UNA USINGIZI? Fahamu mashindano ya kulala duniani
Muktasari:
- Baada ya kuanzishwa katika nchi hizo, tukio hilo lilienea katika mataifa mengine kama, Japan, Korea Kusini, Ufaransa na Marekani.
AMSTERDAM, UHOLANZI: HAKUNA taarifa kamili juu ya wapi rasmi yalipoanzia ingawa ripoti nyingi zinaeleza yalianzia Uholanzi mwaka 2010 katika siku ya maadhimisho ya kulala duniani.
Mji wa Madrid, Hispania pia uliwahi kufanya tukio kama hili, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha watu kulala.
Baada ya kuanzishwa katika nchi hizo, tukio hilo lilienea katika mataifa mengine kama, Japan, Korea Kusini, Ufaransa na Marekani.
Kwa sasa mashindano haya hufanyika mara moja au mbili kwa mwaka katika miji mbalimbali lakini zaidi huandaliwa Hispania, Japan, Korea Kusini na Uholanzi ambako ndiko yamepata umaarufu zaidi.
SHERIA ZA MASHINDANO
Mshiriki lazima alale kweli na usingizi huwa unapimwa kwa vifaa maalum kama sleep monitors, heart rate sensors, na movement detectors.
Mara nyingi pia mashindano huchukua dakika 20 hadi 30 kwa yale ya muda mfupi lakini kua mengine huchukua kati ya lisaa au masaa mawili..
Kawaida mshindi wa mashindano haya hupatikana kwa majaji kuangalia mambo kadhaa ikiwemo muda ambao mshiriki ameutumia hadi kulala, jinsi ambavyo amelala, muda ambao ameutumia usingizini, mapigo ya moyo na utulivu wake wake wakati wa kulala.
Mshiriki haruhusiwi kutumia dawa za usingizi au pombe kabla ya mashindano, kusikiliza muziki ambao utamsaidia kulala au kuomba mtu akubembeleze au kukupiga mgongoni kama sehemu ya kukusaidia kulala.
Washiriki hulala kwenye sehemu za wazi lakini sharti moja wapo ni kuwe na ukimya. Mara katika mashindano makubwa yale ya Dunia mashabiki huwa wengi wakitazama mchezo huo lakini hutakiwa kunyamaza wakati shindano likiendelea ili kuwapa utulivu washindani.
Kabla ya mashindano kuanza, washiriki hupewa dakika tano hadi 10 za kutuliza akili kabla ya mashindano kuanza.
ZAWADI ZA WASHINDI
Zawadi hutofautiana kulingana na mashindano. Kwa kawaida, washindi hupata
Fedha, kati ya Dola 1,000 hadi 10,000 pamoja na vyeti, medali, magodoro, mito, na Safari za bure kwenda kupumzika hoteli za kitalii na muda mwingine mabingwa huwa wanapata matangazo ya bidhaa za usingizi
Katika mashindano makubwa kama ya Barcelona Sleep Expo zawadi kwa mshindi hufikia Euro 15,000.
WASHINDI MAARUFU WALIOWAI KUNG’ARA
Aina Tanaka - Japan
Alishinda kwa kulala ndani ya sekunde 57 tu baada ya kuanza mashindano.
Alipata alama za juu za 'kulala muda mrefu' kwa dakika 22 mfululizo.
2. Maria Gonzalez - Hispania
Huyu ni mshindi wa mashindano ya Barcelona Sleep Fest mwaka 2018, alilala bila ya kujisogea kwa dakika 30.
3. Park Ji-Hoon - Korea Kusini
Mshindi huyu wa Asia Sleep Cup 2021, alishinda mashindano hayo kwa kupata alama za juu zaidi za kulala kwa utulivu.
4. Timu ya taifa ya Uholanzi
Walishinda taji la timu bora ya kulala katika mashindano ya dunia ya mwaka 2022.
NAMNA MASHINDANO YANAVYOENDESHWA
Kabla ya washiriki kuingia katika mashindano, hufanyiwa uchunguzi wa afya ambapo wahusika hupimwa kama wana matatizo ya usingizi kama sleep apnea, ambayo yanaweza kuathiri uhalali wa matokeo.
Kawaida pia kuna aina nne za mashindano, yakwanza ni yale ya mshiriki mmoja mmoja, vikundi, Power nap contest, Deep sleep challenge, Sleep endurance marathon.
Katika aina hizi za mashindano, miongoni mwa yale yanayoonekana magumu ni yale ya Power nap contest ambayo mshiriki huwekewa muda maalumu wa kulala lakini wakati amelala huwa akumbana na usumbufu kama kusikilizishwa sauti za Mbu au watu kunon'gona katika masikio yake. Aina hii ya mashindano mara nyingi hufanyika Korea Kusini.
Mshiriki anatakiwa kulala kati ya dakika saba hadi 10 kabla ya mashindano kuanza, lakini baadhi ya washiriki huweza kulala ndani ya sikunde 40 hadi 50 baada ya kuanza kwa mashindano.