Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhondo… Maisha yalivyokuwa wikiendi hii Ulaya

UHONDO Pict

Muktasari:

  • Mabao mawili ndani ya dakika saba yaliyofungwa na Tajon Buchanan na Tani Oluwaseyi yaliipa Villarreal uongozi katika Uwanja wa Camp Nou na hali ilizidi kuwa mbaya kwa Barcelona baada ya winga Lamine Yamal kukosa penalti katika kipindi cha kwanza.

BARCELONA, HISPANIA: BAADA ya kukubali mabao mawili kutikisa nyavu zake mapema tu, Barcelona ilifanikiwa kurejea kutoka nyuma na kuifunga Villarreal mabao 3-2 nyumbani, na hivyo kurejesha pengo la pointi tatu kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Hispania (La Liga).

Mabao mawili ndani ya dakika saba yaliyofungwa na Tajon Buchanan na Tani Oluwaseyi yaliipa Villarreal uongozi katika Uwanja wa Camp Nou na hali ilizidi kuwa mbaya kwa Barcelona baada ya winga Lamine Yamal kukosa penalti katika kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, miamba hiyo ya Catalonia ilionyesha uwezo mkubwa wa kupambana na kurejea mchezoni kwa kufunga mabao matatu ndani ya dakika 11 za kipindi cha pili na kupata ushindi. Gerard Martín na Fermin Lopez waliisawazishia Barcelona kabla ya bao la kujifunga la Pau Navarro kuipa ushindi.

Barcelona sasa imeshinda michezo minne mfululizo katika mashindano yote tangu ilipofungwa na Real Madrid katika El Clasico mwezi Oktoba. Ushindi huo umeirejeshea pengo la pointi tatu dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho, ambacho kilikuwa kimefikia idadi sawa ya pointi baada ya kuifunga Celta Vigo.

Buchanan aliifungia Villarreal bao la kwanza dakika ya tano kwa shuti kali la umbali mrefu baada ya López kupoteza mpira, na dakika mbili baadaye, wageni waliongeza bao la pili kupitia Mkanada mwingine, Oluwaseyi, ambaye alipenya upande wa kushoto kabla ya kupiga shuti kali lililoingia juu kabisa mwa lango.

Kikosi cha Hansi Flick kilipaswa kupunguza bao moja baada ya Oluwaseyi kumuangusha Yamal ndani ya eneo la hatari. Mwamuzi alitoa penalti baada ya kupitia mfumo wa VAR.

UHOND 03

Nyota huyo alijichukulia jukumu la kupiga penalti lakini shuti lake lilipita pembeni baada ya kugonga mwamba wa lango. Hata hivyo, Barca ilirejea kipindi cha pili ikiwa na ari mpya. Peter Gulacsi aliokoa shuti la chini la López kabla ya Martín kufunga kwa kichwa dakika ya 57 akitumia krosi ya Pedri.

Dakika nne baadaye, López alifunga bao la pili kwa shuti kali baada ya kutengenezewa nafasi na Yamal. Bao la tatu halikuchukua muda kwani pasi ya kisigino ya Yamal ilimfikia Eric Garcia, ambaye alitoa krosi iliyomgonga Navarro na kuingia wavuni, na hivyo kujifunga mwenyewe.

Navarro baadaye alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano, na kuhitimisha siku mbaya kwake.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Atletico Madrid iliendeleza presha kwa vinara kwa vinara wawili wa La Liga baada ya kupata ushindi rahisi wa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao wa jiji, Getafe.

Kikosi hicho cha Diego Simeone sasa kiko nyuma ya Barcelona kwa pointi tano na Real Madrid pointi mbili.

Mabao ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Álex Baena na Johnny Cardoso, yote yakitengenezwa na Julian Alvarez, yaliihakikishia Atletico ushindi katika Uwanja wa Coliseum, uliopo katika viunga vya kusini mwa mji mkuu wa Hispania.

