Vigogo Ulaya katika mtihani mzito

Muktasari:
- Mbali ya timu nane za juu ambazo tayari zimeshafuzu kucheza 16 bora, kuanzia timu ya tisa hadi 24, zitacheza mechi mbili nyumbani na ugenini ili kutafuta nane nyingine zitakazokwenda 16 bora.
MADRID, HISPANIA: BAADA ya jana kumalizika kwa hatua ya ligi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, vigogo mbalimbali barani humo wamejikuta katika mtihani wa kucheza mechi za mtoano kuwania kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo baada ya kumaliza katika nafasi za chini.
Mbali ya timu nane za juu ambazo tayari zimeshafuzu kucheza 16 bora, kuanzia timu ya tisa hadi 24, zitacheza mechi mbili nyumbani na ugenini ili kutafuta nane nyingine zitakazokwenda 16 bora.
Droo ya mechi hizo inatarajiwa kufanyika kesho huko Nyon, Uswisi kuanzia saa 8:00 mchana.
Bingwa mtetezi Real Madrid ambayo imemaliza katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo, kwenye hatua ya mtoano inaweza kukutana na aidha Celtic au Manchester City na ikishinda kwenda 16 bora itakuwa na uwezekano wa kuumana na Atletico Madrid na Bayer Leverkusen sawa na Bayern Munich ambayo pia inaweza kukutana na Man City au Celtic.
Vilevile PSG inaweza kupangwa na Monaco au Brest na ikipita inaweza kukutana na kati ya Liverpool au Barcelona kwenye 16 bora.
Kwa upande mwingne AC Milan na PSV Eindhoven zinaweza kuumana na Feyenoord na Juventus na mmoja wao akipita anaweza kuumana na Arsenal au Inter Milan.
Baada ya droo ya kesho, mechi za mkondo wa kwanza zinatarajiwa kupigwa kuanzia Februari 11 hadi 12 kisha za mkondo wa pili zitaanza Februari 18 hadi 19.
Baada ya hapo itafanyika droo ya robo fainali, Februari 21, baada ya kumaliza kwa mechi hizo za mtoano na kupatikana kwa timu nyingine nane zitakazoungana na nane zilizofuzu moja kwa moja.
HATUA YA MTOANO:
KILA TIMU ITAKUTANA NA MOJA YA TIMU HIZI:
Atlanta: Sporting Lisbon au Club Brugge
Borussia Dortmund: Sporting Lisbon au Club Brugge
Real Madrid: Celtic au Man City
Bayern Munich: Celtic au Man City
AC Milan: Feyenoord au Juventus
PSV: Feyenoord au Juventus
PSG: Monaco au Brest
Benfica: Monaco au Brest
Feyenoord: AC Milan au PSV
Juventus: AC Milan au PSV
Celtic: Bayern Munich au Real Madrid
Manchester City: Bayern Munich au Real Madrid
Sporting Lisbon: Atalanta au Borussia Dortmund
Club Brugge: Atalanta au Borussia Dortmund
HATUA YA 16-Bora:
Liverpool: PSG, Benfica, Monaco au Brest
Barcelona: PSG, Benfica, Monaco au Brest
Arsenal: AC Milan, PSV Eindhoven, Feyenoord au Juventus
Inter Milan: AC Milan, PSV Eindhoven, Feyenoord au Juventus
Atletico Madrid: Real Madrid, Bayern Munich, Celtic au Man City
Bayer Leverkusen: Real Madrid, Bayern Munich, Celtic au Man City
Lille: Atalanta, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon au Club Brugge
Aston Villa: Atalanta, Borussia Dortmund, Sporting Lisbon au Club Brugge