Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuchel atangaza Kikosi cha England, atema mastaa

ENGLAND Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa majina makubwa yaliyoenguliwa ni pamoja na Cole Palmer, Phil Foden, Trent Alexander-Arnold na Harry Maguire hatua ambayo imeibua mjadala mkubwa ndani na nje ya Uingereza.

KOCHA mkuu wa England, Thomas Tuchel, ameshtua wadau wengi wa soka baada ya kutangaza kikosi chake cha wachezaji 26 kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026, akiwabwaga baadhi ya majina makubwa.

Miongoni mwa majina makubwa yaliyoenguliwa ni pamoja na Cole Palmer, Phil Foden, Trent Alexander-Arnold na Harry Maguire hatua ambayo imeibua mjadala mkubwa ndani na nje ya Uingereza.

Kwa upande mwingine, mshambuliaji Ivan Toney amerejea katika kikosi hicho licha ya kucheza dakika chache chini ya Tuchel lakini akiwa na rekodi nzuri ya mabao 32 katika mechi 32 alizocheza kwenye ligi ya  Saudi Arabia akiwa na Al-Ahli.

ENGL 02

Tuchel pia amewajumuisha wachezaji vijana na wenye nguvu mpya kama Kobbie Mainoo, Eberechi Eze, Noni Madueke, Djed Spence na Jarell Quansah huku akiendelea kumtegemea nahodha Harry Kane kuongoza safu ya ushambuliaji.

Katika kikosi hicho, makipa ni Jordan Pickford (Everton), Dean Henderson (Crystal Palace) na James Trafford (Manchester City).

Mabeki; Reece James (Chelsea), Ezri Konsa (Aston Villa), Jarell Quansah (Bayer Leverkusen), John Stones (Manchester City), Marc Guehi (Manchester City), Dan Burn (Newcastle United), Nico O’Reilly (Manchester City), Djed Spence (Tottenham Hotspur) na Tino Livramento (Newcastle United).

Viungo wa kati ni Declan Rice (Arsenal), Elliot Anderson (Nottingham Forest), Kobbie Mainoo (Manchester United), Jordan Henderson (Brentford), Morgan Rogers (Aston Villa), Jude Bellingham (Real Madrid) na Eberechi Eze (Arsenal).

ENGL 01

Washambuliaji; Harry Kane (Bayern Munich), Ivan Toney (Al-Ahli), Ollie Watkins (Aston Villa), Bukayo Saka (Arsenal), Marcus Rashford (Barcelona), Anthony Gordon (Newcastle United) na Noni Madueke (Arsenal).

England itaanza maandalizi ya Kombe la Dunia kwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya New Zealand, Juni 6 na Costa Rica, Juni 10 kabla ya kutua Amerika Kaskazini na kutupa karata yao ya kwanza dhidi ya Croatia, Juni 17.