Álex Grimaldo alikamilisha ushindi huo kwa penalti katika muda wa nyongeza baada ya Djene Dakonam wa Getafe kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Alexander Sorloth.


UHOND 01

SERIE A

Katika Ligi Kuu Italia (Serie A), Atalanta iliokoa pointi moja kwa namna ya kushangaza baada ya kutoka nyuma na kupata sare ya mabao 4-4 dhidi ya Inter Milan.

Matokeo hayo yaliifanya Inter kubaki nyuma kwa pointi tatu katika mbio za ubingwa, licha ya Pio Esposito kufunga hat-trick.

Inter ilionekana kuwa na uhakika wa ushindi mjini Bergamo baada ya penalti ya Petar Sucic kuwapa uongozi wa mabao mawili dakika ya 76, kufuatia mabao ya Esposito. Hata hivyo, bao la pili la Charles De Ketelaere katika mchezo huo pamoja na penalti ya Franck Kessié katika muda wa nyongeza yaliisaidia Atalanta kutoka na pointi moja.

Hii ilikuwa mara ya tatu pekee msimu huu kwa Inter kupoteza pointi katika ligi, lakini matokeo hayo yalikifanya kikosi hicho cha Cristian Chivu kubaki nafasi ya tatu, kikiwa pointi moja nyuma ya Roma na tatu nyuma ya vinara, Lazio.

Esposito alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza, akifungua ukurasa wa mabao baada ya kuuwahi mpira uliopanguliwa ndani ya eneo la hatari na kuupachika wavuni. Baadaye aliongeza bao la pili kwa kichwa akitumia mpira wa kona. Eljif Elmas aliifungia Atalanta bao la kwanza na kuifanya mechi iendelee kuwa na ushindani. Hata hivyo, Esposito alikamilisha hat-trick yake mwanzoni mwa kipindi cha pili kwa utulivu mkubwa. Hilo lilikuwa bao lake la nane katika michezo mitano aliyocheza kwa klabu na timu ya taifa.

De Ketelaere ndiye aliyekuwa chachu ya Atalanta kurejea mchezoni  akifunga bao kwa kichwa kabla ya kuongeza jingine kwa shuti kali, huku bao la penalti la Sucic likiwa katikati ya mabao hayo.

Hali hiyo iliandaa dakika za mwisho zenye msisimko mkubwa huku Atalanta ikisaka sare ambayo mwanzoni ilionekana kuwa ngumu kuipata.

Hatimaye, timu hiyo ilipata penalti baada ya mpira kugusa mkono wa mchezaji wa Inter, na Kessie akaitumia nafasi hiyo kwa utulivu na kusawazisha matokeo.

Kwingineko Kocha wa Juventus, Luciano Spalletti amefikisha rekodi ya mechi 600 akiwa kocha katika Ligi Kuu Italia (Serie A) kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Venezia.

Ushindi huo uliifanya Juventus kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, baada ya kuonyesha kiwango bora katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Ushindi huo uliendeleza rekodi ya kutopoteza katika michezo minne mfululizo kwenye mashindano yote. Nick Woltemade alibadilisha mwelekeo wa mchezo baada ya kuingia akitokea benchi, aliuwahi mpira uliokuwa hauna mchezaji na kuupachika wavuni, na kufunga bao lake la pili la ligi katika michezo miwili.

Baadaye alitoa pasi ya bao kwa Teun Koopmeiners, ambaye alifunga kwa shuti kali, huku Juan Cabal akifunga bao la tatu kwa kichwa kabla ya Kolo Muani kuchezewa madhambi na kupata penalti, kisha kuifunga na kukamilisha ushindi huo mkubwa. Mabao yote manne yalifungwa kati ya dakika ya 53 na 71.

Nayo AC Milan ilirejea katika nafasi nne za juu baada ya kuifunga Frosinone mabao 5-1, huku Gonçalo Ramos akimaliza ukame wa mabao.

