Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gomez aiokoa Yanga Botswana dakika za jioni!

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa leo Septemba 5, 2026 kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Botswana, ilishuhudia Gaborone ikitangulia kupata bao dakika ya 33, kupitia wa mshambuliaji raia wa Namibia, Aubrey Amseb aliyepiga frii-kiki kali iliyomshinda kipa, Djigui Diarra.

BAO la dakika ya 90+5, lililofungwa na mshambuliaji, Seleman Mwalimu 'Gomez', limetosha kuiokoa Yanga na kichapo dhidi ya Gaborone United, baada ya wenyeji kutangulia mapema dakika ya 33, kupitia Aubrey Amseb.

Katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa leo Septemba 5, 2026 kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Botswana, ilishuhudia Gaborone ikitangulia kupata bao dakika ya 33, kupitia wa mshambuliaji raia wa Namibia, Aubrey Amseb aliyepiga frii-kiki kali iliyomshinda kipa, Djigui Diarra.

Wakati Gaborone ikiamini mechi hiyo inaondoka na ushindi, Seleman Mwalimu 'Gomez' aliyeingia dakika ya 81, akichukua nafasi ya Peter Shalulile, ndiye aliyekuwa mwokozi kwa Yanga, baada ya kufunga bao muhimu la kusawazisha.

Gomez alifunga bao hilo lililotokana na mashambulizi ya mara kwa mara ambayo Yanga ilikuwa inatengeneza baada ya wenyeji wao, Gaborone United kujikita zaidi kuzuia ili kulinda uongozi wao, kabla ya mechi ya pili ya marudiano.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga msimu huu kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco, anakuwa ni mchezaji wa kwanza wa Yanga msimu huu kufunga bao katika michuano ya kimataifa, baada ya msimu uliopita kucheza kwa watani zao wa jadi, Simba.

Bao lililofungwa na Aubrey Amseb, linamfanya kuandika rekodi mpya ya kufunga bao lake la kwanza pia la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kikosi hicho cha Gaborone, tangu alipojiunga nacho, Januari 12, 2026, akitokea Young African ya kwao Namibia.

Licha ya Yanga kupata sare mechi hiyo, ila imekuwa na mwenendo mzuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika kwa misimu ya hivi karibuni, kwani tangu mara ya mwisho ilipotolewa hatua ya kwanza msimu wa 2021-2022, haijatolewa tena mapema.

Msimu wa 2021-2022, ndio ulikuwa wa mwisho kwa Yanga kushindwa kuvuka hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kutolewa kwa mshangao na Rivers United ya Nigeria kwa jumla ya mabao 2-0.

Yanga iliyokuwa inajitafuta katika ufalme wa michuano ya kimataifa, ilianza kuchapwa bao 1-0 na Rivers United, Septemba 12, 2021, huku marudiano yaliyofanyika Nigeria Septemba 19, 2021 ikachapwa tena 1-0 na kuaga kwa jumla ya mabao 2-0.

Tangu iliposhangazwa na River United, Yanga imekuwa na mwenendo mzuri katika michuano ya kimataifa, jambo linaloipa nafasi zaidi ya kusonga hatua inayofuata, tofauti na wapinzani wao Gaborone United ambao hawana rekodi za kuvutia.

Sare hii inaipa Yanga matumaini makubwa katika mechi ya marudiano itakayopigwa Septemba 12, 2026, kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, ambapo kikosi hicho kina nafasi ya kusonga hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gaborone United inarejea Dar es Salaam baada ya msimu wa 2025-2026, kucheza na Simba hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutoka sare ya bao 1-1, Septemba 28, 2025, kisha kuondolewa baada ya kuchapwa nyumbani 1-0, Septemba 20, 2025.