Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Liverpool kufanya kufuru kwa Alexander Isak

TETESI Pict

Muktasari:

  • Isak ambaye ana mkataba na Newcastle hadi mwaka 2028 hivi karibuni inadaiwa aliwasilisha barua kwa mabosi wa timu hiyo akiwaleza anahitaji kuondoka na kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

LIVERPOOL ipo tayari kutoa dau litakalovunja rekodi ya usajili ya England dirisha hili kwa ajili ya kumsajli mshambuliaji wa Newcastle na timu ya taifa ya  Sweden Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 25.

Isak ambaye ana mkataba na Newcastle hadi mwaka 2028 hivi karibuni inadaiwa aliwasilisha barua kwa mabosi wa timu hiyo akiwaleza anahitaji kuondoka na kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

Mbali ya Liverpool ambayo ndio inaonekana kupewa nafasi kubwa zaidi ya kumsajili staa huyu, ripoti zinaeleza pia Al-Hilal ya Saudi Arabia pia inahitaji kumsajili.

Matajiri hawa wa Saudi Arabia wapo tayari kutoa karibia Pauni 130 milioni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Hata hivyo, Isak haonekani kuwa tayari kuondoka Ulaya kwa sasa licha ya mshahara mkubwa ambao Waarabu hao wamepanga kumpa.

Isak ambaye sio sehemu ya kikosi cha Newcastle kilichosafiri kwenda Singapore kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, awali alikuwa akimezewa mate na Chelsea na Manchester United lakini zimeamua kutomfuatilia kutokana na ada yake ya uhamisho kuwa kubwa.

Man United ambayo imeshawasajili Matheus Cunha, 26, na mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25 katika dirisha hili, bado inatafuta mshambuliaji mmoja.


Ollie Watkins

MABOSI wa Aston Villa wamewaambia Manchester United mshambuliaji wao Ollie Watkins hauzwi, licha ya klabu hiyo ya Old Trafford kuwa na nia ya kutaka kumsajili dirisha hili. Ripoti zinadai kocha wa Man United, Ruben Amorim bado anahitaji mshambuliai mmoja katika kikosi chake ili kuzidi kuboresha zaidi eneo hilo licha yakuwa tayari ameshasajiliwa wawili hadi sasa. Villa haitaki kumuuza Watkins kwa sababu ndio mshambuliaji wao pekee na tegemeo katika kikosi cha kwanza.


Luis Diaz

BAYERN Munich inajiandaa kuwasilisha ofa mpya Liverpool kwa ajili ya kumsajili winga wa klabu hiyo, Luis Diaz dirisha hili. Diaz ameshawaambia mabosi wa Liverpool anataka kuondoka dirisha hili ili kutafuta changamoto sehemu nyingine. Diaz mwenye umri wa mwaka 28, mkataba wake na Liverpool unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na awali alikuwa akitajwa kuwa katika rada za Barcelona ambayo imeshindwa kutokana na bei yake.


Harvey Elliott

MSHAMBULIAJI wa Liverpool,  Harvey Elliott yuko tayari kuondoka Anfield, dirisha hili na kutua moja ya timu zinazohitaji huduma yake. Tovuti ya Metro imeripoti  West Ham ni miongoni mwa klabu ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili staa huyu wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 22.


Raheem Sterling

VIGOGO wa Napoli wamehamishia nguvu zao kwa winga wa Chelsea, Raheem Sterling, 30, ili kumsajili dirisha hili. Napoli ambao ni mabingwa wetetezi wa Ligi Kuu Italia, wamedhamiria kufanya vizuri kuelekea msimu ujao na hadi sasa imeshakamilisha usajili wa Kevin de Bruyne. Napoli pia inamtaka kiungo wa Manchester City, Jack Grealish.


Douglas Luiz

Douglas Luiz wa Juventus inadaiwa hakuripoti siku ya kwanza ya mazoezi ya kabla ya msimu sababu kubwa ikitajwa anashughulikia uhamisho kwani anahitajika na  West Ham, Everton na Liverpool dirisha hili. Luiz ambaye ni miongoni mwa mastaa ambao Juventus ilitaka kuwatumia kama sehemu ya mabadilishao ili kumpata Jadon Sancho kutoka Manchester United, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Lucas Perri

LEEDS United iliyopanda daraja hivi karibuni imefikia makubaliano ya kumsajili kipa wa Olympique Lyon, Lucas Perri kwa Pauni 15.6 milioni dirisha hili. Kipa huyu raia wa Brazil, 27, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Ujerumani ambako Leeds imeweka kambi. Awali Lyon ilihitaji zaidi ya Pauni 20 milioni lakini ililazimika kumuuza baada ya mchezaji mwenyewe kuweka wazi kuwa haitaji kucheza katika timu yao kwa msimu ujao.


Benjamin Sesko

NEWCASTLE imeelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Slovenia Benjamin Sesko, 22, anayeichezea RB Leipzig, ambayo inahitaji kumsajili dirisha hili ili awe mbadala wa Alexander Isak ambaye ameweka wazi anahitaji kuondoka. Sesko ambaye awali alitajwa kuwa katika rada za Arsenal na baadhi ya vigogo wengine England, ana tamani sana kucheza EPL kwa msimu ujao na yupo tayari kukubali ofa ya Newcastle.