Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upamecano agomea mkataba mpya aibukia rada za mabosi Old Trafford

TETESI Pict

Muktasari:

  • Man United inataka kufanya maboresho kwenye beki pia baada ya kunasa wachezaji watatu kwenye eneo la ushambuliaji, Bryan Mbeumo, Matheus Cunha na Benjamin Sesko.

MANCHESTER United imeripotiwa kutaka kufanya usajili wa kushtukiza wa kumnasa beki wa kati wa Bayern Munich, Dayot Upamecano kabla ya dirisha halijafungwa.

Man United inataka kufanya maboresho kwenye beki pia baada ya kunasa wachezaji watatu kwenye eneo la ushambuliaji, Bryan Mbeumo, Matheus Cunha na Benjamin Sesko.

Kocha Ruben Amorim anataka kuongeza beki baada ya dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana miamba hiyo kunasa saini za Lenny Yoro na Noussair Mazraoui. Na sasa Upamecano ameripotiwa kuwekwa kwenye rada za wababe hao wa Old Trafford.

Mkataba wa Upamecano huko Bayern utafika tamati mwishoni mwa msimu ujao na harakati za miamba hiyo ya Bundesliga kwa sasa ni kumsainisha dili jipya.

Kinachoelezwa ni kwamba Man United imefanya mazungumzo ya beki huyo ya kuongeza mkataba Bayern kuwa magumu baada ya kuonyesha dhamira ya kuhitaji saini yake ili akakipige kwenye Ligi Kuu England.

Staa huyo anaonekana kuvutiwa kuja kucheza katika ligi bora.


Mateus Fernandes

KLABU ya Southampton imekataa ofa ya awali ya West Ham United ya Pauni 30 milioni iliyowasilishwa kwa ajili ya kiungo wao wa kimataifa wa Ureno, 30, Mateus Fernandes, mwenye umri wa miaka 21. Fernandes ameonyesha kiwango bora msimu uliopita katika Ligi Kuu England akicheza michezo 33 na kutoa asisti 6.  Ripoti zinadai mabosi wa Soton wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kwa ajili ya kumuuza staa huyu.


Adam Wharton

REAL Madrid inaendelea kufuatilia maendeleo ya kiungo wa kimataifa wa England anayeichezea Crystal Palace, Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21.

Wharton aliingia katika rada za vigogo baada ya kiwango bora alichoonyesha akiwa na kikosi cha Palace msimu uliopita ambapo alicheza mechi 29 za Ligi Kuu England ambapo alifunga mabao matatu na kutoa asisti tano.

Mabosi wa Palace wanaripotiwa kuwa hawapo tayari kumwachia kwa sasa kwani itakuwa inaharibu mipango ya kocha wao kuelekea msimu ujao.


Marco Asensio

ASTON Villa inatarajiwa kumsajili mkataba wa kudumu kiungo wa Paris Saint-Germain, Mhispania Marco Asensio, mwenye umri wa miaka 29, baada ya kuonyesha kiwango bora sana akiwa kwa mkopo katika kikosi chao ambapo alifunga mabao tisa na kutoa asisti saba katika mechi katika mashindano yote. Ikiwa itashindikana kumsainisha mkataba wa kudumu kutokana na ada ya uhamisho, Villa inafikiria kuomba kumsajili tena kwa mkopo.


Ibrahima Konate

LIVERPOOL haina mpango wa kumuuza beki wao wa  kati wa kimataifa wa Ufaransa, Ibrahima Konate, mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha hili la usajili licha ya kuwa wapo katika harakati za kutaka kusajili mabeki wawili wa kati ili kuimarisha kikosi chao. Konate amekuwa akihusishwa na Real Madrid ambayo inataka kuwasilisha ofa hivi karibuni. Tangu ajiunge na Liverpool, Konate amecheza michezo 89 ya michuano yote.


Nkunku

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Christopher Nkunku, mwenye umri wa miaka 27, anatamani kujiunga na Bayern Munich katika dirisha hili ambapo ameomba kuondoka Chelsea baada ya kuona nafasi yake katika kikosi cha kwanza imezidi kuwa hafifu. Nkunku msimu uliopita alicheza mechi 14 za Ligi Kuu England na kufunga mabao matano.


Facundo Buonanotte

BAYER Leverkusen imeonyesha nia ya kumsajili winga wa Argentina anayeichezea Brighton, Facundo Buonanotte, mwenye umri wa miaka 20. Brighton imeripotiwa kuwa tayari kumuuza kwa takribani Pauni 39 mioni kiasi ambacho kinaonekana kuwa kikubwa kwa Leverkusen. Ripoti kutoka tovuti ya Kicker, imefichua kuwa Leverkusen inataka kutoa Pauni 30 milioni kama ada kumsajili.


Fabio Silva

BORUSSIA Dortmund imejiondoa kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Wolves na timu ya taifa ya Ureno, Fabio Silva, mwenye umri wa miaka 23, baada ya kuona timu yake imeongeza bei.

Dortmund inadaiwa kutaka kulipa Euro 30 milioni kwa ajili ya Fabio lakini Wolves inahitaji Euro 40 milioni kiasi ambacho ndio kinaripotiwa kuwa changamoto hadi sasa.

Tangu ajiunge nayo mwaka 2020, Silva amechezea mechi 91 na kufunga mabao 15..

Msimu uliopita alicheza mechi 28 za michuano yote na kufunga mabao manne. d