Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu kibao Ulaya zaanza kumgombea Gabriel Jesus

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mbali ya Spurs na Newcastle saini ya staa huyu pia inahitajika na vigogo mbalimbali kama Barcelona, AC Milan na Inter Milan wote katika dirisha hili.

NEWCASTLE na Tottenham ziko katika vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 28, katika dirisha hili.

Mbali ya Spurs na Newcastle saini ya staa huyu pia inahitajika na vigogo mbalimbali kama Barcelona, AC Milan na Inter Milan wote katika dirisha hili.

Vilevile mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya taarifa zilifichua kuwa Flamengo na Palmeiras za Brazil pia inahitaji saini yake.

Changamoto kubwa inayoonekana kukwamisha dili la kutua Flamengo au Palmeiras kwa sasa inadaiwa kuwa ni hali yake ya majeraha kwani bado hayupo fiti na timu hizo kwa muda huu ndio zina uhitaji kwa kuwa ligi inaendelea, hivyo zinaweza kurudi Januari mwakani.

Vyanzo vya karibu na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazili vimeiambia tovuti ya CaughtOffside kuwa klabu kama AC Milan, Barcelona na Newcastle United vinamfuatilia kwa karibu.

Kwa upande wa Barcelona, inataka kumsajili kwa sababu inajiandaa na maisha baada ya staa wake Roberto  Lewandowski ambaye haonekani kuwa atakuwa katika timu hiyo ukiisha msimu ujao.

Ingawa hakuna hata moja ya klabu iliyowasilisha ofa rasmi hadi sasa, Jesus mwenyewe ameonyesha kutamani zaidi kuondoka na kupata changamoto mpya sehemu nyingine. Amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha.


Jack Grealish

AC Milan inafanya mazungumzo na wawakilishi wa winga wa Manchester City na England, Jack Grealish mwenye umri wa miaka miaka 29,  ambaye pia anawindwa sana na Napoli inayohitaji kumsajili katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha safu yao ya ushambuliaji. Grealish ni miongoni mwa wachezaji waliopewa barua za kutafuta timu na Man City kwani hayupo katika mipango ya kocha Pep Guardiola kuelekea msimu ujao.

Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Douglas Luiz

WEST Ham inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuipiku Everton katika vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Juventus, Douglas Luiz katika dirisha hili.

Staa huyu wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, mara kadhaa pia amekuwa akihusishwa na Manchester United. Mkataba wake na Juventus unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Awali, Aston Villa ilidaiwa kutaka kumrudisha kikosini lakini iliamua kujiondoa.


Kiernan Dewsbury-Hall

FULHAM imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsainisha kiungo wa Chelsea, Kiernan Dewsbury-Hall, katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango chake alichoonyesha katika dirisha lililopita msimu uliopita. Hull ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na amevutiwa sana na dili la Fulham kwa sababu alikuwa akitaka kuondoka.


Aleksandar Mitrovic

MANCHESTER United, Newcastle, na Tottenham zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Al-Hilal ya Saudi Arabia, Aleksandar Mitrovic, mwenye umri wa miaka 30. Staa huyu wa kimataifa wa Serbia anataka kuondoka Al-Hilal na kurudi England kutokana na ofa nono ambazo amepokea kutoka kwa vigogo wa England.

Mabosi wa Al-Hilal wapo tayari kumwachia staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwakani. Msimu uliopita alifunga mabao 28, katika mechi 36 za michuano yote.


Roberto Piccol

BENFICA inaripotiwa kuwasilisha ofa rasmi kwenda  Cagliari kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo na Italia, Roberto Piccoli mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha hili. Mabosi wa Cagliari wapo tayari kumuuza staa huyu na wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 26 milioni kama ada yake ya uhamisho. Mkataba wa Piccoli unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, West Ham ndio inaonekana kuwa na nafasi ya kumpata.


Seth Ridgeon

KIUNGO wa Fulham, Seth Ridgeon, amewaambia vigogo wa timu hiyo kuwa anataka kuondoka katika dirisha hili ambapo Manchester United, Liverpool na Chelsea zimeonyesha nia ya kumsajili. Seth ambaye anaichezea timu ya taifa ya England kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, amekuwa akifuatiliwa na maskauti wa timu nyingi tangu msimu uliopita.


Beto

MABOSI wa Atalanta wanataka kumsajili mshambuliaji wa Everton na timu ya taifa ya Guinea-Bissau, Beto, mwenye umri wa miaka 27, katika dirisha hili ili akawe mbadala wa Ademola Lookman ambaye kuna uwezekano mkubwa ikamuuza katika dirisha hili kwa sababu anawindwa na vigogo wengi barani Ulaya. msimu uliopita,alifunga mabao 12.