Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TOTAL FUTBOL: Ukweli unaoumiza kuhusu Man United

UKWELI Pict

Muktasari:

  • Kinachoelezwa kwa sasa ile ofa ya msosi wa bure wa mchana kwa wachezaji wote sasa umepunguzwa na jambo hilo linawahusu pia makocha wa kikosi hicho pamoja na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya ufundi.

MANCHESTER, ENGLAND: BILIONEA Sir Jim Ratcliffe anafyeka tu gharama moja baada ya nyingine kwa lengo la kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima na sasa  panga limehamia kwenye mgahawa uliopo kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United huko Carrington.

Kinachoelezwa kwa sasa ile ofa ya msosi wa bure wa mchana kwa wachezaji wote sasa umepunguzwa na jambo hilo linawahusu pia makocha wa kikosi hicho pamoja na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya ufundi.

Man United kwa sasa inapambana katika kila namna kupunguza gharama. Hata mechi ya vijana ya Kombe la FA na Man United ilishinda 5-1 kwenye robo fainali dhidi ya Chelsea, kwa kawaida ilipaswa kuchezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, lakini badala yake ilipelekwa uwanjani Leigh Sports Village ili tu kuokoa Pauni 8,000.

Katakata hiyo ya kupunguza gharama kwenye kikosi inaonekana kuvuruga baadhi ya mambo kikosini.

UK 01

Man United hata baada ya kutokea nyuma na kupata sare ya mabao 2-2 na Everton kwenye mechi iliyopita ya Ligi Kuu England, kinachotokea nje ya uwanja kimekuwa na athari kubwa uwanjani pia.

Mabao ya kipindi cha kwanza ya mastaa Beto na Abdoulaye Doucoure yaliifanya Everton kuongoza 2-0 hadi mapumziko, kabla ya kusawazisha kupitia kwa Bruno Fernandes na Manuel Ugharte.

Kocha wa sasa wa Man United, Ruben Amorim ameshakiri yupo kwenye kazi ya kuinoa timu ya hovyo zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya klabu hiyo.

Dhidi ya Everton, inayonolewa na kocha wa zamani wa Man United, David Moyes miamba hiyo ya Old Trafford ilikuwa na bahati tu kupata sare kwa sababu wapinzani wao walistahili kupata penalti kwenye dakika 93, lakini walinyumwa na VAR.

UK 02

Lakini, msaidizi wa bilionea Ratcliffe, Sir Dave Brailsford alisema sare hiyo imewanufaisha kidogo kwa sababu kinyume cha hapo mambo yangekuwa mabaya zaidi.

Mambo yalivyo kwa sasa, hata Man United ya Moyes, ambaye alifutwa kazi miaka 11 iliyopita kutokana na matokeo mabaya, haikuwa mbaya kiasi hiki.

Man United ya sasa haina wachezaji wenye ubora unaostahili kuwapo kwenye timu kubwa aina ya miamba hiyo.

Mpango wa kwanza wa bilionea Ratcliffe ni kupiga chini wachezaji wote na kuanza upya, huku pia likiwa ni suala la kupunguza gharama kubwa za mishahara inayolipwa kwa wachezaji ambao mchango wao haukidhi.

Kitu kibaya ni Man United haitapata hata nusu ya gharama ya kikosi ilichokipanga kwenye mechi hiyo ya Everton, iliyokaribia Pauni 500 millioni.

Mtazame Casemiro, kwenye umri wa miaka 33 anavyocheza kwenye sehemu ya kiungo. Mbrazili huyo mshahara wake ni Pauni 350,000 kwa wiki na aliweka wazi anataka kubaki Man United hadi mwisho wa mkataba wake na itakuwa mwisho wa msimu ujao.

UK 03

Hana chaguo jingine zaidi ya kusema hivyo. Hakuna klabu yoyote itakayothubutu kwenda kumsajili mchezaji wa aina hiyo. Casemiro amechoka, anavyocheza kwa sasa, si yule aliyeshinda mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na kikosi cha Real Madrid.

Hata timu ambazo zimekuwa zikisajili kwa pesa nyingi kutoka kwenye Saudi Pro League haziwezi kukubali kumlipa Casemiro mshahara kama anaolipwa kwa sasa Man United. Hata Casemiro mwenyewe analifahamu hilo na ndiyo maana ametulizana Old Trafford kukinga tu pesa hata kama hachezi.

Straika, Rasmus Hojlund, aliyegharimu ada ya uhamisho ya Pauni 64 milioni hana anachofanya cha maana kwenye timu, amekuwa mzururaji tu uwanjani, huku mshahara wake ukiwa Pauni 85,000 kwa wiki, ambao ataendelea kuukinga hadi mwisho wa msimu wake 2028.

