Waamuzi wenye kazi yao kombe la dunia la klabu

Muktasari:
- Michuano hiyo itashirikisha timu 32 kutoka mabara yote duniani likiwa ni jukwaa muhimu la kuonyesha ushindani wa juu kati ya mabingwa wa mashindano mbalimbali ya timu duniani.
FLORIDA, MAREKANI: KOMBE la Dunia la Klabu la Fifa 2025 lenye mfumo mpya linatarajiwa kufanyika nchini Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13, 2025.
Michuano hiyo itashirikisha timu 32 kutoka mabara yote duniani likiwa ni jukwaa muhimu la kuonyesha ushindani wa juu kati ya mabingwa wa mashindano mbalimbali ya timu duniani.
Kuelekea michuano hiyo, FifaA imeteua waamuzi 117 kutoka nchi 41 tofauti duniani.
Orodha hiyo inajumuisha waamuzi wa kati 35, wasaidizi 58 na wale wa VAR 24.
Hii hapa ni orodha kamili ya waamuzi hao na mataifa wanayotoka.
ASIA
Alireza Faghani (Australia)
Fu Ming (China)
Ma Ning (China)
Salman Falahi (Qatar)
Shaun Evans (Australia)
Ilgiz Tantashev (Uzbekistan)
AFRIKA
Mustapha Ghorbal (Algeria)
Dahane Beida (Mauritania)
Mahmoud Ashour (Misri)
Jean-Jacques Ndala (DR Congo)
Issa Sy (Senegal)
AMERIKA KASKAZINI NA KATI
Ivan Barton (El Salvador)
Drew Fischer (Canada)
Armando Villarreal (Marekani)
Said Martinez (Honduras)
Walter Lopez (Guatemala)
AMERIKA KUSINI
Wilton Sampaio (Brazil)
Facundo Tello (Argentina)
Jesus Valenzuela (Venezuela)
Leodan Gonzalez (Uruguay)
Ramon Abatti (Brazil)
ULAYA
Michael Oliver (Uingereza)
Clement Turpin (Ufaransa)
Szymon Marciniak (Poland)
Slavko Vincic (Slovenia)
Glenn Nyberg (Sweden)
Danny Makkelie (Uholanzi)
WASAIDIZI (Asia)
Anton Shchetinin (Uzbekistan)
Ashley Beecham (Australia)
Mohammad Obaid Khadim (UAE)
Afrika
Stephen Yiembe (Kenya)
Hamza Al-Fariq (Sudan)
Mutaz Ibrahim (Sudan)
Abbes Akram Zerhouni (Algeria)
Mokrane Gourari (Algeria)
Amerika Kaskazini
Kathryn Nesbitt (USA)
Brooke Mayo (USA)
David Moran (Honduras)
Henry Pupiro (Nicaragua)
Tatiana Guzman (Costa Rica)
Amerika Kusini
Rafael Alves (Brazil)
Gabriel Chade (Argentina)
Juan Soto (Paraguay)
Bruno Boschilia (Brazil)
Tulio Moreno (Brazil)
Ulaya
Gary Beswick (Uingereza)
Adam Nunn (Uingereza)
Hessel Steegstra (Uholanzi)
Tomasz Listkiewicz (Poland)
Nicolas Danos (Ufaransa)
VAR
Asia
Khamis Al-Marri (Qatar)
Omar Al Ali (Qatar)
Afrika
Jean-Jacques Ndala (DR Congo) - pia kama mwamuzi wa kati
Nouha Bangoura (Guinea)
Amerika Kaskazini
Cesar Arturo Ramos (Mexico/USA)
Walter Lopez (Honduras)
Amerika Kusini
Eduardo Cardozo (Paraguay)
Gabriel Chade (Argentina)
Ulaya
Carlos del Cerro Grande (Hispania)
Marco Di Bello (Italia)
Robert Kempter (Ujerumani)
Tomasz Kwiatkowski (Poland)
Bastian Dankert (Ujerumani)
MABADILIKO YA SHERIA, TEKNOLOJIA
Mabadiliko ya sheria yaliyopo ni pamoja na ile ya makipa ambao katika mashindano hayo hawataruhusiwa kushika mpira kwa zaidi ya sekunde 8 na kwamba wakikiuka kanuni hiyo timu pinzani itapewa kona. Vilevile kila mwamuzi atafungwa kamera mbele ya kifua chake ambayo itatumika kama sehemu ya majaribio katika baadhi ya mechi za hatua ya makundi na robo fainali ili kusaidia uwazi na elimu ya waamuzi. Pia kutakuwa na mfumo mpya wa mpira kuwekwa kifaa maalumu ndani kwa ajili ya kusaidia kutoa uamuzi matukio ya kuotea kwa haraka.