Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UKIZUBAA UMELIWA: Mamelodi, Inter Milan, Dortmund zarusha kete muhimu Kombe la Dunia

USA Pict

Muktasari:

  • Mamelodi Sundowns itarusha kete yake ya pili kwenye michuano hiyo, wakati itakapokabiliana na vigogo wa Bundesliga, Borussia Dortmund katika kipute kitakachofanyika usiku wa Jumamosi.

LOS ANGELES, MAREKANI: HUKO kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu mambo yamezidi kunoga.

Mamelodi Sundowns itarusha kete yake ya pili kwenye michuano hiyo, wakati itakapokabiliana na vigogo wa Bundesliga, Borussia Dortmund katika kipute kitakachofanyika usiku wa Jumamosi.

Si wengi waliokuwa wakiipa Mamelodi Sundowns nafasi ya kushinda hata mechi moja kwenye fainali hizo, hasa huko kwao Afrika Kusini. Lakini, mabingwa hao wa ligi ya Sauzi, waliziba masikio na kuachana na kelele za watu kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ulsan na hivyo kuandikisha ushindi wao wa kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu, Jumatano iliyopita.

Kinachoshangaza sasa, miamba hiyo maarufu kama Brazilians sasa inaongoza Kundi F baada ya Fluminense na Borussia Dortmund kutoka sare kwenye mechi nyingine ya kundi hilo.

Ushindi kwenye mechi ya Jumamosi hii dhidi ya BVB utatosha kwa Mamelodi kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo.

Hata hivyo, ni rahisi kuzungumza kuliko kufanya. Dortmund hakuwa kwenye kiwango bora kabisa mechi ya kwanza na bila shaka kocha Niko Kovac atakuwa ametoa onyo kali kwa wachezaji wake kitu ambacho kitafanya mechi yao ya Mamelodi kuwa na upinzani mkali uwanjani.

Dortmund inaamini inahitaji kushinda mechi hiyo ili kujiweka pazuri kwenye mchakamchaka wa kusonga hatua inayofuata. Hilo ndilo litakalofanya mechi hiyo kuwa na upinzani mkali.

Mamelodi Sundowns inaweza kuridhika na kiwango cha washambuliaji wake kwenye mechi dhidi ya Ulsan, ambapo ilipiga mashuti 14. Iqraam Rayners angeweza kufunga hat-trick katika mechi hiyo, lakini mabao yake mawili yalikataliwa. Hilo linaonekana kikosi hicho cha kocha Miguel Cardoso kimepania kufanya kitu kwenye fainali hizo, hivyo Dortmund watakuwa na kazi nzito ya kuwazuia washambuliaji wa timu hiyo ya kutoka Afrika Kusini.

Dortmund ni timu yenye fowadi matata kabisa ndani ya uwanja kitu ambacho kinaweza kuleta ushindi mkali kwenye mechi hiyo na kushuhudia vuta nikuvute. Kazi ipo.

Mikikimikiki hiyo pia ilishuhudiwa mechi za usiku wa kuamkia Jumamosi, ambapo saa 7:00 usiku kulikuwa na kipute matata kabisa, ambapo Los Angeles FC ilitupa kete yake ya pili kwa kumenyana na wawakilishi wengine wa Afrika, Esperance katika mechi iliyotazamiwa kuwa na upinzani mkali katika Kundi D.

Timu hizo kila moja itasaka ushindi wake wa kwanza, jambo ambalo litafanya kuwa mchezo utakaokuwa na mvuto mkubwa wa kuutazama.

Mechi nyingine ya usiku wa kuamikia Jumamosi ilipigwa alfajiri ya saa 10:00, ambapo Bayern Munich ilikuwa na shughuli pevu ya kukabiliana na Boca Juniors.

Mchezo mwingine wa michuano hiyo utakaopigwa usiku wa Jumamosi, utaikutanisha miamba iliyofika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, Inter Milan itakapochuana na Urawa Red Diamonds. Inter yenyewe pia itahitaji ushindi wa kwanza baada ya kutoka sare katika mechi ya kwanza, sawa na ilivyo kwa Urawa, ambayo yalipoteza mechi yao ya kwanza ilipokipiga na River Plate. Mambo ni moto kwelikweli.

Vikosi vinavyotarajiwa:     Mamelodi Sundowns: Williams; Mudau, Kekana, Cupido, Lunga; Allende Bravo, Mokoena; Ribeiro, Arthur Sales, Zwane; Rayners

Borussia Dortmund: Kobel; Sule, Anton, Bensebaini; Ryerson, Sabitzer, Gross, Svensson; Brandt, Adeyemi, Guirassey.