Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sowah afichua siri ya kuiua Azam

SOWAH Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Novemba 20, 2026 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Azam FC ilianza kwa kasi na kupata mabao mawili ndani ya dakika 30 za kipindi cha kwanza, kupitia Feisal Salum aliyefunga dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti na Zidane Sereri aliyeongeza la pili dakika ya 29.

MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah amefichua siri iliyowasaidia kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC, akisema imani na nidhamu ya kuendelea kucheza soka lao hata walipokuwa nyuma kwa mabao mawili ndiyo iliyowapa nguvu ya kugeuza matokeo.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Novemba 20, 2026 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Azam FC ilianza kwa kasi na kupata mabao mawili ndani ya dakika 30 za kipindi cha kwanza, kupitia Feisal Salum aliyefunga dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti na Zidane Sereri aliyeongeza la pili dakika ya 29.

Hata hivyo, Singida Black Stars haikukubali matokeo hayo ya mapema yawavunje moyo, kwani iliendelea kutafuta njia ya kurejea mchezoni na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 40 kupitia Emmanuel Keyekeh. Wakaenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1.

SOW 02

Kipindi cha pili kilikuwa na sura tofauti baada ya Singida kuongeza kasi ya mashambulizi na kuanza kuitawala mechi, juhudi zilizozalisha bao la kusawazisha kupitia James Mwashinga dakika ya 51 na kurejesha matumaini ya kupata ushindi.

Baada ya kusawazisha, Singida iliendelea kutumia nafasi ilizozipata na dakika ya 68 Sowah akaifungia timu hiyo bao la tatu, kabla ya kurejea tena dakika ya 72 na kufunga la nne, akihakikisha timu yake inaondoka na ushindi wa mabao 4-2 katika mchezo ambao ilianza ikiwa kwenye wakati mgumu.

Akizungumzia namna walivyoweza kugeuza matokeo hayo, Sowah amesema hawakupoteza imani baada ya kuruhusu mabao mawili, badala yake waliamua kuendelea kucheza soka lao huku wakijitahidi kuongeza presha ya mshambulizi.

“Tuliamini kwamba tunaweza kufanya kitu, hivyo tuliamua kuendelea kucheza soka letu huku tukitengeneza nafasi tukiwa na tahadhari ya kutoruhusu mabao mengine.Hilo lilitusaidia kurejea mchezoni,” amesema na kuongeza;

SOW 01

“Kuendelea kufunga ni jambo zuri kama mshambuliaji, lakini jambo zuri zaidi ni kusaidia timu kupata matokeo ambayo yanatufanya kuongeza alama tatu muhimu.”

Mabao hayo mawili yamemfanya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana kufikisha 21 katika Ligi Kuu Bara tangu alipotua nchini dirisha dogo la usajili Januari 2024-2025.

Katika msimu wa 2024/25, ambao ulikuwa wa kwanza kwake kucheza Ligi Kuu Bara, Sowah alifanya vizuri akiwa na Singida Black Stars kwa kufunga mabao 13, kabla ya kujiunga na Simba msimu uliofuata ambako alifunga mabao matatu ya ligi, kisha kurejea Singida msimu huu wa 2026/27.