Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oura aibeba Simba Malawi

OURA Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo uliopigwa leo Septemba 6, 2026 kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi, Simba haikucheza vizuri dakika 45 za kwanza ikimaliza bila hata kupiga shuti lililolenga lango huku yale yasiyolenga yakiwa sita.

SIMBA imeanza vyema hesabu za Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupata ushindi safi ugenini, ikiichapa Mighty Wanderers kwao Malawi bao 1-0 likifungwa na Anicet Oura.

Mchezo huo uliopigwa leo Septemba 6, 2026 kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi, Simba haikucheza vizuri dakika 45 za kwanza ikimaliza bila hata kupiga shuti lililolenga lango huku yale yasiyolenga yakiwa sita.

Wanderers ilicheza vizuri kipindi cha kwanza ikifanya mashambulizi ya kushtukiza na kuwapa wakati mgumu wageni.

OU 01

Nafasi bora ambazo Simba ilizetengeza kipindi cha kwanza ni dakika ya sita kwa kona ya Neo Maema kugonga mwamba wa juu na kurudi uwanjani.

Simba tena dakika ya 29, winga wake Kaletso Makgalwa akitengeneza nafasi nzuri lakini shuti lake likatoka nje kidogo.

Nafasi nyingine ya Simba ilipatikana dakika ya 32, Elie Mpanzu akipokea pasi safi kutoka kwa Ibraheem Jabaar, lakini shuti lake likapaa juu.

Wanderers ikatengeneza shambulizi zuri dakika ya 45, beki wake wa kulia Stanley Sanudi krosi yake ikadhibitiwa vizuri na beki Ismael Toure wakati akimtafuta mshambuliaji Muhammad Sulumba.

Winga Anicet Oura ambaye hakuonekana muda mwingi, dakika ya 65 akafanikiwa kuipa Simba bao pekee likitokana na juhudi binafsi akitumia makosa ya mabeki wa wenyeji na kuwazidi akili akienda kufunga.

Kabla ya kuingia kwa bao hilo, kipa wa Simba, Mahamadou Kassali aliupiga mpira mrefu kama anaokoa, ndipo ukamkuta Oura aliyeukwamisha nyavuni.

OU 02

Mbali na hilo, Kassali alifanya kazi bora ya kuokoa mashuti mawili, moja kwa Kila kipindi ambapo kipindi cha kwanza shuti la Peter Ngambi alilipangua vizuri.

Kassali tena dakika ya 88 akafanya kazi nzuri ya kupangua shambulizi hatari, shuti la kiungo Blessing Sengini lilifika mikononi mwake na kuliweka lango salama.


DOUMBIA BADO

Simba ilifanya mabadiliko mawili dakika ya 62 ikiwaingiza mshambuliaji Ibrahim Doumbia akichukua nafasi ya Mpanzu huku kiungo Clatous Chama akichukua nafasi ya Jabaar.

Doumbia ambaye bado anatafuta bao lake la kwanza tangu atue Simba msimu huu, alipokea nafasi nzuri kufunga kwa kichwa, kufuatia krosi ya Oura, akiwa aneo zuri, lakini akashindwa kulenga lango la wapinzani.

Doumbia nafasi nyingine aliipata dakika ya 86, shuti lake hafifu liliguswa na beki na kutoka nje, ikawa kona.

Matokeo hayo yanaipa Simba mwanzo mzuri ikisubiri marudiano Septemba 13, 2026 ikiwa mwenyeji kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo matokeo yoyote ya sare au ushindi, ni faida kwa vijana hao wa Kocha Steve Barker.