Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe England viponde tu kwa vigogo

ENGLAND Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo huo wa kusisimua, Three Lions ilishindwa kuhimili ubora wa Hispania, ikipoteza kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Wembley, huku makosa ya safu ya ulinzi yakiigharimu timu hiyo.

LONDON, ENGLAND: TIMU ya taifa ya England 'Three Lions' imepokea kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Hispania 'La Roja', hali inayoibua tena maswali kuhusu uwezo wake wa kushinda dhidi ya timu kubwa duniani.

Katika mchezo huo wa kusisimua, Three Lions ilishindwa kuhimili ubora wa Hispania, ikipoteza kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Wembley, huku makosa ya safu ya ulinzi yakiigharimu timu hiyo.

Ushindi huo wa Hispania ulipatikana kupitia bao la Mikel Oyarzabal, aliyeingia akitokea benchi, ambaye ana historia ya kuumiza England baada ya kufunga bao la ushindi katika fainali ya Euro 2024.

Baada ya England kuonesha soka lenye kasi na msisimko lililowafanya mashabiki wake kukasirika na kushangilia kwa nyakati tofauti, inaonekana safari ya timu hiyo kuelekea kutwaa taji kubwa la kimataifa bado ni ndefu.

Lamine Yamal aliifungia Hispania bao la kwanza dakika ya pili, likiwa bao la tatu la mapema zaidi kuwahi kufungwa England katika Uwanja wa Wembley.

England ilipaswa kuwa nyuma kwa mabao 4-0, au hata 5-0, kabla ya Anthony Gordon na Harry Kane kufunga mabao yaliyoiwezesha timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1, matokeo yaliyoonekana kutotarajiwa kutokana na mwenendo wa mchezo.

ENG 03

Kane baadaye alikosa penalti baada ya kuteleza wakati akipiga mpira, hali iliyokumbusha tukio kama hilo katika robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Ufaransa.

Mbadala Alex Baena aliisawazishia Hispania kabla ya Oyarzabal kutumia udhaifu mwingine wa safu ya ulinzi ya England na kufunga bao la ushindi.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Thomas Tuchel kutumia kikosi chenye wastani mdogo zaidi wa umri, miaka 25 na siku sita, lakini umri hauwezi kuwa kisingizio cha makosa ya msingi yaliyoigharimu timu hiyo.

Kwa England, changamoto sasa ni namna ya kuunganisha kasi na makali ya ushambuliaji na uimara wa ulinzi ili iweze kushindana na timu bora duniani katika hatua za mwisho za mashindano makubwa.

Rekodi ya England dhidi ya timu zinazoshika nafasi 10 za juu katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) inaibua maswali kuhusu uwezo wake wa kukabiliana na wapinzani wa kiwango cha juu.

Katika mechi 15 zilizopita dhidi ya timu zilizokuwa ndani ya 10 bora duniani, England imeshinda sita pekee.

Miongoni mwa ushindi huo, mitatu ilipatikana katika mashindano makubwa, nusu fainali za Euro 2020 na 2024 dhidi ya Denmark na Uholanzi, pamoja na mechi ya kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Ufaransa katika Kombe la Dunia la mwaka huu.

Ushindi dhidi ya Ufaransa ulimpa kocha Tuchel ushindi wake wa kwanza kama kocha wa England dhidi ya timu iliyokuwa ndani ya 10 bora duniani.

Ushindi wake wa kwanza dhidi ya timu iliyokuwa ndani ya 20 bora ulikuwa katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya mashindano hayo dhidi ya Croatia.

Hali hiyo inaibua swali: Je, England ina tatizo inapokutana na timu zinazoshika nafasi za juu duniani?


ENG 01

TAKWIMU ZINASEMAJE?

Kushinda sita katika mechi 15 zilizopita dhidi ya timu zilizokuwa ndani ya 10 bora duniani si rekodi inayoweza kuiridhisha England, ambayo ina dhamira ya kutwaa mataji makubwa.

Kushinda mbili kati ya hiyo uliiwezesha Three Lions kufuzu fainali za Euro 2020 na 2024. Mwingine ulipatikana katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu ya Kombe la Dunia, ambayo hakuna timu inayotaka kucheza.

Ushindi mwingine ilipatikana katika mechi za kufuzu Euro dhidi ya Italia, wakati timu hiyo ikiwa tayari imeanza kushuka kiwango, huku mmoja ukipatikana dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa Ligi ya Mataifa miaka sita iliyopita.

Kwa kifupi, England imeendelea kupata wakati mgumu inapokutana na timu zenye ubora wa juu, hasa katika Kombe la Dunia na mashindano Ulaya.

