Villa yatakata ugenini, Celtic, Rangers hali mbaya Europa League
Muktasari:
- Mechi hizo zimekuwa na msisimko wa aina yake kutokana na kila timu kuhitaji ushindi. Hapa kuna ripoti ya mechi hizo ikionesha kilichotokea.
USIKU wa Ulaya umeendelea Oktoba 2, 2025 ambapo mechi 36 za michuano ya Europa League na Europa Conference zimechezwa.
Mechi hizo zimekuwa na msisimko wa aina yake kutokana na kila timu kuhitaji ushindi. Hapa kuna ripoti ya mechi hizo ikionesha kilichotokea.
ROMA 0-1 LILLE
Kipa wa Lille, Berke Özer, aliokoa penalti tatu mfululizo katika dakika za mwisho za ushindi kwenye Europa League dhidi ya Roma.
Klabu hiyo ya Ufaransa ilitangulia mapema kupitia bao la dakika ya 6 la Hakon Arnar Haraldsson, ambaye alitumia kosa la wapinzani wao kufunga.
Hata hivyo, wenyeji Roma walipata nafasi bora ya kusawazisha dakika ya 80 baada ya Aissa Mandi kushika mpira na refa kutoa penalti.
Mbadala Artem Dovbyk alipewa jukumu la kupiga mkwaju huo, lakini Özer aliokoa. Refa Erik Lambrechts akaamuru marudio baada ya kipa huyo kuonekana kutoka katika mstari mapema.
Dovbyk akapiga tena, lakini mara nyingine akazuiwa na Özer, ingawa safari hii refa akasema kuna watu waliingia ndani mapema kabla ya mpira kupigwa.
Mara ya tatu jukumu likahamishiwa kwa Matias Soule, naye pia akazuiwa na Özer, huku safari hii refa hakuamuru irudiwe na kuipa Lille ushindi.
Baada ya mechi, Kocha wa Roma, Gian Piero Gasperini, amesema: "Sijawahi kuona penalti tatu zikikosekana mfululizo katika mechi moja. Hali ile ilikuwa ya kipekee na ya bahati mbaya, ambayo mwishowe iliharibu matokeo yetu."
FEYENOORD 0-2 ASTON VILLA
John McGinn aliendelea na mwendelezo wake wa kufunga baada ya kuiwezesha Aston Villa kupata ushindi wa kuvutia dhidi ya Feyenoord kwenye michuano ya Europa League.
Villa ilianza kampeni yake Ulaya wiki iliyopita ikiwa haijapata ushindi katika mechi sita mfululizo. Lakini mabao matatu katika mechi tatu kutoka kwa nahodha wake yameipa ushindi mfululizo kwenye Europa League, sambamba na ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu.
McGinn alifunga bao la pili jijini Rotterdam baada ya mpira kuangukia miguuni mwake kufuatia mbio za Donyell Malen, ambaye alizuiwa na wachezaji watatu wa Feyenoord alipokuwa akipenya kwenye eneo la hatari.
Awali, Emiliano Buendia aliwafungia Villa bao la kwanza dakika ya 61 kwa shuti la mzunguko baada ya kipindi cha kwanza kilichokuwa cha kasi na chenye uamuzi tata kutoka kwa waamuzi.
Wachezaji wa Unai Emery walionekana kukerwa na uamuzi wa refa wakati Anel Ahmedhodzic alipomchezea faulo Ollie Watkins dakika ya 13 huku mshambuliaji huyo akiwa anaelekea moja kwa moja langoni.
Beki huyo raia wa Sweden alionyeshwa kadi ya njano, na refa Rade Obrenovic alishauriwa kutazama tukio hilo kwenye VAR ili kuamua kama afute uamuzi wake na kutoa kadi nyekundu. Hata hivyo, alibaki na uamuzi wa awali licha ya kuonekana wazi Ahmedhodzic alinyima fursa ya wazi ya kufunga.
Villa pia iliepuka kipigo mapema baada ya kichwa cha Ayase Ueda kipindi cha kwanza kuonekana wazi kuvuka mstari wa goli, lakini jitihada za kipa Marco Bizot zilisaidia na goli hilo halikukubaliwa kwa sababu ya faulo dhidi ya Matty Cash ndani ya boksi.
STURM 2-1 RANGERS
Mwanzo mbaya wa Rangers msimu huu umeendelea baada ya kupoteza kwa mara ya pili mfululizo kwenye michuano ya Europa League, safari hii ikichapwa na mabingwa wa Austria, Sturm Graz.
Ushindi wa dakika za majeruhi dhidi ya Livingston siku ya Jumapili uliwapa kikosi cha Russell Martin ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya Scotland baada ya jaribio la mara saba, lakini matumaini ya kuendeleza mwendo huo yalizimwa mapema na bao la awali la Tomi Horvat.
Kwa mara nyingine tena, Rangers ilijiharibia yenyewe. James Tavernier alirusha mpira dhaifu katika eneo lao la hatari, ukarudishwa nyuma na kupigwa kwa urahisi kumshinda kipa Jack Butland ambaye hakuonekana imara.
Mpira wa adhabu uliopigwa kwa ustadi ulipasua safu ya ulinzi ya Rangers na kumruhusu nyota wa kimataifa kutoka Georgia, Otar Kiteishvili, kufunga kabla ya mapumziko.
