Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Simba nje wiki nne

CHILAMBO Pict

Muktasari:

  • Beki huyo ambaye amekuwa katika kiwango bora kwa msimu huu, amepata majeraha hayo wakati wa mechi ya kufuzu Fainali za Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), kati ya Tanzania dhidi ya Nigeria maarufu ‘Super Eagles’, Novemba 17, 2026.

SIMBA imepata pigo baada ya beki wa kulia wa kikosi hicho, Nathaniel Chilambo kupata majeraha ya mpasuko wa kano, hali itakayomfanya kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu hadi nne, jambo ambalo limetibua hesabu za timu hiyo msimu huu.

Beki huyo ambaye amekuwa katika kiwango bora kwa msimu huu, amepata majeraha hayo wakati wa mechi ya kufuzu Fainali za Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), kati ya Tanzania dhidi ya Nigeria maarufu ‘Super Eagles’, Novemba 17, 2026.

Katika mechi hiyo ya kundi L, iliyochezwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Complex, Zanzibar na kuisha kwa suluhu (0-0), beki huyo alipata majeraha hayo dakika ya 30, huku nafasi yake ikichukuliwa na kiungo mshambuliaji, Abdul Suleiman ‘Sopu’.

CHILA 02

Baada ya tathimini ya kina, beki huyo amegundulika amepata majeraha ya kupasuka nyama za paja na kusababisha kumweka nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu hadi nne, ikiwa ni pigo kwa Kocha Mkuu, Steve Barker kutokana na umuhimu wake kikosini.

Beki huyo aliyejiunga na Simba Julai 20, 2026, akitokea Azam FC, amekuwa muhimili katika timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker, akiwa ni mchezaji mzawa aliyesajiliwa msimu huu wa 2026-2027, mwenye uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza.

Taarifa hiyo ni pigo kwa Simba kutokana na umuhimu wa mchezaji huyo, ambaye licha ya kucheza kiasili beki wa kulia, ila ana uwezo wa kuingia katikati kusaidia eneo la kiungo, ikiwa ni moja ya faida kubwa inayomfanya kuendelea kung’ara pia.

CHILA 01

Beki huyo aliyechangia mabao mawili ya Ligi Kuu Bara kwa maana ya kutoa asisti, tangu ajiunge na kikosi hicho amekuwa ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango cha kuvutia, japo kuumia kwake ni pigo kwa timu hiyo kwa mechi zijazo zaidi.

Licha ya kuumia kwake, ila timu hiyo imepata ahueni baada ya urejeo wa nahodha wa timu hiyo, Shomari Kapombe ambaye pia alikuwa majeruhi wa muda mrefu, atakayesaidiana na beki mwenzake, David Kameta ‘Duchu’, kwa kipindi hicho cha wiki nne.

Kapombe ambaye ni mchezaji mzoefu ameanza mazoezi na timu hiyo ambayo inatarajia kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara kesho Jumamosi dhidi ya JKT Tanzania, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali, Isamuhyo, Mbweni, jijini, Dar es Salaam.

Beki huyo alipata nafasi ya kucheza mechi ya kirafiki ya ushindi wa timu hiyo wa bao 1-0, dhidi ya maafande wa Mashujaa FC, Novemba 14, 2026, ikiwa ni hatua nzuri kwake na ya kikosi hicho kiujumla ya kurejea upya katika ushindani msimu huu.

CHILA 03

Kapombe ni beki anayeweza kuzuia na kutengeneza mashambulizi kutokea pembeni ikiwa ni kazi pia iliyokuwa ikifanywa na Chilambo anayemudu kuingia kati kusaidia eneo la katikati, ambalo hucheza kiungo mkabaji wa timu hiyo, Yusuph Kagoma.