Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yaweka Sh350 Bilioni kwa Barcola

Muktasari:

  • Hata hivyo, mabingwa wa Ufaransa hawapo tayari kumwachia kirahisi nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, wakidai ada inayokaribia Pauni 145 milioni, jambo linalomaanisha mazungumzo kati ya klabu hizo bado yanaendelea.

LONDON, England: LIVERPOOL imeweka nguvu katika mbio za kumsajili winga wa Paris Saint-Germain (PSG), Bradley Barcola, huku ikiwa tayari kutoa ada inayokaribia Pauni 100 milioni (zaidi ya Sh350 bilioni) ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kabla ya msimu mpya.

Hata hivyo, mabingwa wa Ufaransa hawapo tayari kumwachia kirahisi nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, wakidai ada inayokaribia Pauni 145 milioni, jambo linalomaanisha mazungumzo kati ya klabu hizo bado yanaendelea.

Iwapo usajili huo utakamilika, utakuwa ni mara ya tatu kwa Liverpool kutumia zaidi ya Pauni100 milioni kwa mchezaji ndani ya kipindi kifupi, baada ya kumsajili Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen na mshambuliaji Alexander Isak, aliyekuwa usajili wa rekodi wa klabu hiyo.


BARCOLA LULU INAYONG'AA ULAYA

Barcola amejijengea sifa kutokana na kasi yake, uwezo wa kupiga chenga na kuwatoka mabeki mmoja kwa mmoja, jambo lililomfanya kuwa mmoja wa mawinga wanaotafutwa zaidi barani Ulaya.

Tangu ajiunge na PSG akitokea Lyon mwaka 2023 kwa ada ya takribani Pauni 38.5milioni, amesaidia klabu hiyo kutwaa mataji matatu ya Ligue 1, mawili ya Kombe la Ufaransa, pamoja na UEFA Super Cup na Kombe la Mabara la FIFA.

Pia, aliingia akitokea benchi katika fainali mbili zilizopita za Ligi ya Mabingwa Ulaya, PSG ilipoifunga Inter Milan mabao 5-0 na baadaye kuitetea tena taji hilo dhidi ya Arsenal.


SALAH AMEONDOKA

Kuondoka kwa Mohamed Salah, aliyehitimisha safari yake ya miaka tisa Anfield baada ya kufunga mabao 257, kumeiacha Liverpool ikihitaji nguvu mpya katika safu ya ushambuliaji.

Hali hiyo imezidishwa na majeraha ya Hugo Ekitike, ambaye alipasuka wa kisigino mwezi Aprili na hatarajiwi kurejea uwanjani ndani ya mwaka huu.

Wakati huohuo, Cody Gakpo ameendelea kuhusishwa na tetesi za kuhamia Tottenham, ingawa Liverpool imeweka wazi kuwa haina mpango wa kumuuza.


ANATAKA NAFASI ZAIDI YA KUCHEZA


Barcola ni mchezaji anayependelea kucheza winga wa kushoto, pia ana uwezo wa kucheza kulia au katikati ya ushambuliaji.

Akiwa PSG amekuwa akipambana kupata nafasi ya kudumu kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa Khvicha Kvaratskhelia na Desire Doue, jambo ambalo linaaminika kumshawishi kufikiria kuhamia Anfield ambako angeweza kupata dakika nyingi zaidi za kucheza.


AMENG'ARA PIA TIMU YA TAIFA

Nyota huyo tayari ameichezea Ufaransa mechi 28, huku akifunga mabao matatu katika Kombe la Dunia 2026, likiwemo bao alilofunga kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya England uliomalizika kwa kipigo cha mabao 6-4.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa PSG, nafasi yake kikosini ilikuwa ikigombewa na chipukizi mwenzake Desire Doue, ambapo kocha Didier Deschamps aliwatumia kwa kupokezana, huku wote wakianza mechi nne kati ya nane za Ufaransa kwenye mashindano hayo, lakini hawakuanza pamoja hata mchezo mmoja.

Sasa macho yote yanaelekezwa Anfield kuona kama Liverpool itaongeza ofa yake na kuishawishi PSG kumruhusu Barcola kuanza ukurasa mpya wa maisha yake nchini England.