Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utata mwingine! Kauli ya Enzo Fernandez baada ya kusajiliwa Man City

ENZO Pict

Muktasari:

  • Fernandez, 25, alikamilisha uhamisho wake wa pauni 125 milioni kwenda Manchester City siku ya mwisho ya usajili, ada ambayo inalingana na rekodi ya uhamisho wa Uingereza iliyowekwa na Liverpool ilipomsajili Alexander Isak kutoka Newcastle msimu uliopita.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Argentina, Enzo Fernandez, ameingia katika hatari ya kuwakasirisha mashabiki wa Chelsea baada ya kudai kwamba kwa muda mrefu alikuwa akiota kucheza katika klabu kubwa kama Manchester City.

Fernandez, 25, alikamilisha uhamisho wake wa pauni 125 milioni kwenda Manchester City siku ya mwisho ya usajili, ada ambayo inalingana na rekodi ya uhamisho wa Uingereza iliyowekwa na Liverpool ilipomsajili Alexander Isak kutoka Newcastle msimu uliopita.

Kauli za Fernandez zimeibua hasira miongoni mwa mashabiki wa Chelsea, hasa kutokana na historia yake ya kutaka kuhusishwa na Real Madrid msimu uliopita. Wakati huo, alikasirisha mashabiki wa Chelsea na hatimaye kusimamishwa na klabu hiyo kwa mechi mbili.

Katika ujumbe wake wa kuwaaga mashabiki wa Chelsea kwenye mitandao ya kijamii, Fernandez amesema uamuzi wa kuondoka Stamford Bridge ulikuwa mgumu na kwamba kipindi chake cha mwisho klabuni hapo hakikuwa katika hali nzuri.

ENZ 01

“Maisha yanahusu kufanya maamuzi, na kwa sasa nimejikuta nikilazimika kufanya moja ya maamuzi hayo magumu. Nimesema hili hapo awali, lakini nataka kulisema tena: Nimeipenda sana klabu hii. Chelsea daima itakuwa katika mawazo yangu na zaidi ya yote, moyoni mwangu,” aliandika Fernandez.

Hata hivyo, licha ya kutoa maneno hayo ya kuaga, Fernandez alionekana kuepuka kulitaja jina la Chelsea moja kwa moja baada ya kujiunga na City, akiiita klabu yake ya zamani kuwa “klabu yangu iliyopita.”

Kauli hiyo imefanana na mwenendo wa kocha Enzo Maresca, ambaye naye aliepuka kuitaja Chelsea baada ya kujiunga na Manchester City, akirejea tu kama “klabu tofauti.”

Akizungumza baada ya kukamilisha uhamisho wake, Fernandez amesema amefurahi sana kutimiza ndoto yake ya kucheza katika klabu kubwa kama City.

ENZ 02

“Nina furaha sana kuwa hapa. Daima nimekuwa nikiota kucheza katika klabu kubwa kama City. Ninashukuru kwa nafasi hii. Ni wakati wa kihisia sana kwangu na familia yangu kuchukua hatua hii nikiwa na miaka 25 katika maisha ya soka ambayo nimekuwa nikiyaota,” amesema.

Fernandez ameongezakuwa tayari ameanza kuona ukubwa wa Manchester City na anaamini watafanikiwa kushinda mataji mengi pamoja.

“Manchester City lazima ishinde kila kombe inayoshiriki. Katika kila mashindano tunayocheza, tunapaswa kushindana na kushinda kwa sababu historia ya klabu hii inadai hivyo,” amesema.

Kiungo huyo pia alifichua kuwa hakusita hata kidogo baada ya City kumweleza kwamba inamtaka.

“Kusema kweli, tangu siku ya kwanza waliponiamini na kunipigia simu kuniambia kwamba walitaka nijiunge na klabu, sikusita hata kwa sekunde moja,” amesema.

ENZ 03

Fernandez pia alizungumzia kuungana tena na Maresca, ambaye aliwahi kufanya naye kazi katika klabu yake ya zamani.

“Ni kocha wa kiwango cha juu. Kwa kweli, nilifanya kazi naye katika klabu yangu iliyopita. Zilikuwa nyakati za kipekee na nilijifunza mengi kutoka kwake,” amesema.

Alimshukuru Maresca kwa mchango wake katika kufanikisha uhamisho huo, akisema kocha huyo alikuwa muhimu katika kumleta Manchester City.

“Ninashukuru pia kwa sababu alikuwa muhimu katika kunileta hapa. Ni furaha kubwa kufanya kazi naye tena na kufurahia safari hii,” amesema.

Fernandez amesema mchakato wa uhamisho huo haukuwa rahisi na kwamba yeye pamoja na Maresca walikuwa na hamu kubwa ya kuona dili hilo likikamilika.

“Siku chache zilizopita zilikuwa ndefu, lakini mwisho wa yote niko hapa na nina furaha sana kujiunga na klabu hii,” alimaliza.