Huo ulikuwa ushindi wa pili mfululizo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja na kupanda hadi nafasi ya nne, ikiwa pointi tano nyuma ya vinara, Lazio.

Ramos, ambaye alisajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu, alifanikiwa kumaliza ukame wa kutofunga katika michezo mitano mfululizo, ambapo

Milan ilianza kwa kasi baada ya kujipatia bao kupitia mchezaji wa Frosinone, Gabriele Calvani, aliyejifunga. Ramos aliongeza bao la pili kwa utulivu ndani ya dakika 19 za mwanzo.

Kabla ya mchezo huo, kocha Ruben Amorim alikuwa amewakosoa wachezaji wake kwa “kutomsaidia Ramos”, ambaye alikuwa amefunga mabao mawili pekee katika michezo 11 ya kwanza ya ligi tangu alipohamia kutoka PSG majira ya kiangazi.

Bao lake la tatu lilipokewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wa San Siro baada ya kutengenezewa asisti na Adrien Rabiot ambaye naye aliweka historia kwa kuwa kiungo wa kwanza wa Milan tangu Kaka mwaka 2004 kufunga bao au kutoa asisti katika michezo saba mfululizo ya ligi.

Wageni walifanikiwa kupata bao kupitia Patrizio Masini, lakini Milan waliongeza kasi kipindi cha pili kupitia mashambulizi ya kushtukiza.

Wachezaji walioingia kutoka benchi, Ardon Jashari na Alphadjo Cisse, walifunga mabao kabla ya Christian Pulisic kukamilisha ushindi huo mkubwa kwa bao bora. Huo ulikuwa ushindi mkubwa zaidi katika kipindi cha uongozi wa Amorim.

Katika michezo mingine, Milutin Osmajic alifunga mabao mawili na kuisaidia Genoa kuifunga Sassuolo mabao 2-0, huku Bologna ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Udinese, ambayo iliondoka katika nafasi ya mwisho ya msimamo na kuiacha Venezia ikiwa mkiani.


UHOND 02

LIGUE 1

Katika Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1), Paris FC ilipanda hadi nafasi ya pili nyuma ya wapinzani wao wa jiji, PSG baada ya kuifunga Angers mabao 4-0 nyumbani.

Patrick Zabi, Luca Koleosho, Maxime Lopez na Diego Coppola wote walifunga mabao katika kipindi cha pili kwa timu hiyo inayofundishwa na Liam Rosenior, kocha wa zamani wa Chelsea, na ambayo imekuwa katika kiwango kizuri.

Nayo Le Mans ilifunga bao la ushindi dakika ya tano ya muda wa nyongeza na kukamilisha ushindi wa kusisimua wa mabao 3-2 dhidi ya Marseille ugenini. Ushindi huo uliisaidia Le Mans kujiondoa katika eneo la kushuka daraja.

Jean Vercruysse aliyeingia kutokea benchi ndiye aliyefunga bao la ushindi na kukatiza mfululizo wa ushindi wa michezo mitano ya ligi kwa Marseille.

Marseille ilionekana kuwa na udhibiti kamili wa mchezo baada ya Amine Gouiri kufunga bao katika mchezo wake wa nne mfululizo na winga Mbrazili Igor Paixao kuongeza la pili katika kipindi cha kwanza. Louis Mafouta alipunguza pengo kwa mkwaju wa faulo dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika.

Hata hivyo, alikosa nafasi ya kusawazisha baada ya penalti yake kuokolewa dakika ya 78. Erwan Colas alisawazisha dakika sita baadaye kabla ya Vercruysse kufunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuipa Le Mans pointi zote tatu. Nayo Lorient ilimalizana na Rennes kwa kufungana bao 1-1.


BUNDESLIGA

Katika Ligi Kuu Ujerumani, wikiendi ilimalizika kwa Dabi ya Hamburg kuishuhudia Werder Bremen ikiirarua Hamburger SV kwa mabao 4-0, huku Augusburg ikiichapa Mainz 3-1.