Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya mastraika, viungo Ballon d ‘or

TUZO Pict

Muktasari:

  • Mshindi wa mwaka jana, Ousmane Dembele anaweza kutetea tuzo hiyo?, Lakini kwa hali ilivyo sasa, kuna uwezekano mkubwa wa kuona mchezaji mpya akitwaa taji hilo mwaka huu.
  • Rodri aliyeshinda Ballon d’Or mwaka 2024, amejiongezea nafasi ya kuwania tuzo hiyo baada ya kuiongoza timu yake kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia msimu huu kwa kiwango bora. 

BAADA ya utawala wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kumalizika sasa tuzo ya Ballon d’Or haina mwenyewe jana ilitangazwa orodha ya wachezaji 30, na macho ya mashabiki yakielekezwa kwa mchezaji atakayetawazwa kuwa bora zaidi duniani.

Mshindi wa mwaka jana, Ousmane Dembele anaweza kutetea tuzo hiyo?, Lakini kwa hali ilivyo sasa, kuna uwezekano mkubwa wa kuona mchezaji mpya akitwaa taji hilo mwaka huu.

Rodri aliyeshinda Ballon d’Or mwaka 2024, amejiongezea nafasi ya kuwania tuzo hiyo baada ya kuiongoza timu yake kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia msimu huu kwa kiwango bora. Harry Kane, Lamine Yamal na Michael Olise pia wanatajwa kuwa miongoni mwa wagombea wenye nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo.

Lionel Messi naye alitarajiwa kuwa mmoja wa wanaowania tuzo hiyo kutokana na kuendelea kung’ara katika Kombe la Dunia, lakini kushindwa katika fainali kunaaminika kumepunguza kwa kiasi kikubwa nafasi yake ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tisa, jambo ambalo lingemuweka katika rekodi mpya.

TUZ 02

Katika kundi hilo la nyota 30 wengi walioteuliwa ni wale wanaocheza nafasi za ushambuliaji na kiungo ingawa wapo mabeki na makipa wachache.

Orodha ya jumla ya washindani wa tuzo hiyo inawajumuisha Jude Bellingham, Pau Cubarsi, Ousmane Dembele, Marc Cucurella, Bruno Fernandes, Luis Diaz, Gabriel Magalhaeis, Erling Haaland, Harry Kane, Achraf Hakimi,

Washindani wa tuzo ya Kipa Bora wa Kiume ya mwaka ni Yassine Bounou (Morocco), Thibaut Courtois (Ubelgiji), Gregor Kobel (Switzerland), Joan Garcia (Hispania), Eduardo Mendy (Senegal), Emiliano Martinez (Argentina), David Raya (Hispania), Vozinha (Cape Verde), Matvey Safonov (Russia) na Unai Simon (Hispania).

Wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume kijana ni Eli Junior Kroupi (Ufaransa), Pau Cubarsi (Hispania), Yan Diomande (Ivory Coast), Ayyoub Bouaddi (Morocco), Kerim Alajbegovic (Bosnia&Herzegovina), Lennart Karl (Ujerumani), Lamine Yamal (Hispania), Johan Manzambi (Switzerland), Ibrahim Maza (Algeria) na Warren Zaire-Emery (Ufaransa).

TUZ 01

Kuna washindani watano wa tuzo ya Kocha Bora wa timu za kiume wa mwaka ambao ni Mikel Arteta (Arsenal), Luis de la Fuente (Hispania), Unai Emery (Aston Villa), Vincent Kompany (Bayern Munich) na Luis Henrique (PSG).

Upande wa Kocha Bora Wanawake kuna Jonatab Giraldez (Olympique Lyonnes), Andres Jeglertz (Manchester City), Nils Nielsen (Japan), Pere  Romeu (Barcelona) na Elena Sadiku (Celtic/BK Hacken).