Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vaibu la Lionel Messi akitua kambini

Muktasari:

  • Huu huenda ukiwa ni mwisho wake kufanya mazoezi na kikosi hicho akiwa nyumbani kama mchezaji wa timu hiyo ya taifa, kwani kuna kila dalili kwamba baada ya fainali za Kombe la Dunia miezi minne ijayo akastaafu kuichezea.

Buenos Aires, Argentina: DIRISHA la kimataifa la mechi za Fifa limemrejesha Lionel Messi kuungana tena na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Argentina, lakini vaibu la mashabiki wakati alipotua nchini humo limekuwa la kusisimua zaidi tofauti na wakati mwingine wowote.

Huu huenda ukiwa ni mwisho wake kufanya mazoezi na kikosi hicho akiwa nyumbani kama mchezaji wa timu hiyo ya taifa, kwani kuna kila dalili kwamba baada ya fainali za Kombe la Dunia miezi minne ijayo akastaafu kuichezea.

Nahodha huyo wa Argentina aliwasili katika kambi ya mazoezi ya Albiceleste akiwa na kumbukumbu nyingi huku akinywa juisi akisubiri kutimiza miaka 39 wakati wa Kombe la Dunia 2026.

Hata hivyo, kabla ya hapo, kuna michezo ya kirafiki ya kimataifa inayosubiriwa, mechi zitakazochukua nafasi ya Finalissima ambayo haikufanyika dhidi ya Hispania.

Wakati mshindi huyo mara nane wa Ballon D’or akiwasili nchini humo, mamia ya mashabiki walimpokea kwa bashasha na hata alipowasili katika uwanja wa mazoezi nyuma yake alisindikizwa na nyimbo za kumpongeza.

Lakini, katika kuhitimisha hilo kulikuwa na ujumbe wa Messi uliowasisimua mashabiki, kwani kama ilivyo kila anachofanya huwa habari, ndiyo maana macho yote yalikuwa kwake alipowasili katika uwanja wa mazoezi wa Ezeiza.

Akiwa huko, aliwashangaza wengi baada ya kuchapisha picha kadhaa katika akaunti yake ya Instagram pamoja na ujumbe maalumu uliosema: “La ilusion intacta, otra vez juntos (akimaanisha msisimko bado upo, pamoja tena).”

Ujumbe huo unaweza kuwa hisia zake kwa wachezaji wenzake kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo wao ni mabingwa watetezi.

Ni wazi kwamba Messi na Argentina wanapewa nafasi kubwa ya kushinda Kombe la Dunia. Lakini kabla ya fainali hizo kina Messi watakutana na Mauritania na Zambia katika dirisha hili la kalenda la Fifa, mechi ambazo huenda zikawa za mwisho kwake kucheza nyumbani Argentina akiwa amevaa jezi ya taifa lake.

Baada ya dirisha lijalo la kimataifa, Argentina itaendelea na maandalizi ya Kombe la Dunia nchini Marekani, ikilenga kutetea ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.