Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuchel: Hatutampata Kane mwingine

TUCHEL Pict

Muktasari:

  • Kane, mwenye miaka 33, alifunga bao lake la 87 kwa England katika ushindi dhidi ya Jamhuri ya Czech Jumanne, na kuongeza rekodi yake ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa England, Thomas Tuchel amesema haitakuwa rahisi kwa timu hiyo kumpata mshambuliaji mwingine wa kiwango cha nahodha wake, Harry Kane ambaye anaendelea kuvunja rekodi na kuweka historia mpya akiwa na kikosi hicho.

Kane, mwenye miaka 33, alifunga bao lake la 87 kwa England katika ushindi dhidi ya Jamhuri ya Czech Jumanne, na kuongeza rekodi yake ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo.

Nyota huyo wa Bayern Munich sasa amebakiza mechi mbili tu kufikisha mechi 125 za kimataifa, rekodi inayoshikiliwa na kipa wa zamani ya Peter Shilton, huku akielekea kuwa mchezaji aliyevaa jezi ya England mara nyingi zaidi.

TUCH 01

Hata hivyo, wakati Kane akiwa kwenye kiwango bora cha maisha yake ya soka, Tuchel amesema England haina mchezaji mwingine anayefanana naye ambaye anaweza kuchukua nafasi yake siku atakapostaafu.

Msimu uliopita, Kane alifunga jumla ya mabao 73 akiwa na klabu na timu ya taifa, jambo lililomuingiza kwenye mjadala wa kuwania tuzo ya Ballon d’Or.

“Jambo la kwanza, hamtampata Harry Kane mwingine,” amesema Tuchel.

TUCH 02

“Yeye ndiye wa kwanza kuwahamasisha wengine. Ana mtazamo huo na amekuwa mshambuliaji anayefanya kazi kwa bidii, juu ya uwezo wake wa kufunga mabao. Ni mchezaji aliyekamilika.

“Tunaangalia chaguo na suluhisho tofauti. Tulimaliza mchezo Jude (Bellingham) akiwa mbele kama namba tisa.

“Tutampata mwingine, lakini hatakuwa Harry wala nakala yake. Tutapata suluhisho wakati utakapofika, lakini huenda si mimi nitakayeliona. Inaweza kuchukua miaka mingine 10.”

Kane ni miongoni mwa washambuliaji bora wa kizazi chake, lakini kupata mbadala wake kumekuwa tatizo la muda mrefu kwa England.

Ollie Watkins na Ivan Toney wamekuwa wakitumika kama washambuliaji wa akiba katika michuano miwili mikubwa iliyopita, lakini wawili hao sasa wako kwenye miaka ya 30 na hawakuitwa kwenye kikosi cha sasa cha Ligi ya Mataifa.

Dominic Calvert-Lewin yupo kwenye kikosi, ingawa pia anakaribia kutimiza miaka 30, huku Liam Delap akiwa ndiye mshambuliaji pekee wa kati wa England aliye chini ya miaka 27 aliyewahi kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

TUCH 03

Kutokana na hali hiyo, Tuchel ameongeza chaguo lake la ushambuliaji katika mchezo dhidi ya Czech kwa kumtumia Bellingham, nyota wa Real Madrid, katika nafasi ya juu zaidi kuliko alivyozoeleka baada ya kumtoa Kane.

“Napenda kumtumia kama namba tisa. Hapo anaweza kusaidia pande zote mbili na kuongeza idadi ya wachezaji pembeni bila kuvuruga sana uwiano wa timu,” ameongeza Tuchel.

“Tuligundua nafasi mpya kwake katika mchezo uliopita, akiwa kama namba 10 wa kati, hivyo anaweza kwenda pande zote mbili. Mfumo unakuwa zaidi 4-2-3-1 badala ya 4-3-3, ili kuwaweka Harry na Jude karibu zaidi na kuwapa nafasi ya kuongeza idadi ya wachezaji katika pande zote mbili.

“Tunaendelea kufanyia kazi hilo. Jude ni mfungaji wa asili na ana njaa ya kuona jina lake kwenye ubao wa mabao. Anataka kuwa eneo hilo na kufanya tukio la kuamua mchezo, hivyo si tofauti kubwa kwake kucheza kama namba tisa au 10.”