Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao lampa mzuka Mayele CAF, aahidi jambo

Muktasari:

  • Mayele amefunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 wa Al Ahli Tripoli dhidi ya KMKM ya Zanzibar, leo Septemba 5, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

BAO la kwanza katika jezi ya Al Ahli Tripoli ya Libya, limempa mzuka mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo, Fiston Kalala Mayele, ambaye amesema kufunga katika mechi yake ya kwanza kumemjengea kujiamini kwenye maisha yake mapya ndani ya klabu hiyo, huku akibainisha kwamba malengo yao msimu huu ni kufika mbali katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mayele amefunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 wa Al Ahli Tripoli dhidi ya KMKM ya Zanzibar, leo Septemba 5, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Mayele amesema amefurahi kuanza safari yake mpya kwa bao, akiamini hatua hiyo itampa nguvu zaidi kama mshambuliaji.

“Nimekuja kwenye klabu mpya, nimefanikiwa kucheza na kufunga kwenye mechi yangu ya kwanza jambo linalonipa kujiamini kama mshambuliaji,” amesema Mayele.

Bao hilo pia lilikuwa la kipekee kwake kwa sababu limekuja katika mchezo wake wa kwanza kurejea Tanzania tangu alipoondoka nchini mwaka 2023.

“Nimefurahi sana kurudi tena hapa. Hii ni mara ya kwanza narejea tangu niondoke Tanzania na nimecheza na kufunga bao. Kwa kweli nimefurahi sana,” amesema.

Mayele, aliyewahi kuitumikia Yanga kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 kabla ya kuondoka na kujiunga na Pyramids ya Misri, amesema kurejea Tanzania na kuanza kwa bao kumempa furaha ya ziada.

Licha ya Al Ahli Tripoli kupata ushindi huo, Mayele amesema mchezo haukuwa mwepesi kutokana na Ligi Kuu ya Libya bado haijaanza, jambo lililowafanya wakose kidogo muunganiko na kasi ya ushindani.

“Kwanza kabisa namshukuru Mungu tumepata ushindi. Mchezo haukuwa mwepesi kwa sababu ligi yetu ya Libya bado haijaanza.

“Tulikuwa na shida kidogo ya kupata muunganiko wa kucheza vizuri, lakini tunashukuru tumefanikiwa kupambana na kupata mabao matatu,” amesema.

Mbali na bao lake, Mayele pia amezungumzia mabadiliko aliyoyaona kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, akisema amekuta uwanja ukiwa katika hali bora zaidi tofauti na alivyocheza mara ya mwisho.

Amesema mara ya mwisho kucheza hapo akiwa na Yanga katika Kombe la Mapinduzi, ubora wa uwanja haukuwa wa kuridhisha, lakini safari hii ameshangazwa na maboresho yaliyofanyika.

“Mara ya mwisho nilipocheza hapa kwenye Kombe la Mapinduzi nikiwa na Yanga, ubora wa uwanja haukuwa mzuri sana.

“Lakini nilipokuja kufanya mazoezi ya mwisho jana na kucheza leo, nilishangaa sana. Uwanja sasa ni mzuri mno na mpira unatembea vizuri,” amesema.

Mshambuliaji huyo amesema, Al Ahli Tripoli ina malengo makubwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na haitaki kuishia katika hatua za mwanzo, bali inataka kusonga mbele na kuwapa furaha mashabiki wake.

“Malengo yetu ni kufika mbali kwenye mashindano haya na kuwapa furaha mashabiki wetu wengi waliopo Libya,” amesema.

Al Ahli Tripoli sasa ina faida ya mabao 3-0 kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya KMKM, ambao utapigwa Septemba 12, 2026 nchini Libya.

Mshindi wa jumla wa michezo hiyo miwili atasonga mbele kwenda hatua ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.