Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Qatar yapata ushindi dakika za jioni

QATAR Pict

WENYEJI wa Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 17, Qatar, wamepata ushindi kwenye mechi yao ya kwanza ya kundi A baada ya kuitandika Panama mabao 2-0 dakika za mwishoni.

Qatar ilivunja ukuta wa Panama dakika ya 90+1 kupitia Taha Nassir aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, kabla ya Abdoulaye Ndiaye kuongeza bao la pili dakika ya 90+5 na kuhitimisha ushindi huo wa wenyeji.

Katika mechi nyingine, Msumbiji ilifanya vizuri kwenye mchezo wake wa kwanza katika fainali za Kombe la Dunia U-17 kwa kuichapa Denmark mabao 4-0. Khenzane aliifungia timu hiyo bao la kwanza dakika ya nne, kabla ya Alirio Cuna kuongeza mawili dakika za 32 na 44, huku Mubai akihitimisha idadi hiyo  dakika ya 90+1.

Ufaransa nayo ilianza kwa ushindi baada ya kuifunga Haiti mabao 3-1 katika Kundi D. Loan Merrifield alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kufunga mabao mawili dakika za nne na 41, huku Noha Tiehi akiweka la tatu dakika ya 47. Haiti ilipata bao moja kupitia Macenat Prophete dakika ya 88.

Uruguay ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Saudi Arabia katika mchezo mwingine wa Kundi D, licha ya kulazimika kusawazisha mara mbili. Faris Bushaqraa aliifungia Saudi Arabia mabao mawili kwa penalti dakika ya 38 na 58, huku Pablo Barreiro akisawazisha dakika ya 44. Bao la kujifunga la Jawad Alhashemalsayed dakika ya 69 liliisawazishia Uruguay, kabla ya Facundo Rodriguez kufunga bao la ushindi dakika ya 86.

Katika michezo mingine ya leo, Australia iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina katika mchezo wa Kundi C. Korea Kusini nayo iliifunga Uganda mabao 3-0, kupitia Kim Jiho dakika ya nane, bao la kujifunga la Mujad Mbalire dakika ya 50 na Kim Jiwoo dakika ya 84. Ecuador iliichapa New Caledonia bao 1-0, lililofungwa na Jhon Guerrero dakika ya 45+1.