Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba zinavyoguna Man Utd kubaki EPL

POCHETINO Pict

Muktasari:

  • Kwa kuzingatia Manchester United ilikuwa nyuma kwa mabao 4-2 wakati saa ikiingia dakika ya pili ya nyongeza dhidi ya Aston Villa, huenda ungetarajia hali ya timu hiyo baada ya mchezo kumalizika, kufuatia sare ya mabao 4-4 kupunguza huzuni kidogo kwa mashabiki wake.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imempata kocha mpya, Mauricio Pochettino, lakini inakumbukwa iliokolewa kwa namna fulani na kupata pointi moja kutoka kwenye taya za kupoteza dhidi ya Aston Villa katika mechi ya mwisho kabla ya kalenda ya mechi Fifa kuanza, lakini hilo halikufanya chochote kuondoa ukweli ipo katika eneo la kushuka daraja Ligi Kuu England.

Kwa kuzingatia Manchester United ilikuwa nyuma kwa mabao 4-2 wakati saa ikiingia dakika ya pili ya nyongeza dhidi ya Aston Villa, huenda ungetarajia hali ya timu hiyo baada ya mchezo kumalizika, kufuatia sare ya mabao 4-4 kupunguza huzuni kidogo kwa mashabiki wake.

Hali ya mashabiki ilikuwa ya hasira kidogo kuliko ilivyokuwa mwishoni mwa mchezo wa nyumbani ilipofungwa 3-0 na Bournemouth.

POCHE 02

Safari hii, timu kwa ujumla ilipigiwa makofi ilipokuwa ikiondoka uwanjani. Hata hivyo, nyuso za wachezaji na benchi la ufundi hazikuwa na tabasamu. Baada ya yote, mabao ya dakika za nyongeza yaliyofungwa na Joshua Zirkzee na Patrick Dorgu hayakuzuia United kumaliza ikiwa katika eneo la kushuka daraja. Na kwa kuwa sasa mapumziko ya mechi za kimataifa yanaendelea, itabaki hapo kwa takribani wiki moja zaidi.

Ingawa bado ni mapema kiasi kwamba tishio la kushuka daraja halipaswi kuchukuliwa kwa uzito mkubwa, pia msimu umefika hatua ambayo nafasi kwenye msimamo ni chanzo halisi cha aibu. Na huenda hiyo ndiyo sababu wachezaji wa United walionekana wamekata tamaa mchezo wao wa mwisho ulipomalizika. United huenda isishuke daraja.

Sema unavyotaka kuhusu timu, wachezaji na kocha, lakini kwa kiasi kikubwa ni kundi lilelile lililomaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu England msimu uliopita. Kwa hiyo, bila shaka watakuwa na uwezo wa kutosha angalau kuepuka kushuka daraja. Hata hivyo, hali yao bado ni mbaya sana unapozingatia hadhi ya kihistoria ya klabu hiyo na matarajio yaliyopo.

POCHE 04

Ni kweli kwamba mara ya mwisho United ilipomaliza siku ikiwa katika timu tatu za mwisho za Ligi Kuu England kabla ya sasa haikuwa muda mrefu uliopita. Ilikuwa Agosti 2025, baada ya kufanya hivyo pia Agosti 2022. Lakini kuwa katika eneo la kushuka daraja mwezi Agosti kunatuambia tu kwamba timu huenda imepata matokeo mabaya moja au mawili mwanzoni mwa msimu. Ni mapema mno kwa hali hiyo kuwa kiashiria halisi cha matatizo.

Kwa mfano, United ilikuwa nafasi ya pili kutoka mwisho mwezi Agosti 2007, kabla ya kwenda kutwaa ubingwa. Kwa sehemu kubwa, kuwa katika eneo la kushuka daraja kabla ya Septemba hakumaanishi chochote. Hata hivyo, kuwa katika timu tatu za mwisho mwezi Novemba kunatoa picha tofauti zaidi, na kwa hiyo ni jambo la kulaumiwa kwa klabu yenye hadhi ya United.

United ilisukumwa katika timu tatu za mwisho majuzi kutokana na Nottingham Forest kuifunga Manchester City mabao 3-1. Hilo lilifanya iwe mara ya kwanza United kumaliza ikiwa katika eneo la kushuka daraja nje ya Agosti tangu Oktoba 1986, muda mfupi kabla ya Alex Ferguson kuteuliwa mwanzoni mwa Novemba kuwa kocha mkuu mpya.

