Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubingwa upo: Carrick atuliza mzuka Man United

UBIUNGWA Pict

Muktasari:

  • United ilitumia pauni148 milioni  kusajili wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili, kiasi ambacho ni kidogo kuliko fedha zilizotumiwa na Ipswich Town, klabu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inaamini bado inaweza kuwania mataji makubwa licha ya kushindwa kufikia kiwango cha matumizi ya fedha kinachoonyeshwa na baadhi ya wapinzani wake kwenye usajili.


United ilitumia pauni148 milioni  kusajili wachezaji wapya katika dirisha hili la usajili, kiasi ambacho ni kidogo kuliko fedha zilizotumiwa na Ipswich Town, klabu iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.

Chelsea na Tottenham zilitumia zaidi ya pauni300 milioni kila moja, huku Manchester City ikiweka rekodi kwa kutumia takribani pauni458 milioni.

Tofauti hiyo ya matumizi ilionekana pia katika ushindi wa Liverpool dhidi ya Ipswich Ijumaa usiku, ambapo Liverpool iliwaanza wachezaji watatu Alexander Isak, Bradley Barcola na Florian Wirtz ambao kila mmoja aligharimu zaidi ya pauni100 milioni.

Kwa upande wa United, usajili ghali zaidi katika dirisha hili ni kiungo wa Cameroon, Carlos Baleba, aliyesajiliwa kutoka Brighton kwa mkataba ambao unaweza kufikia pauni70 milioni.

Kiasi hicho bado kiko pauni19 milioni chini ya rekodi ya klabu ya pauni89 milioni iliyotumika kumsajili Paul Pogba miaka 10 iliyopita.

Hata hivyo, kocha mkuu Michael Carrick anaamini fedha pekee haziwezi kuwa jibu la kujenga timu yenye mafanikio na amesisitiza United inaweza kushindana na wapinzani wake.

“Hakika naamini tunaweza. Changamoto ni kupata muunganiko sahihi, uwiano mzuri na kundi sahihi la wachezaji; kuwa na wachezaji bora ambao wanaweza kuwaendeleza wengine. Iwe unahitaji uzoefu au wachezaji vijana,” amesemsa Carrick.


UB 01

MAPUNGUFU YATAJWA

Mbinu ya United katika usajili imekosolewa na baadhi ya wadau, huku ukosefu wa beki wa kushoto wa kushindana na Luke Shaw pamoja na kutokuwepo kwa mshambuliaji wa kumsaidia Benjamin Sesko vikitajwa kuwa miongoni mwa mapungufu ya kikosi.

Carrick amekataa madai kwamba uongozi wa klabu uliweka vikwazo katika matumizi ya fedha wakati wa dirisha hili.

“Naelewa kwamba kiasi halisi cha fedha kinaweza kuwa jambo kubwa, lakini si lazima kila mara kiwe jibu,” amesemsa.


UB 02

DENI LA UNITED

Maswali kuhusu uwezo wa United kutumia fedha yamekuwa yakihusishwa pia na madeni makubwa ya klabu.

Mjadala huo uliibuliwa katika mkutano wa Fans Forum mwishoni mwa Juni, huku mchambuzi wa masuala ya fedha, Swiss Ramble akikadiria Septemba 2025 kuwa United ilikuwa imelipa takribani pauni852 milioni  kwa riba pekee tangu familia ya Glazer iliponunua klabu hiyo mwaka 2005.

Takwimu za hivi karibuni za kifedha za klabu zinaonyesha kuwa jumla ya madeni yake imefikia pauni1.29 bilioni, kiasi kinachojumuisha pia ada za usajili wa wachezaji ambazo bado hazijalipwa.

United pia, iliongeza deni jingine la pauni91.92 milioni baada ya kurekebisha upya mikopo yake ya hati fungani mwezi Juni.

Wakati huohuo, klabu bado haijaweka wazi itakavyogharamia ujenzi wa uwanja mpya unaokadiriwa kugharimu zaidi ya pauni2 bilioni.

Ripoti kamili za mwaka wa kifedha unaoishia Juni 30 zinatarajiwa kutolewa katika wiki zijazo na zitatoa picha mpya kuhusu hali ya kifedha ya klabu, hasa baada ya kumaliza msimu uliopita bila kushiriki mashindano ya Ulaya.

UB 04

Licha ya hali hiyo, mashabiki wameendelea kuandamana dhidi ya familia ya Glazer karibu kila mechi.

Hata hivyo, mtendaji mkuu wa klabu, Omar Berrada, anaamini United inaweza kuendelea kuwa na ushindani huku ikisimamia madeni yake na mipango ya kujenga uwanja mpya.

“Tumeonyesha kwamba tukiwa na deni, si tu kwamba tunaweza kupata faida, bali muhimu zaidi tunaweza kushinda mataji. Na lengo letu ni kufanya hivyo tena,” amesemsa Berrada katika Fans Forum ya klabu Julai 30.

Aliongeza “jukumu letu kama uongozi ni kuhakikisha tunaendesha klabu kwa ushindani huku tukiwa na mfumo wa kifedha endelevu.

“Tunataka pia kujenga uwanja mpya, lakini tunapaswa kufanya hivyo kwa namna itakayotuwezesha kuendelea kuwa na ushindani.

“Tunapaswa kuwa na nidhamu na kuendelea kufanya uamuzi sahihi uwanjani ili tuwe katika nafasi ya kusimamia deni, kujenga uwanja mpya na, muhimu zaidi, kujaribu kushinda mataji mengi iwezekanavyo.”


UB 03

CARRICK ANAONA MWANGA

Usajili wa Baleba, Andrey Santos kutoka Chelsea na Youri Tielemans kutoka Aston Villa, pamoja na kuibuka kwa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19, Shea Lacey, umemfanya Carrick kuamini kikosi chake sasa kiko katika hali nzuri zaidi kuliko kilivyokuwa mwishoni mwa msimu uliopita.

United ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya tatu baada ya Carrick kushinda mechi 12 kati ya 17 alizoisimamia.

“Ukiwa katika klabu hii, lazima ulazimishe ushindi. Hapo ndipo tunapotaka kuwa na tunataka kufikia kiwango hicho kwa uendelevu,” amesemsa.

“Sipendi kuendelea kuangalia nyuma, lakini wanajua kilichohitajika kuandaa mwenendo ule. Ni kweli kulikuwa na mashindano moja tu, hivyo tunahitaji kufanya hivyo mara nyingi zaidi msimu huu.

“Lakini tumeimarisha kikosi, kwa hiyo tunaamini kuna mambo makubwa yanayowezekana.”

Iwapo matumaini hayo yana msingi yataanza kuonekana katika miezi ijayo, lakini Carrick anaamini United imeunda kikosi kinachoweza kupambana kuwania mataji licha ya kutumia fedha chache zaidi kuliko wapinzani wake wengi.