Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video ya mazoezi ya Pochettino yavuja

MAZOEZi Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo limekuwa aibu kubwa kwa Manchester United, hasa ikizingatiwa kuwa klabu hiyo imelipa pauni milioni 10 ili kumng'oa kocha huyo raia wa Argentina pamoja na wasaidizi wake kutoka mikataba yao na Shirikisho la Soka la Marekani (US Soccer Federation).

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imejikuta katika wakati mgumu baada ya video ya mazoezi ya kwanza ya kocha mpya Mauricio Pochettino kuvuja mtandaoni, kufuatia tukio la ndege isiyo na rubani (drone) kurekodi shughuli za kikosi hicho katika uwanja wao wa mazoezi wa Carrington.

Video hiyo yenye urefu wa dakika 12, iliyorekodiwa Alhamisi, inawaonyesha Pochettino pamoja na benchi lake la ufundi wakifanya kazi na wachezaji wa United katika siku yake ya kwanza kamili ya kuongoza mazoezi ya timu hiyo.

Tukio hilo limekuwa aibu kubwa kwa Manchester United, hasa ikizingatiwa kuwa klabu hiyo imelipa pauni milioni 10 ili kumng'oa kocha huyo raia wa Argentina pamoja na wasaidizi wake kutoka mikataba yao na Shirikisho la Soka la Marekani (US Soccer Federation).

Pochettino anatarajiwa kuanza rasmi kazi yake ya ushindani Jumapili kwa mchezo dhidi ya Liverpool utakaopigwa Uwanja wa Anfield. Hata hivyo, bado haijafahamika iwapo Liverpool inaweza kupata faida yoyote kutokana na video hiyo iliyovuja.

MAZO 01

United imekuwa ikitumia ndege zake zisizo na rubani kurekodi mazoezi kwa ajili ya uchambuzi wa kiufundi. Hata hivyo, miaka sita iliyopita klabu hiyo iliweka mabango yanayopiga marufuku matumizi ya vifaa hivyo karibu na eneo la mazoezi ili kulinda siri za mbinu zake dhidi ya wapinzani.

Video hiyo iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube na akaunti inayojulikana kwa jina la CC Overview, ambayo ilidai kuwa anga la juu ya Carrington halina zuio na kwamba drone iliyotumika ilikuwa ikifanya kazi kwa mujibu wa kanuni za Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uingereza.

Kwa mujibu wa akaunti hiyo, video ilirekodiwa dakika 30 baada ya mazoezi kuanza na inamwonyesha Pochettino akitoa maelekezo kwa wachezaji akiwa pamoja na kikosi chake cha makocha.

MAZO 02

Wasaidizi wake ni pamoja na kocha msaidizi Jesus Perez, kocha wa kikosi cha kwanza Miguel D’Agostino, kocha wa makipa Toni Jimenez, mwanawe Sebastiano Pochettino anayehusika na mazoezi ya viungo pamoja na kocha wa maandalizi ya kimwili Silvia Tuya.

Pochettino aliwasili Manchester Jumatano akiwa na D’Agostino, Tuya na mchambuzi Alec Scott baada ya kumaliza mchezo wake wa mwisho akiwa kocha wa Marekani dhidi ya Haiti mjini Cincinnati.

Baada ya mchezo huo, United iliwatuma ndege binafsi kuwarudisha England, huku Pochettino akielekea moja kwa moja Carrington baada ya kutua nchini humo muda mfupi kabla ya saa sita mchana.

Kwa upande mwingine, Perez, Jimenez na Sebastiano walikuwa wameanza kufika katika kituo hicho tangu mwishoni mwa wiki baada ya kuruhusiwa na Shirikisho la Soka la Marekani kuondoka kufuatia mchezo wa kwanza dhidi ya Haiti uliochezwa Miami.

Pochettino ataka kubadili utamaduni United

Akizungumza kwa mara ya kwanza na chombo cha habari cha ndani cha Manchester United Alhamisi, Pochettino alieleza mpango wake wa kuijenga upya timu hiyo na kuirejesha katika ushindani wa nafasi za juu kwenye Ligi Kuu England.

MAZO 03

Kocha huyo alisisitiza kuwa jambo la kwanza analotaka kulifanyia kazi ni utamaduni wa klabu, nidhamu na kujenga mazoea mazuri kwa wachezaji.

"Utamaduni ndio jambo muhimu zaidi. Tunahitaji kujenga mazoea, misingi na kanuni ambazo zitatusaidia kufikia malengo yetu," amesema Pochettino.

Ameongeza kuwa anataka kuunda mazingira yatakayowapa wachezaji uhuru wa kutumia vipaji vyao bila kubeba presha kubwa.

"Wachezaji wanahitaji kuonyesha vipaji vyao. Tunapaswa kutengeneza mazingira na mfumo utakaowawezesha kufanya vizuri. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi na kipaumbele chetu kwa sasa ni kufanya kazi nao na kujaribu kupunguza presha," amesema.

Pochettino pia alieleza kuwa hataki kuangalia zaidi nafasi ya sasa ya Manchester United kwenye msimamo wa ligi, bali anataka kuzingatia uwezo mkubwa uliopo ndani ya klabu hiyo.

"Ni makosa kuangalia hali ya sasa pekee. Tunahitaji kuangalia uwezo wa klabu hii. Tunapaswa kuwajibika kwa mazingira tuliyopo, lakini wakati huohuo tuelewe kuwa huu ni mchezo wa soka na tunahitaji kucheza tukiwa huru," alisisitiza.

Amesema presha inapaswa kuwapa wachezaji nguvu na si kuwafanya washindwe kuonyesha uwezo wao.

Pochettino anaamini kwa ushirikiano wa benchi lake la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Manchester United, klabu hiyo inaweza kurejea katika nafasi inayostahili.

"Tunahitaji kujenga falsafa yetu wenyewe, kuanzia mwanzo. Kwa nguvu ya klabu hii na sapoti ya mashabiki, naamini tutafika pale tunapostahili kuwa," amesema.