Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vurugu zatikisa ufunguzi wa Kombe la Dunia, Mexico

Muktasari:

  • Wakati shamrashamra za ufunguzi zikiendelea ndani ya uwanja huo maarufu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 87,000 unaojulikana kama Estadio Azteca, matukio tofauti yalikuwa yakitokea nje ya milango yake.

MEXICO CITY, MEXICO: VURUGU ziliibuka wakati wa ufunguzi wa Fainali za Kombe la Dunia 2026, baada ya waandamanaji kupambana na polisi wa kutuliza ghasia nje ya Uwanja wa Mexico City uliokuwa ukitumika kwa mechi hiyo kati ya Mexico na Afrika Kusini.

Wakati shamrashamra za ufunguzi zikiendelea ndani ya uwanja huo maarufu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 87,000 unaojulikana kama Estadio Azteca, matukio tofauti yalikuwa yakitokea nje ya milango yake.

Daily Mail ilishuhudia vurugu zikizuka huku waandamanaji, ambao baadhi yao walidaiwa ni familia za watu waliopotea wakati wa vita dhidi ya magenge ya dawa za kulevya nchini humo wakijaribu kuvunja vizuizi na kuingia uwanjani kabla ya kukabiliwa kwa nguvu na polisi.

Inaelezwa dakika 10 kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, waandamanaji hao walifika eneo la uwanja kutoka upande wa Kaskazini Mashariki wakijaribu kuingia karibu na eneo la uwanja, huku wakirusha fataki na mawe kwa polis na waliharibu lori lililokuwa limeegeshwa karibu na eneo hilo.

Polisi wa kutuliza ghasia waliongezwa haraka eneo hilo na kuwatimua wakitumia mabomu ya machozi.

Baadaye, Sekretarieti ya Usalama wa Raia ya Jiji la Mexico (SSC) ilithibitisha kuwa kulikuwa na makundi mawili ya waandamanaji yenye watu takribani 800 kila moja na karibu watu 200 waliokuwa wamejifunika nyuso wakijitenga na kuanzisha vurugu.

Wakati vurugu hizo zikiendelea nje ya uwanja, ndani mashabiki walikuwa wakishangilia na kusherehekea kuanza kwa mechi ya ufunguzi, hali iliyoonyesha tofauti kubwa kati ya matukio yaliyokuwa yakitokea ndani na nje ya uwanja.

Baada ya mechi kuanza na vurugu za awali kudhibitiwa, polisi wa kutuliza ghasia walipangwa kuimarisha usalama. Hata hivyo, hofu juu ya usalama bado ipo kwani maandamano hayo yamekuwapo kwa muda mrefu katika nchi hiyo.