Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata la West Ham, Arsenal laibua mjadala Kombe la Dunia 2026

SAKATA Pict

Muktasari:

  • ‘The Hammers’ walilalamikia vitendo vya kushikana na kuzuiana vilivyofanywa na wachezaji wa Arsenal wakati kona ya Jarrod Bowen ikipigwa, ingawa hakuna mchezaji aliyefanya hivyo aliyeathiri mchezo moja kwa moja.

LONDON, ENGLAND: WACHEZAJI wa timu ya taifa ya England wamepewa onyo na kujiandaa na sheria kali dhidi ya mchezo wa kushikana na mivutano ndani ya eneo la hatari wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2026.

Hatua hii imekuja baada ya klabu ya West Ham kudai maelezo kutoka kwa wakuu wa bodi ya waamuzi ya PGMO. Hii ni kufuatia goli la kusawazisha la Callum Wilson dakika za lala salama dhidi ya Arsenal kukataliwa. Mwamuzi alidai mchezaji Pablo, alimfanyia madhambi kipa wa Gunners, David Raya.

‘The Hammers’ walilalamikia vitendo vya kushikana na kuzuiana vilivyofanywa na wachezaji wa Arsenal wakati kona ya Jarrod Bowen ikipigwa, ingawa hakuna mchezaji aliyefanya hivyo aliyeathiri mchezo moja kwa moja.

SAKA 01

Ingawa uamuzi wa mwamuzi Chris Kavanagh uliungwa mkono na wachambuzi kama Wayne Rooney, mkuu wa jopo la wataalamu wa FIFA amedokeza kuwa viongozi wa soka duniani wanataka kuona waamuzi wakichukua hatua kali msimu huu.

Mabadiliko haya yanaweza kuathiri mipango ya England. Kocha Thomas Tuchel tayari ameeleza mkakati wake wa kutumia krosi hatari za mipira ya kutenga kutoka kwa nyota wa Arsenal, Declan Rice na Bukayo Saka.

SAKA 02

Pascal Zuberbuhler, kipa wa zamani wa Uswisi na mkuu wa Kikundi cha Utafiti wa Kiufundi (TSG) chenye wajumbe 11 wakiwemo nyota wa zamani wa Premier League kama Jurgen Klinsmann, Gilberto Silva, Pablo Zabaleta, Paulo Wanchope, na Jon Dahl Tomasson amesema: "Tumeona hili, hasa katika Ligi Kuu ya England tukiitazama Arsenal. Huu ni mtindo mpya, ndio, lakini nina uhakika kwa Kombe la Dunia 2026 tutakuwa na waamuzi bora zaidi na watasiamia hali hii kikamilifu. Tunajua ni vigumu kwa waamuzi kwa sababu kuna makosa madogo madogo dhidi ya kipa, na maafisa wanapaswa kutazama kati ya watu wengi wanaowazunguka. Si rahisi kuona, lakini ni lazima tuwe waangalifu tangu mwanzo."

Katika malalamiko yao, West Ham walitaka maelezo ya kwa nini mwamuzi wa VAR, Darren England, aliingilia kati na kumshauri Kavanagh kubadilisha uamuzi wake wa kwanza wa kukubali goli hilo.

SAKA 01 (1)

Wakati huo huo, imebainika kuwa watengeneza sheria wa Bodi ya Soka ya Kimataifa (IFAB) wanaweza kuangalia upya njia za kupambana na ushikaji wa kupitiliza, lakini hiyo itakuwa baada ya Kombe la Dunia 2026.

Hii ina maana kwamba jukumu hilo litabaki kwa waamuzi waliochaguliwa na FIFA wakiwemo wa Ligi Kuu ya England, Michael Oliver na Anthony Taylor kusimamia maagizo yote kutoka kwenye chombo hicho cha soka duniani.