Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VUNJA MBAVU! Fahamu kuhusu mashindano ya kucheka

MBAVU Pict

Muktasari:

  • Hali hiyo imesababisha baadhi ya watu kubuni mashindano ya kucheka ambayo sasa yanafanyika sehemu mbalimbali duniani.

ODESSA, UKRAINE: KATIKA dunia ya sasa ambayo tatizo la changamoto za afya ya akili na msongo wa mawazo limezidi kupamba moto na moja kati ya mambo ambayo yanaonekana kupotea ni furaha kwa watu wengi.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya watu kubuni mashindano ya kucheka ambayo sasa yanafanyika sehemu mbalimbali duniani.

Leo tumekusogezea undani wa mchezo huu kuanzia asili yake, kanuni, sheria na hata mabingwa wao waliowahi kushinda tangu kuanza kwa kufanyika kwa mara ya kwanza hadi sasa ikiwa imefikia miaka 16.

MBAV 01

ASILI YA MASHINDANO

Wazo la Mashindano ya Kucheka lilibuniwa na mtayarishaji wa filamu Albert Nerenberg kutoka Canada ambaye alipata wazo hilo baada ya siku moja kuhudhuria mchezo wa kupigana na baada ya pambano kuisha akaona wapiganaji wakipeana mikono huku wakicheka.

Kupitia kicheko na pambano hilo alipata wazo la kuanzisha mchezo huo kwani kama kupigana ngumi kwenye uso ni mchezo na ukiisha watu huwa wanafurahia, kwa nini kucheza isiwe ni mchezo pia.

Inaelezwa mpango rasmi ukaanza mwaka 2010, huko Canada na Ukraine katika Jiji la Odessa.

Hata hivyo, ripoti nyingine zinaeleza kwamba mchezo huo ulibuniwa mwaka 2008, wakati ambao nchi nyingi barani Ulaya zilikuwa zinakumbana na matatizo ya kiuchumi, hivyo wanasaikolojia wakaubuni ikiwa ni sehemu ya kujaribu kurudisha furaha kwa raia wa bara hilo.

Mashindano ya mwanzo  kabisa yaliyofanyika Ukraine yalihusisha washiriki 17 na ilipofikia mwaka 2013 mchezo huo ulisambaa nchi mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Moldova.

Mchezo huu ulipata umaarufu mkubwa kwa sababu ulionekana kuwa ni tiba kwa washiriki na wale mashabiki na tafiti za kisayansi zilizofanya zikaonyesha kuwa kicheko hupunguza uzalishaji wa homoni zinazosababisha msongo wa mawazo kwa asilimia 25.

Hospitali na wataalamu wa afya ya akili wakaanza kutumia mashindano hayo  kama sehemu ya tiba mbadala.

Baada ya hapo kikaundwa chama maalumu cha kusimamia mashindano yote duniani kiitwacho World Laughter Sports Federation (WLSF).

MBAV 02

AINA YA VICHEKO

Mashindano haya yana aina nne kuu za kicheko, cha kwanza ni kicheko cha asili ambacho mshiriki anatakiwa kukitoa bila ya kujilazimisha au kuigiza inabidi kije tu chenyewe.

Mshindi wa kicheko cha aina hii huwa ni yule aliyecheka muda mrefu zaidi kuliko mwenzake.

Kicheki cha aina ya pili ni kile ambacho siyo asili bali cha uigizaji na mshiriki atatakiwa kutumia mbinu mbalimbali ili kujilazimisha kucheka. Hii ndiyo aina maarufu zaidi.

Vilevile kuna kicheko cha Contagious Laughter ambacho msingi wake ni kucheka hadi mashabiki nao wacheke na huwa kuna vifaa maalumu vya kupima watazamaji wanacheka kwa kiwango gani.

Mwisho ni kicheko cha Endurance Laughter ambacho mshiriki atatakiwa kucheka hadi mwisho na mshindi ni ambaye atacheka bila ya kunyamaza kuliko wengine. Mara nyingi huitwa kicheko cha Marathon.

Mtu ambaye anashikilia rekodi kubwa zaidi duniani katika aina hii ya kicheko ni yule kutoka India aliyecheka kwa dakika 42 mfululizo, akifanya hivyo mwaka 2019.

MBAV 03

KANUNI NA SHERIA

Mashindano yanaongozwa na miongozo kutoka chama kinachosimamia mchezo huo na kuna masharti kadhaa ambayo washiriki wanatakiwa kuyafuata.

Kwanza kila mchezaji anatakiwa kuwasilisha cheti cha afya ya moyo na mapafu, hairuhusiwi kutumia dawa au kemikali zinazoongeza hisia za kucheka, sauti hairuhusiwi kupandishwa kwa vifaa vya kielektroniki, hairuhusiwi kutumia lugha chafu au yenye kudhalilisha.

Ikiwa itakuwa ni mashindano ya timu, lazima kuwe na washiriki watatu hadi sita kwa kila timu. Mchezaji anatakiwa kutumia katika sekundi 30 hadi dakika moja kujiandaa na kuanza kucheka.

MBAV 04

TARATIBU ZA MASHINDANO

Mashindano huandaliwa kwa siku tatu hadi nne.

Siku ya kwanza huwa ni kwa ajili ya maandalizi na mafunzo  na washiriki hufanyiwa vipimo vya afya, ukaguzi wa ubora wa kicheko. Siku ya pili hufanyika mchujo na kawaida washiriki takribani 200 hupunguzwa hadi 30. Siku ya tatu huwa nusu fainali na fainali.

MBAV 05

MABINGWA WA MUDA WOTE 2010-2024

Mwaka              Mshindi                        Nchi

2010               Alexei Morenko             Ukraine

2011               Sanjay Patel                   India

2012                Lidia Bowman               England 

2013                Team India                     India

2014                 Team Brazil                   Brazil

2015                  Peter Williams             Australia

2016                  Team Japan                 Japan

2017                   Mercy Okon                 Nigeria

2018                   Team USA                    Marekani

2019                    Rajesh Kumar             India

2021                    Team Germany           Ujerumani

2022                     Team India                  India

2023                      Maria Rodriguez        Mexico

2024                      Team Ukraine              Ukraine


MBAV 06

ZAWADI KWA WASHINDI

Mashindano haya yamekuwa na wadhamini wakubwa kama kampuni za vinywaji, hoteli na mashirika ya afya ya akili duniani.

Zawadi zinazotolewa mara nyingi huwa ni pesa, medali na vyeti. Pesa hizo huanzia Dola 10,000 hadi Dola 25,000.

Baadhi ya washiriki pia hupata nafasi ya kuajiriwa katika kampuni za Komedi na vipindi mbalimbali vya televisheni.

Kwa upande wa timu za taifa zinazoshinda huwa zinapata medali na zawadi ya fedha zinazokadiriwa kufikia Dola 50,000.

Kicheko hupunguza msongo wa mawazo kwa asilimia 25 hadi 45.

Huongeza kinga ya mwili kwa asilimia 12 hadi 15. Huongeza furaha na kujiamini.