Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tottenham, Arsenal vita kali kwenye mkwanja

LONDON Pict

Muktasari:

  • Lakini, Manchester City itakuwa timu itakayopata mkwanja mkubwa zaidi kwa Ligi Kuu England, ambapo miamba hiyo ya Etihad itaweka kibindoni Pauni 53 milioni kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya hata haijaanza kucheza michuano hiyo.

LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM Hotspur itavuna pesa nyingi kuliko Arsenal kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao baada ya kufanikiwa kunyakua ubingwa wa Europa League.

Lakini, Manchester City itakuwa timu itakayopata mkwanja mkubwa zaidi kwa Ligi Kuu England, ambapo miamba hiyo ya Etihad itaweka kibindoni Pauni 53 milioni kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya hata haijaanza kucheza michuano hiyo.

Na mashabiki wa Newcastle United watawaza kuhusu mgawo wa Pauni 100 milioni utakuwaje na kinachoelezwa ni kwamba miamba hiyo itatanguliziwa Pauni 25 milioni baada ya kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Licha ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England nyuma ya Liverpool na Arsenal, Man City ndiyo timu itakayopata mgawo mkubwa kati ya timu sita za England zilizokamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Lakini, kuna habari njema kwa mashabiki wa Spurs, ambapo kikosi chao baada ya kushinda taji la Europa League kitapata mgawo mkubwa wa pesa kuzidi mahasimu wao wa London Kaskazini, Arsenal.

Kwa mujibu wa Uefa, timu zote sita zilizofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa upande wa England, zitaanza kwa bonasi ya Pauni 15.72 milioni. Lakini, kwa kutazama mgawo wote wa Pauni 717 milioni unaotokana na viwango vya timu kwenye michuano ya Ulaya kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano na 10 na pesa ya mikataba ya televisheni katika kila nchi, hilo ndilo lililofanya kuwapo na tofauti ya karibu Pauni 30 milioni baina ya Man City na Newcastle. TNT Sport inalipa Pauni 305 milioni kwa msimu kwa ajili ya kuonyesha mechi mubashara, lakini ni 17 tu kati ya 189 huku Amazon Prime ikionyesha mechi nyingine.

Thamani ya madili hayo yanazidi Pauni 411 milioni kwa mwaka huku kukiwa na Canal+ ambayo ina haki ya matangazo ya michuano hiyo kwa nchi ya Ufaransa. Man City imeshika namba mbili kwa kipindi cha miaka mitano licha ya msimu huu kutolewa mapema, kwamba mechi zake zimeonyeshwa sana na hivyo imekamatia Pauni 28.23 milioni. Kwa viwango vya miaka 10 imeshika nafasi ya tatu na hivyo kuvuna Pauni 9.18 milioni nyingine na kufanya kuwa na mgawo wa jumla wa Pauni 53.13 milioni.

Liverpool inafuatia kwa timu za Ligi Kuu England, ikivuna Pauni 51.64 milioni kwenye michuano hiyo ya Ulaya, wakati Chelsea pia ipo juu ya Arsenal baada ya kuvuna Pauni 48.82 milioni.

Arsenal imevuna Pauniu 47.86 milioni. Spurs itavuna Pauni 44.62 milioni, lakini kuna uhakika wa kulipwa pia Pauni 3.38 milioni kwa kupata tiketi ya kucheza Uefa Super Cup, jambo litakaloifanya Spurs kuwa na mgawo wa jumla wa Pauni 48 milioni na kuizidi Arsenal.