Rangers iliyopoteza nyumbani dhidi ya Genk katika mechi ya kwanza, ilionekana kuimarika kipindi cha pili na Gassama, ambaye mara nyingi ndiye shujaa wa kikosi hicho, akapiga shuti kali na kufungua matumaini.
Wakiwa wamerudishwa mchezoni, vijana wa Ibrox walihangaika kusaka pointi yao ya kwanza barani Ulaya msimu huu, huku Youssef Chermiti, Nico Raskin na John Souttar wakikaribia kufunga dhidi ya Graz waliokuwa wamepoteza wiki iliyopita ugenini kwa Midtjylland.
Hata hivyo, jitihada hizo zilichelewa kwa kikosi cha Martin, ambacho sasa kimekusanya ushindi wa mechi tano pekee kati ya 16 ilizocheza kwenye mashindano yote.
CELTIC 0-2 BRAGA
Celtic imeendelea kusikitisha kwenye michuano ya Ulaya baada ya kuruhusu bao kila kipindi huku yenyewe ikinyimwa bao la kusawazisha kwa uamuzi tata, hali iliyowawezesha Sporting Braga kushinda mchezo wa Europa League uliokuwa na vurugu nyingi huko Parkhead.
Kipa Kasper Schmeichel alicheza kwa makosa mengi, akishindwa kuokoa shuti la mbali la mapema kutoka kwa Ricardo Horta lililowanyamazisha mashabiki wa Celtic Park.
Mda mfupi kabla ya mchezo kumalizika, Schmeichel aliokoa shuti moja kali, lakini akawa hana la kufanya baada ya jaribio lake la kuondoa mpira kugonga mwili wa Gabri Martinez na kujaa wavuni, na kufanikisha Braga kupata alama zote tatu.
Baada ya kufeli kufuzu Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kairat Almaty, na kutoka sare katika mchezo wa kwanza wa Europa League dhidi ya Red Star Belgrade, matokeo haya yameendeleza mwanzo mbaya wa Celtic katika kampeni yao ya Ulaya.
Kiwango cha timu hiyo kimeshuka sana ikilinganishwa na msimu uliopita, jambo linalompa hofu kocha Brendan Rodgers kwamba huenda mabingwa hao wa Scotland wakashindwa kufuzu hatua za mtoano endapo hawatashtuka mapema.
Braga ilitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, hali iliyomlazimu Rodgers kubadilisha mfumo wake kipindi cha pili kwa kutumia mabeki watatu na kuimarisha kiungo.
Celtic ilionekana kuimarika baada ya mabadiliko hayo na ilidhani imesawazisha kupitia Kelechi Iheanacho aliyefunga kwa utulivu baada ya kosa la safu ya ulinzi ya Braga.
Hata hivyo, furaha hiyo ilikatishwa na refa Tobias Stieler aliyepuliza filimbi akidai kulikuwa na tukio la kushika mpira. VAR ilikagua kwa muda mrefu na kuunga mkono uamuzi huo, ingawa picha zilionekana kuonyesha kuwa mpira haukuugusa mkono bali ulimgonga mfungaji kichani.
Kipa wa Braga, Lukas Hornicek aliokoa nafasi mbili muhimu wakati Celtic ilipoongeza mashambulizi kusaka bao. Kwanza, aliruka upande wa kushoto kuokoa kichwa cha Kieran Tierney, kisha akajitupa upande wa pili kuokoa shuti la mzunguko kutoka kwa Sebastian Tounekti lililoonekana kuelekea wavuni.
Rodgers alifanya mabadiliko zaidi akiwatoa Reo Hatate, Arne Engels na James Forrest, lakini hakuna aliyefanikiwa kutoa ubora ulioweza kuokoa pointi kwa Celtic.
MATOKEO EUROPA LEAGUE
Bologna 1-1 Freiburg
Brann 1-0 Utrecht
Celtic 0-2 Braga
FCSB 0-2 Young Boys
Fenerbahçe 2-1 Nice
Ludogorets 0-2 Real Betis
Panathinaikos 1-2 Go Ahead
Roma 0-1 Lille
Viktoria Plzeň 3-0 Malmö
Basel 2-0 Stuttgart
Celta Vigo 3-1 PAOK
Feyenoord 0-2 Aston Villa
Genk 0-1 Ferencváros
Maccabi Tel Aviv 1-3 Dinamo Zagreb
Nottingham Forest 2-3 Midtjylland
Lyon 2-0 RB Salzburg
Porto 2-1 Red Star Belgrade
Sturm Graz 2-1 Rangers
MATOKEO CONFERENCE LEAGUE
Dynamo Kyiv 0-2 Crystal Palace
Jagiellonia Białystok 1-0 Hamrun Spartans
KuPS 1-1 Drita
Lausanne-Sport 3-0 Breidablik
Lech Poznań 4-1 Rapid Vienna
Noah 1-0 Rijeka
Omonia Nicosia 0-1 Mainz
Rayo Vallecano 2-0 Shkendija
Zrinjski 5-0 Lincoln Red Imps
AEK Larnaca 4-0 AZ Alkmaar
Aberdeen 2-3 Shakhtar Donetsk
Celje 3-1 AEK Athens
Fiorentina 2-0 Sigma Olomouc
Legia Warszawa 0-1 Samsunspor
Raków Częstochowa 2-0 Universitatea Craiova
Shelbourne 0-0 Häcken
Slovan Bratislava 1-2 Strasbourg
Sparta Prague 4-1 Shamrock