Hojlund hajafunga bao lolote kwenye mechi 16 mfululizo, kiwango kimeshuka sana kiasi kwamba hata timu ya League One itasita kumlipa mchezaji huyo mshahara wa Pauni 5,000 kwa wiki.

Man United ina mastaa inayowalipa pesa nyingi sana, lakini thamani ya pesa wanazolipwa haionekani uwanjani.

Tazama kile kinachofanywa na mabeki wa kati wa timu hiyo, akiwamo Harry Maguire na Matthijs de Ligt.

Kwenye mechi ya Everton, mabeki hao walihusika moja kwa moja na mabao ya wapinzani na walikaribia kuifanya Man United kupoteza mchezo huo baada ya kumvuta jezi Ashley Young ndani ya boksi, shukrani tu kwa VAR ilipindua uamuzi wa mwamuzi wa kati wa kutaka ipigwe mkwaju wa penalti.

Mwaka 2023, Maguire aligoma kwenda West Ham United kwa sababu tu alitakiwa ashushe mshahara wake.

UK 04

Man United ilishakubali ofa ya Pauni 20 milioni kutoka kwa West Ham, lakini mchezaji Maguire, hakuwa tayari kushusha mshahara wake ili akajiunge na timu hiyo ya London, badala yake aliamua kubaki zake Old Trafford kuendelea kufaidi matunda ya kulipwa mshahara mkubwa bila ya matokeo mazuri uwanjani.

Nahodha huyo wa zamani ameongeza mwaka mmoja kwenye mkataba mwezi uliopita na analipwa Pauni 195,000 kwa wiki. Lakini, ukweli Maguire, 31, alipaswa kuachwa na Man United miezi 18 iliyopita- kama tu Man United ingekuwa tayari kumlipa Pauni 15 milioni alizotaka ili aondoke.

Bilionea Ratcliffe, ambaye amewekeza Pauni 1.03 bilioni na kusimamia masuala ya kisoka kwenye klabu hiyo kwa mwaka mmoja sasa, anapasuka kichwa namna ya kuondoa wachezaji ambao walisainishwa mishahara mikubwa huko nyuma, wakati viwango vyao vya uwanjani ni hovyo kabisa.

Kinachoelezwa ni kwamba Brailsford kwa sasa ndiye anayepambana na suala hilo na kuondoa wachezaji wenye mchango hafifu usiostahili kwa timu hiyo ya Old Trafford.

Na kwa sababu hakuna mpango mbadala wa kocha Amorim kwenye kubadili mtindo wake wa uchezaji na kung’ang’ania fomesheni ya 3-4-3, ambayo inawapa shida wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kwa sasa, hilo halina ubishi ni lazima waondoke ili waje watakaoweza kuendana na mtindo huo wa uchezaji.

Man United kwa sasa haipo kwenye janga la kushuka daraja, lakini kama itabaki na wachezaji waliopo kwa sasa na kuendelea kutumia mtindo huo wa 3-4-3, basi msimu ujao watakuwa kwenye janga la kushuka.

Timu ina deni la Pauni 1 bilioni, hivyo kwa kocha Amorim kusajili mchezaji mpya kwenye timu hiyo ni lazima auze waliopo kwanza. Wasiwasi uliopo ni kama wachezaji mizigo wakikosa timu za kuwasajili, je bilionea Ratcliffe atalipa fidia kuvunja mikataba yao?

Moyes, alifutwa kazi kama kocha wa Man United mwaka 2014 kwa sasa yupo kwenye klabu nyingine na mambo yake yanaweza kuwa mazuri kuliko alipokuwa Old Trafford.

Timu yake ya Everton kwa sasa itahamia kwenye uwanja mpya wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 52,888, Bramley-Moore Dock - ambao utampa fursa ya kuingiza mapato zaidi ya Pauni 80 milioni kwa mwaka, huku mmiliki mpya wa timu hiyo, The Friedkin Group ina utajiri wa Pauni 10 bilioni na Everton haina madeni, hivyo itasajili dirisha lijalo.

Kwenye dirisha lijalo, Moyes atakuwa na pesa ya kusajili, wakati klabu yake hiyo ya zamani ya Man United itakuwa inahaha kuwa na wachezaji ghali kwenye kikosi ambao hawauziki.

Bilionea Ratcliffe amechukua timu na kushughulikia masuala ya kisoka, lakini si kwenye kulipa madeni ya timu hiyo, tofauti na ofa ya mzabuni mwenzake waliokuwa wakichuana kuinunua klabu hiyo, sheikh Jassim, ambaye alitaka kuinunua klabu hiyo jumla kutoka kwenye mikono ya wanafamilia ya Glazer na kulipa madeni yote.