Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video ya ‘koneksheni’ yamtia matatani staa wa Real Madrid

CONECTION Pict

MADRID, HISPANIA: Raul Asencio wa Real Madrid anaweza kufungwa hadi miaka miwili na nusu jela huku waendesha mashtaka nchini Hispania wakitaka ahukumiwe kwa sakata la unyanyasaji wa kingono kwa mtoto.

NINI KILITOKEA?
Beki huyo wa Real Madrid anashtakiwa kwa kushea video ya ngono inayomhusisha mtoto. Muhtasari uliotolewa kwa The Athletic kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka unaeleza kuwa "wachezaji wawili wa zamani wa akademi ya Real Madrid walijihusisha kimapenzi kwa hiari na msichana mdogo pamoja na msichana mwingine na kurekodi tukio hilo bila idhini yao."

Inadaiwa kuwa Asencio aliziomba video hizo, ingawa hakuhusika katika tukio la kimapenzi, na baadaye akazionyesha kwa rafiki yake  jambo linalochukuliwa kuwa makosa mawili dhidi ya faragha, kwa mujibu wa Kifungu cha 77 cha Kanuni ya Adhabu ya Hispania. Waathirika wanaripotiwa kupata msongo wa mawazo (PTSD), na muhtasari huo unamtaka Asencio kuwalipa Euro 5,000 kila mmoja huku wanaume wengine watatu wakikabiliwa na uwezekano wa kifungo.

Kesi hiyo inahusiana na tukio lililotokea katika klabu ya ufukweni huko Gran Canaria mwaka 2023. Wachezaji wengine watatu  Ferran Ruiz, Juan Rodriguez, na Andres Garcia walikamatwa mwezi Septemba 2023. Asencio alihusishwa katika uchunguzi baada ya kuanza kuitwa kutoa ushahidi kama shahidi. Guardia Civil ilisema wakati huo kuwa kesi hiyo ilihusiana na "malalamiko ya kusambazwa kwa video ya faragha kupitia WhatsApp."

ASENCIO ALISEMA NINI?
Mnamo Mei 2025, Asencio alitoa tamko kufuatia nyaraka ya mahakama iliyokosewa na baadaye kusahihishwa kubainisha kuwa anakabiliwa na shtaka moja la kushiriki video ya ngono inayomhusisha mtoto:

"Sijawahi kushiriki katika tabia yoyote inayokiuka uhuru wa kingono wa mwanamke yeyote, achilia mbali watoto. Amri ya mahakama, kadri inavyonihusu, inaeleza tu uwezekano wa mimi kuwa nilitazama kwa muda mfupi picha hizo, bila kunihusisha moja kwa moja katika kurekodi au kusambaza."

"Shitaka lililotolewa dhidi yangu, kama lilivyoelezwa wazi na mahakama, bado ni la muda tu. Kwa hiyo, dhana ya kutokuwa na hatia lazima iendelee kushika nafasi. Iwapo mashtaka yataidhinishwa na kesi ya wazi kuanzishwa, nitaendelea kujitetea mbele ya Mahakama, ambayo nina imani nayo kikamilifu, nikisisitiza kuwa sijahusika na kosa lolote la jinai."

KIPI KINAFUATA?
Ilifichuliwa mwezi Februari kuwa mahakama ya Hispania ilikataa rufaa ya Asencio iliyokuwa ikipinga kusitishwa kwa muda kwa kesi hiyo. Wawakilishi wake wameiambia The Athletic kuwa "wana imani haki itatendeka" na kwamba kifungo kwa mteja wao kinaweza kuepukika.