Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tottenham yamnasa Savinho kutoka Man City

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Savinho mwenye miaka 22, sasa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa muda mrefu na Tottenham.

LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM Spurs imefikia makubaliano na Manchester City ya kumsajili winga wa Brazil, Savinho, kwa ada ya pauni 75milioni, huku kukiwa na uwezekano wa kuongeza pauni10 milioni kupitia bonasi mbalimbali.

Savinho mwenye miaka 22, sasa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa muda mrefu na Tottenham.

Uhamisho wa winga huyo kwenda kaskazini mwa London umekuwa ukipangwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, baada ya Tottenham kushindwa kumnasa msimu uliopita wa usajili.

Savinho aliamua kubaki Manchester City, lakini alikosa nafasi ya kutosha chini ya kocha Pep Guardiola msimu uliopita, akianza michezo saba pekee ya Ligi Kuu England.

Baada ya kutumia jumla ya pauni185 milioni, kuwasajili viungo Mateus Fernandes kutoka West Ham na Sandro Tonali kutoka Newcastle, kocha wa Tottenham, Roberto De Zerbi sasa amegeukia kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Hata hivyo, Tottenham huenda bado haijamaliza matumizi yake katika dirisha hili la usajili.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na BBC Sport, mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Omar Marmoush yanaendelea vizuri.

Mshambuliaji huyo wa Misri, ambaye Manchester City ilimsajili kutoka Eintracht Frankfurt mwaka 2025 kwa pauni59 milioni, alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza msimu uliopita.

Tottenham pia bado inavutiwa na mshambuliaji wa Liverpool, Cody Gakpo, ingawa haijafahamika kama klabu hiyo itaweza kumudu gharama za kumsajili nyota huyo wa Uholanzi sambamba na dili za Marmoush na Savinho.

Ikiwa itakamilisha usajili huo, Tottenham itakuwa imeendelea na mpango wake wa kujenga kikosi kipya chini ya De Zerbi, huku ikitumia nguvu kubwa katika soko la usajili.


AXEL DISASI

Crystal Palace imefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo beki wa Chelsea, Axel Disasi, kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya uhamisho, Fabrizio Romano. Disasi alitumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo West Ham baada ya kutokuwa kwenye mipango ya Chelsea, na sasa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo asubuhi kabla ya kukamilisha uhamisho huo.


LIAM DELAP

Leeds United imejiunga kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Liam Delap, msimu huu wa joto, kwa mujibu wa taarifa za usajili. Leeds inakutana na ushindani kutoka Nottingham Forest na Everton, ambazo pia zinatajwa kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye amepoteza nafasi kwenye mipango ya Chelsea chini ya kocha Xabi Alonso na hata kuvuliwa jezi namba 9 aliyokuwa akiivaa Stamford Bridge.


YANKUBA MINTEH

Mchambuzi anayefuatilia kwa karibu Brighton wa The Athletic, Andy Naylor, anaamini winga Yankuba Minteh ataishia Liverpool huku kiungo Carlos Baleba akihamia Manchester United, akisema ofa zilizowasilishwa na klabu hizo “haziko mbali sana kufikia makubaliano.” Naylor ameongeza kuwa Brighton inaweza kupata faida kubwa tena kutokana na uuzaji wa wachezaji hao, baada ya kuwapa nafasi ya kucheza na kuwaendeleza kabla ya kuhamia klabu kubwa, akisisitiza kuwa huo ndio mfumo wa biashara wa klabu hiyo.


DARWIN NUNEZ

Mshambuliaji Darwin Nunez ameendelea na safari yake ya kuichezea klabu nyingine nchini Saudi Arabia, baada ya kuondoka Al-Hilal na kujiunga kwa mkopo na Al-Diriyah, bila kuwepo kipengele cha klabu hiyo kuwa na haki ya kumsajili moja kwa moja baada ya mkataba wa mkopo kumalizika. Hatua hiyo imekuja baada ya Nunez, ambaye alihangaika kufanya vizuri katika Ligi Kuu England.


ADAM WHARTON

Manchester City imepewa ushauri wa kubadili uamuzi wake katika siku za mwisho za dirisha la usajili na kumsajili kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton, baada ya mchambuzi Ally McCoist kuvutiwa na uwezo wa nyota huyo. McCoist alisema: “Ninampenda sana Wharton. Nafikiri anafanana zaidi na Rodri kuliko Fernandez. Sidhani kama watapata mbadala wa moja kwa moja baada ya Rodri kuondoka, kwa sababu yeye ndiye bora zaidi katika kile anachokifanya.


BARIS ALPER YILMAZ

Tottenham na Everton zimeanza kuwania saini ya mshambuliaji wa Galatasaray, Baris Alper Yilmaz, ambaye anatajwa kuwa na thamani ya karibu pauni35 milioni, huku klabu hizo zikiripotiwa kutoa ofa za awali kwa njia ya mazungumzo. Yilmaz, 26, amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Galatasaray.


ENDRICK

Mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil, Endrick, hana mpango wa kuondoka Hispania licha ya Liverpool kuripotiwa kuvutiwa na huduma zake, huku nyota huyo akitaka kubaki Real Madrid na kupambana kuwania nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Jose Mourinho. Endrick anaamini anaweza kupata nafasi ya kuthibitisha uwezo wake akiwa Madrid, hivyo Liverpool italazimika kuendelea kusubiri ikiwa bado inataka kuongeza mshambuliaji mwingine katika kikosi chake.


GEORGE HIRST

Stoke City imekamilisha usajili wa mshambuliaji George Hirst kutoka Ipswich Town kwa ada inayokadiriwa kuwa karibu pauni milioni 10, baada ya mchezaji huyo kuisaidia Ipswich kupanda Ligi Kuu England. Hirst sasa anarejea Championship baada ya msimu mmoja akiwa katika Ligi Kuu.


TROY PARROTT

Mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland, Troy Parrott, amekamilisha uhamisho wake kutoka AZ Alkmaar ya Uholanzi kwenda Real Betis kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni milioni 15, akitia saini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya Hispania. Parrott amesema miaka miwili aliyotumia AZ Alkmaar ilikuwa bora zaidi katika maisha yake hadi sasa, akifichua kuwa alipowasili klabuni hapo alikuwa amepoteza kwa kiasi fulani hamu ya kucheza soka.