Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yashusha winga wa Nabi

WINGA Pict


MASHABIKI wa Simba wanachekelea namna usajili wa kikosi chao unavyoendelea huku tajiri wao Mohammed Dewji ‘MO’ akiwakosha zaidi akisema wanasuka timu lakini kule Yanga nako wanafanya yao wakishusha watu wao wapya sasa kocha wa zamani wa mabingwa hao amefunguka harakati hizo.


Kocha aliyezungumzia hayo ni Nasreddine Nabi ambaye aliwahi kufanya kazi Yanga kwa mafanikio makubwa, ameliambia Mwanaspoti kuwa Simba imemuumiza kwa kumchukua winga Keletso Makgalwa ambaye alitaka ajiunge naye nchini Morocco.


Nabi ambaye kwasasa anaifundisha Raja Athletic ya Morocco, amesema Makgalwa alikuwa kwenye hesabu zake lakini kuna mambo yakachelewa kwa Waarabu hao na Simba kufanya mambo kwa haraka na kumchukua.

Kocha huyo amesema Simba imepata winga mzuri mwenye kasi na akili ya kujua kuwapangua mabeki, ambapo ataiongezea nguvu timu hiyo msimu ujao, akisifu kwamba wekundun hao walifanya usajili sahihi.

“Simba nimeona wamemchukua Keletso(Makgalwa) ni mchezaji mzuri sana, wameniwahi, nilikuwa nataka aje Morocco hapa Raja lakini kuna mambo yakachelewa, wamepata mchezaji mzuri Simba naona ni usajili bora sana kwenye timu hiyo kwa sasa,”amesema Nabi.

“Ni winga ambaye anajua kukimbia ana kasi lakini pia anajua kuwapangua mabeki, ni mchezaji mwenye nishati ya kutosha, sijui ataanza kwa bahati gani akiwa huko lakini alipokuwa Afrika Kusini alikuwa anafanya vizuri sana na timu nyingi zilikuwa zikimfuatilia, kwangu naona ni usajili bora," amesema Nabi ambaye amekuwa akifuatia ligi kuu kwa muda mrefu.

Makgalwa alituia nchini alfajiri ya kuamkia jana na kunaswa na Mwanaspoti, ambapo anatarajiwa kutambulishwa hivi karibuni kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na Simba msimu huu akitokea Sekhukhune ya Afrika Kusini.

Mbali na winga huyo, Nabi pia alimzungumzia kocha mpya wa Yanga Manqoba Mngqithi na kusema kuwa timu hiyo imefanikiwa kupata mtu sahihi kwenye benchi lake.

Nabi amesema kocha huyo ni mmoja wa makocha wenye heshima kubwa nchini Afrika Kusini.

“Nimeona Yanga nao wamemchukua kocha Manqoba ni kocha mzuri, niliwahi kukutana naye wakati akiwa Mamelodi na mimi Kaizer Chiefs bahati mbaya nilipoteza, kikosi changu hakikuwa na nguvu kuonyesha makali mbele ya Mamelodi wakati huo.

“Ni kocha mzuri anacheza soka la kushambulia na kasi kidogo, naijua Yanga kama atapata ushirikiano ambao naufahamu basi atafanikiwa wamepata kocha mzuri anayejua kuwajenga wachezaji wake kufanya makubwa.

“Nadhani ligi ya huko itakuwa na ushindani zaidi msimu ujao unaona Simba na Yanga wana makocha wanaojuana lakini Azam nao wana kocha mzuri rafiki yangu Florent Ibenge, mtaona ligi bora sana.”