POCHE 01

Wakati huo, United ilitumia siku 28 mfululizo katika eneo la kushuka daraja. Na sasa imehakikishiwa kuwa na kipindi chake kirefu zaidi katika timu tatu za mwisho, siku 15, tangu wakati huo kutokana na mapumziko ya mechi za kimataifa. Mchezo unaofuata wa United utakuwa Jumapili, Novemba 22, itakaposafiri kwenda Anfield kukutana na Liverpool.

Timu mbili zilizo chini yao, Sunderland na Crystal Palace, kila moja zitacheza kabla yao mwishoni mwa wiki hiyo. Kwa hiyo, inawezekana United ikaingia katika mchezo huo ikiwa mkiani mwa msimamo. Kwa vyovyote, matokeo ya timu nyingine hayataweza kuiondoa katika eneo la kushuka daraja. Na hata ushindi huenda usitoshe.

Iwapo United bado itakuwa katika eneo la kushuka daraja baada ya mechi ya 11, hilo litakuwa jambo kubwa kwa sababu itakuwa katika timu tatu za mwisho mwishoni mwa Novemba 22. Tangu United iliposhuka kutoka ligi ya daraja la juu 1974, tarehe ya mwisho zaidi katika msimu ambayo iliwahi kujikuta katika eneo la kushuka daraja ni Novemba 21, 1986.

Kauli ya ‘kuzama katika kina kipya cha matatizo’  imetumika sana kuhusiana na United katika kipindi cha miaka 13 iliyopita.

POCHE 02

Hata hivyo, haitakuwa na maana zaidi kuliko iwapo bado watakuwa katika timu tatu za mwisho baada ya mechi ya 11. Bila shaka, bado kutakuwa na muda mwingi wa kubadilisha mambo, lakini hawapaswi kujidanganya kwamba hali haiwezi kuwa mbaya zaidi. Inaweza.


NAMBA ZINAKUBALI, ZINAGOMEA HAPA

Lakini, kushuka daraja kwa United kuna uwezekano kiasi gani? Pointi nane katika mechi 10 bila shaka ni kiwango kibovu kinachostahili kuleta wasiwasi. Baada ya yote, kumekuwa na timu 41 zilizopata pointi nane katika hatua hii ya msimu wa Ligi Kuu England, na 17 kati yake, sawa na asilimia 41.5, hatimaye zilishuka daraja.

Katika matukio 10 ya hivi karibuni ambapo timu ilipata pointi nane katika mechi 10 za kwanza za msimu wa ligi hiyo, timu nne zilishuka daraja; Southampton (2022/23); Swansea (2017/18); Norwich (2013/14) na Wolves (2011/12)

United imepata ushindi mmoja pekee katika mechi 10 za ligi hadi sasa, ikiwa ni idadi ndogo zaidi ya ushindi iliowahi kupata katika hatua hiyo tangu 1930/31, ilipokuwa haijapata ushindi wowote.

Huo pia ulikuwa msimu wa mwisho ilipoanza kampeni ya ligi ya daraja la juu ikiwa na mechi nyingi zaidi bila kuweka rekodi ya kutoruhusu bao, ikiwa na mechi 12.  Opta katika utabiri wake hivi karibuni, iliitabiria United kushuka daraja kwa asilimia 20.9, kwani katika majaribio 10,000 ya kompyuta iliyofanya  ilishuka daraja mara 2,090.

Ni kweli kwamba bado kuna klabu saba zinazochukuliwa kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kushuka daraja, lakini linganisha kiwango hicho na makadirio yaliyotolewa kabla ya msimu kuanza.

Kabla ya msimu kuanza, United ilikuwa inapewa uwezekano wa asilimia 3.6 pekee wa kushuka daraja. Katika asilimia 41.7 ya majaribio, ilimaliza kwenye nafasi tano za juu, na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika makadirio ya hivi karibuni, ilimaliza nafasi ya tano au juu zaidi katika asilimia 2.8 pekee ya majaribio. Matumaini yoyote ya United kuibukia juu kama msimu uliopita yanaonekana yamekwisha, lakini hawapaswi kujidanganya kwamba hali haiwezi kuwa mbaya zaidi. Inaweza.