Tangu mwaka 1998, England imeondolewa mara saba katika hatua za mtoano za Kombe la Dunia, kila mara baada ya kukutana na timu iliyokuwa ndani ya 10 bora ya viwango vya Fifa.

Katika mechi 10 zilizopita za Kombe la Dunia dhidi ya timu hizo, ushindi pekee wa England ulikuwa dhidi ya Argentina katika hatua ya makundi mwaka 2002.

Pia, inapokutana na mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, England imefungwa katika matukio yote manne yaliyotajwa:

1954: Uruguay 4-2 England.

1962: Brazil 3-1 England.

2022: England 1-2 Ufaransa.

2026: England 1-2 Argentina.

Katika michuano ya Euro, England imefanya vizuri zaidi, ikizishinda Denmark na Uholanzi katika nusu fainali za mashindano ya mwaka 2020 na 2024 na kufuzu fainali zote mbili.

Hata hivyo, ilishindwa katika hatua ya mwisho, ikifungwa na Italia mwaka 2020 na Hispania mwaka 2024.

Takwimu za umiliki wa mpira katika mechi 15 zilizopita dhidi ya timu 10 bora zinaonesha kuwa England ilikuwa na umiliki mdogo zaidi katika nusu fainali dhidi ya Argentina, kwa asilimia 35.8, katika Kombe la Dunia la mwaka huu.

Katika fainali za Euro, ilikuwa na umiliki wa asilimia 34.9 dhidi ya Hispania mwaka 2024 na asilimia 42.1 dhidi ya Italia mwaka 2020.

‘Tunachotakiwa ni kucheza kwa utambulisho wetu’

Mfungaji bora wa muda wote wa England, Harry Kane, mwenye mabao 86, aliulizwa ni kitu gani kinakosekana ili timu hiyo iweze kuvuka hatua ya mwisho na kutwaa mataji makubwa.

"Nadhani katika nyakati kubwa zaidi, tunachotakiwa ni kuendelea kuwa sisi wenyewe," alisema Kane.

Hali ingeweza kuwa tofauti kama Kane angefunga penalti yake. Hakufunga, na mambo hayakwenda hivyo.

Kane alisema: “Siku nyingine tungeweza kushinda.” Lakini siku hiyo haikuwa nyingine, na England haikushinda.

Kane, ambaye amefunga mabao 152 katika mechi 154 akiwa na Bayern Munich na kutwaa mataji mawili ya Bundesliga, alisema uzoefu wake katika klabu hiyo umemfundisha kutokuwa na hofu dhidi ya wapinzani.

"Nimepitia hali hiyo Bayern Munich, kwa mfano. Hatuogopi timu yoyote," alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

"Unaenda uwanjani na kucheza kwa utambulisho wako. Kama timu nyingine itakushinda, unapeana mikono baada ya mchezo na kuikubali ushindi wake.

"Unakuwa na utambulisho unaouendeleza wakati wote.

"Nadhani hilo ndilo tunalopaswa kuliangalia England kwa sasa.

"Tuko karibu sana. Tumekuwa karibu mara nyingi, lakini mwishowe hatupaswi kumwogopa mtu yeyote.

"Tunachotakiwa ni kuwa sisi wenyewe katika nyakati kubwa na, kwa matumaini, tutafika mwisho na kutwaa taji."


ENG 02

MASWALI YALE YALE YANAENDELEA KUREJEA

England imekuwa ikikaribia mafanikio ya kutwaa mataji makubwa kwa miaka kadhaa, lakini swali lilelile linaendelea kubaki: Je, inaweza kutawala umiliki wa mpira na kuzishinda timu bora duniani?

Katika Euro 2020, ushindi wa England dhidi ya Ujerumani katika hatua ya 16 bora ulikuwa muhimu sana kwa sababu iliifunga moja ya mataifa yenye historia kubwa katika soka. Hata hivyo, Ujerumani hiyo ilikuwa katika kipindi cha mpito na wakati huo ilikuwa nje ya 10 bora duniani.

England inaonekana kushindwa kugeuza ubora wa wachezaji wake wa kiwango cha dunia kuwa umiliki wa mpira na udhibiti wa mchezo.

Tuchel amesema huenda akalazimika kukubali mfumo wa soka lao la kuwa la matukio yasiyotabirika, huku Anthony Gordon akiongeza kuwa England inapaswa kutegemea mtindo wake wa jadi wa kucheza soka la moja kwa moja.

Huenda huo ukawa mwelekeo unaohitajika ili hatimaye kumaliza kusubiri kwa muda mrefu kwa England kutwaa taji kubwa la kimataifa.