Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Manchester United wamfungia kazi Sesko

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Staa huyo ambaye pia anawindwa na Newcastle United inayomtazama kama mbadala sahihi wa Isak, anawindwa kwa nguvu na Mashetani Wekundu kwa sasa.

MANCHESTER United imeingia katika mchakato wa kuiwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig na timu ya taifa ya  Slovenia, Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 22.

Staa huyo ambaye pia anawindwa na Newcastle United inayomtazama kama mbadala sahihi wa Isak, anawindwa kwa nguvu na Mashetani Wekundu kwa sasa.

Sesko ni mmoja kati ya machaguo ya kwanza ya kocha Ruben Amorim ambaye amewaambia mabosi wa Manchester United kwamba bado anahitaji kupata mshambuliaji mwingine ili kuimarisha zaidi eneo la ushambuliaji.

Hivi karibuni Mashetani Wekundu walifanikisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo.

Mwanzoni mwa dirisha hili, Sesko alikuwa akihusishwa pia na vigogo wengine wakiwamo Chelsea, Arsenal na Liverpool, lakini sasa zinaonyesha kutokuwa na mpango naye na zimegeukia wachezaji wengine.

Man United italazimika kutoa zaidi ya Pauni 70 milioni kama ada yake ya uhamisho ingawa inaweza kuzidi hapo ikiwa itatokea timu nyingine kutaka kumsajili.

Sesko mwenyewe anaripotiwa kutamani kutua England, lakini hana haraka wala hatalazimisha kutaka kuondoka ikiwa Mashetani Wekundu hawatafikia mwafaka na RB Leipzig.

Hata hivyo, kwa upande wa makubaliano binafsi na mchezaji mwenyewe na Man United pia bado hakuna mwafaka wowote uliofikiwa ingawa inaaminika haiwezi kuwa changamoto sana kwani mchezaji mwenyewe anataka kujiunga na chama hilo.


Marc Cucurella

CHELSEA imesisitiza haifikirii kumuuza beki  wa kushoto wa kimataifa wa Hispania, Marc Cucurella, 27, anayewindwa na timu kibao za Saudi Arabia ambazo nyingi zilivutiwa na kiwango bora alichoonyesha katika michuano ya Euro akiwa na Hispania. Uamuzi wa Chelsea kutomuuza staa huyo unatokana na kocha Enzi Maresca kusisitiza kuwa beki huyo yupo kwenye mipango yake kwa msimu ujao.


Morgan Rogers

KIUNGO wa Aston Villa na England, Morgan Rogers, 23, ni miongoni mwa wachezaji ambao kocha wa Chelsea amependekeza wasajiliwe katika kikosi chake dirisha hili. Kwa sada Chelsea inafanya mazungumzo na Villa kuhusu inshu za ada ya uhamisho, lakini matajiri hao wa Jiji la London wanadaiwa kutaka kuwatumia mastaa kadhaa kama sehemu ya ofa akiwemo beki raia wa England, Tosin Adarabioyo, 27, na straika wa Senegal, Nicolas Jackson, 24.


Nathan Zeze

LIVERPOOL, Everton, Aston Villa na Bournemouth huenda zikaangukia pua kumsajili beki kisiki wa Nantes, Mfaransa Nathan Zeze  katika dirisha hili la majira ya kiangazi baada ya staa huyo kupokea ofa nono kutoka Saudi Arabia. Kwa mujibu wa taarifa, Zeze mwenye umri wa miaka 20 amepokea  ofa kutoka Neom inayoshiriki Ligi Kuu Saudi Arabia na tayari ameshafanya uamuzi wa kujiunga nayo.


Xavi Simons

‎BBAYERN Munich imebaki pekee ambayo inaonyesha nia ya kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Xavi Simons, 22, katika dirisha hili. Simons ambaye alisaini mkataba wa kudumu kuendelea kusalia Leipzig mwaka jana, Bayern inadaiwa kuweka mezani zaidi ya Pauni 40 milioni kwa ajili ya uhamisho wa staa huyo wa kimataifa wa Uholanzi.



Endrick

REAL Madrid inasikiliza ofa kutoka timu mbalimbali zinazotaka huduma ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil,  Endrick katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Mabosi wa Real Madrid wanata kumtoa kwa mkopo ili kumpa nafasi ya kukua zaidi kisoka kwa kucheza mechi nyingi tofauti na ilivyo sasa ambapo hapewi nafasi kubwa. Hata hivyo, taarifa inaeleza Endrick hataki kuondoka akiamini anaweza kupambania namba.


Douglas Luiz

EEVERTON, West Ham United na  Nottingham Forest zipo katika vita ya kuwania saini ya kiungo wa Juventus, Douglas Luiz, 27, ambaye anataka kurudi England katika dirisha hili. Luiz anataka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza Juventus. Taarifa zinadai awali Man Utd ilitaka kumsajili ikashindwa.