Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

The Last ride: Nini kinaendelea Migahawa ya Kalitos way group?

REDAL Pict

ILIANZA kama chombo cha usafiri, ikapitia mabadiliko mbalimbali ya kiteknolojia, ikawa suluhisho la changamoto za usafiri nchini Cuba na baadaye ikapata matumizi ambayo huenda wengi wasingeyafikiria nchini Tanzania. 

Hiyo ndiyo safari ya baiskeli iliyogeuzwa kuwa kivutio cha kuwapeleka wageni maliwatoni ambao walikuwa Kukukuku. Sasa, baada ya kuwa sehemu ya burudani hiyo, inatarajiwa kuagwa mwishoni mwa wiki hii.

Fikiria umetembelea eneo la chakula na burudani, lakini unapohitaji kwenda kujisitiri unaelekezwa kupanda baiskeli badala ya kutembea kwa miguu. 

Kwa wengi, jambo hilo linaweza kuonekana la kushangaza, lakini kwa waliowahi kutembelea Kukukuku, lilikuwa sehemu ya uzoefu walioupata katika eneo hilo.

Ubunifu huo ulifanywa na Carlos ‘Kalito Samaki’, ambaye aliona uwezekano wa kukipa chombo hicho matumizi tofauti na yale yaliyozoeleka. Badala ya kuishia kwenye safari za kawaida, baiskeli ikawa sehemu ya huduma iliyowapa wageni uzoefu wa kipekee.

REDA 01

Lakini ili kuelewa namna chombo hicho kilivyofika kwenye matumizi hayo, inafaa kurejea historia yake ambayo inaanzia karne ya 19.

Mwaka 1817, mvumbuzi Mjerumani Karl von Drais alitengeneza kifaa cha usafiri chenye magurudumu mawili kilichojulikana kama running machine. Hakikuwa na pedeli, hivyo mtumiaji alilazimika kujisukuma kwa miguu ili kusonga mbele.

Baadaye, ubunifu wa baiskeli uliendelea kukua, ukafikia hatua ya kuwekwa pedeli na kuboreshwa kwa mifumo ya magurudumu. Hata hivyo, baadhi ya matoleo ya awali yalikuwa na magurudumu ya chuma na yalijulikana kwa safari zake zenye misukosuko, kiasi cha kupewa jina la boneshaker.

Miaka mingi baadaye, baiskeli ilionyesha tena umuhimu wake katika mazingira tofauti kabisa, safari hii nchini Cuba.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Cuba ilikumbwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi uliotokana kwa kiasi kikubwa na kuporomoka kwa uhusiano wake wa kibiashara na nchi za Umoja wa Kisovieti. 

REDA 02


Upatikanaji wa mafuta ulipungua, huduma za usafiri zikaathirika na wananchi wakalazimika kutafuta njia nyingine za kusafiri.

Kipindi hicho kilichojulikana kama Special Period kilishuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya baiskeli. Nchi hiyo iliingiza baiskeli kwa wingi kutoka China, zikiwemo aina maarufu ya Flying Pigeon ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya usafiri.

Kwa wananchi wa Cuba, baiskeli haikuwa tena chaguo la ziada, bali sehemu muhimu ya maisha ya kila siku. Uhaba wa vipuri nao uliwafanya watumiaji kuwa wabunifu katika kutengeneza na kurekebisha baiskeli zao ili ziendelee kufanya kazi.

Ni katika mazingira hayo ya historia na matumizi ya baiskeli ndipo safari ya Carlos ‘Kalito Samaki’ ilipopata msukumo wake. Baada ya kutembelea Cuba na kuona nafasi ya chombo hicho katika maisha ya watu, alirejea Tanzania akiwa na mtazamo tofauti kuhusu matumizi yake.

Katika Kukukuku, wazo hilo likapata sura nyingine. Baiskeli ikawa njia ya kuwafikisha wageni kwenye eneo la maliwato, jambo lililogeuza shughuli ya kawaida ya kujisitiri kuwa sehemu ya burudani.

Huo ndio ulikuwa utofauti wa ubunifu huo. Wageni hawakukutana na huduma ya kawaida pekee, bali walipata jambo ambalo lingeweza kuwashangaza na kuwa kumbukumbu ya ziara yao.

Sasa, baada ya kuwa sehemu ya simulizi ya Kukukuku, baiskeli hiyo inakaribia kuhitimisha safari yake. Mwishoni mwa wiki hii inatarajiwa kuagwa kupitia tukio la Fireway Weekend, ambalo litakuwa na safari yake ya mwisho.

Kuondoka kwake kunafungua ukurasa mwingine na kuibua swali kuhusu  ubunifu mwingine unaofuata katika eneo hilo.