Vigogo Manchester City bado wanaitaka saini ya Rodrygo
Muktasari:
- Ripoti zinadai Madrid inahitaji kiasi kisichopungua Euro 80 milioni ili kimuuza fundi huyu ambaye hapati nafasi ya kutosha kwa sasa.
MANCHESTER City bado haijafunga milango ya kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, dirisha hili la majira ya kiangazi.
Ripoti zinadai Madrid inahitaji kiasi kisichopungua Euro 80 milioni ili kimuuza fundi huyu ambaye hapati nafasi ya kutosha kwa sasa.
Rodrygo ambaye pia alikuwa akiwindwa na Bayern Munich kabla ya timu hiyo kumgeukia Luis Diaz, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.
Hadi sasa kwa timu za England, Liverpool ndio imebakia katika vita hii dhidi ya Man City kwani inamtaka Rodrygo ili akawe mbadala wa Luis Diaz.
Madrid iliweka wazi haina mpango wa kumuuza staa huyo lakini ikitokea ofa nzuri na yeye mwenyewe akiwa tayari haitomzuia kuondoka.
Rodrygo anataka kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kucheza ili kurudi tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil na hivi karibu hajajumuishwa.
Kukosekana katika kikosi kunaweka nafasi ya kucheza michuano ijayo ya Kombe la Dunia mwakani kuwa matatani.
Adam Wharton
REAL Madrid inamfuatilia kwa karibu kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton,21, ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Palace kutokana na kiwango chake anachoendelea kukionyesha kwenye Ligi Kuu England. Palave haina mpango wa kumuuza kwa sasa ingawa inaweza kubadili mawazo yao ikiwa Madrid itaweka mezani ofa nono. Mkataba wake na Palace unatarajiwa kumalizika mwaka 2030 na kuna uwezekano akaondoka dirisha hili kabla halijafungwa.
Nicolas Jackson
ASTON Villa huena ikaachaa na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, 24, katika dirisha hili baada ya kuambiwa kuwa inatakiwa Pauni 70 milioni ili kuvunja mkataba wake. Jackson ni miongoni mwa wachezaji ambao Chelsea imewaweka sokoni dirisha hili na awali ilionekana kama angeuzwa nje ya England lakini yeye mwenyewe alikataa na kusisitiza bado anataka kucheza Ligi Kuu England.
Andre Onana
KIPA wa kimataifa wa Cameroon, Andre Onana, 29, anatarajiwa kuendelea kusalia Manchester United, licha ya uvumi wa kuhusishwa kuondoka dirisha hili. Inaelezwa hata Man Uniter itakapofanikisha usajili wa kipa mwingine, bado Onana atasalia kama kipa namba mbili. Mashetani hao wekundu wanatajwa kuwa katika mpango wa kumsajili kipa wa Royal Antwerp Senne Lammens, 23, ambaye inahitajika Pauni 17 milioni ili kumpata.
Savinho
TOTTENHAM iko tayari kutoa zaidi ya Pauni 60 milioni ili kumsajili winga chipukizi wa Brazil Savinho, 21, kutoka Manchester City, ambaye msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Girona na aling’ara kwenye La Liga. Timu nyingi zimevutiwa sana na kiwango cha staa huyu alichoonyesha msimu uliopita lakini changamoto kubwa imekuwa ni pesa zinazohitaji na Man City ili kumuuza ambapo inakadiriwa kufikia Pauni 70 milioni.
Etta Eyong
EVERTON imewasiliana na Villarreal kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Etta Eyong, 21, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao. Villarreal inapambana kutaka kumsainisha mkataba mpya na ikiwa itashindikana ndiyo itaamua kumuuza. Hata hivyo, inaonekana kuna asilimia nyingi za kumuuza kwa sababu hajakubali kusaini mkataba mpya hadi sasa.
Soungoutou Magassa
WEST Ham United imewasilisha ofa ya kumsajili kiungo wa AS Monaco, Soungoutou Magassa, 21, dirisha hili. Hata hivyo, Monaco imekataa ofa hiyo ya awali ya takribani Pauni 16 milioni. West Ham inapanga kurejea tena na ofa mpya inayoweza kufikia Pauni 20 milioni kiasi ambacho inaamini hakitokataliwa.
Tyler Dibling
CRYSTAL Palace inataka kuwasilisha ofa ya Pauni 35 milioni kwenda Southampton ili kuipata saini ya winga wa klabu hiyo, Tyler Dibling. Awali Everton ilidaiwa kuweka mezani Pauni 30 milioni, hivyo itatakiwa kutoa zaida ya kile kilichotolewa na Palace au kukubali kushindwa. Palace imeingia vitani kumsajili fundi huyu ili kuziba mapengo yaliyoachwa na walioondoka.