na Kaletso Makgalwa, Anicet Oura, Nathanie Chilambo na Mpanzu.
Bao pekee la kufutia machozi la 15 de Agosto limepachikwa na Alozie Uwandu.
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, wakati akifunga bao la kwanza kati ya mawili katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya pili ya awali dhidi ya 15 de Agosto.
Matokeo hayo yameiweka Simba katika nafasi nzuri na kubwa ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Simba inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote katika mechi ya marudiano Jumapili wiki hii ili itinge hatua ya makundi.