Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag: Man United inashuka daraja

TEN HAG Pict

Muktasari:

  • Kichapo hicho kimeifanya United kufikisha mechi tisa mfululizo bila ushindi, huku ikiendelea kujikuta katika mazingira magumu kwenye msimamo wa ligi na kuanza kuangalia kwa karibu hatari ya kushuka daraja.

MANCHESTER, ENGLAND: ALIYEKUWA kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, ameibua hofu kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuonya kuwa timu hiyo inaweza kushuka daraja endapo itaendelea na mwenendo wake mbaya wa matokeo.

Onyo la Ten Hag limekuja kufuatia Manchester United kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea katika mchezo uliochezwa Jumamosi iliyopita, matokeo yaliyoongeza presha kwa kocha wa sasa Michael Carrick.

Kichapo hicho kimeifanya United kufikisha mechi tisa mfululizo bila ushindi, huku ikiendelea kujikuta katika mazingira magumu kwenye msimamo wa ligi na kuanza kuangalia kwa karibu hatari ya kushuka daraja.

TEN H 01

Ten Hag, ambaye aliipa United mataji mawili ya Carabao Cup na FA Cup katika kipindi chake cha kukinoa kikosi hicho, amesema hakuna timu inayopaswa kujiona salama kwenye Ligi Kuu England kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Akizungumza na kipindi cha Goedemorgen Eredivisie cha ESPN NL, akijibu swali kama Man United inaweza kushuka daraja kocha huyo Mholanzi amesema:

"Katika Ligi Kuu England, kushuka daraja kunawezekana kwa sababu timu zote zina nguvu. Zina vikosi vizuri na makocha bora."

"Unapojikuta upande usio sahihi wa matokeo na kuingia kwenye mzunguko mbaya wa kushindwa, mambo yanaweza kuwa magumu sana."

TEN H 02

Kauli hiyo imekuja wakati United ikionekana kuingia katika mzunguko huo mbaya, huku ushindi ukiendelea kuwa mgumu kupatikana.

Katika michezo ya mwishoni mwa wiki, United ilikuwa kwenye hatari ya kuingia kwenye nafasi tatu za mwisho, lakini Crystal Palace, Nottingham Forest na Sunderland nazo zilishindwa kushinda, hivyo kuipa nafuu ya muda kikosi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, Carrick amepewa muda hadi angalau mapumziko yajayo ya mechi za kimataifa kurekebisha mwenendo wa timu hiyo.

Hata hivyo, kichapo cha Chelsea kimeongeza mashaka kuhusu uwezo wake wa kuibadilisha hali hiyo.

Takwimu zinaonesha kuwa United imeshindwa kushinda katika mechi zake saba za kwanza za ugenini katika mashindano yote msimu huu, jambo ambalo haijawahi kulifanya tangu msimu wa 1973/74, ambao iliishia kushuka daraja.

Kwa sasa Ten Hag anahudumu kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya FC Twente ya nchini Uholanzi.

Licha ya hali mbaya ya United, kocha huyo amesisitiza kuwa anaamini alifanya vizuri wakati akiwa Old Trafford, akitaja mataji aliyoshinda na mafanikio ya timu hiyo chini ya uongozi wake.

TEN H 03

"Nadhani tulifanya vizuri sana Manchester United. Kabla hatujafika, klabu ilikuwa imetumia miaka sita bila kushinda taji. Tulifika Wembley mara sita, tukacheza fainali mbili za FA Cup, tukashinda mataji mawili na kumaliza nafasi ya tatu."

Ten Hag alikiri kuwa kulikuwa na vipindi vigumu, lakini akasisitiza kuwa ushindani mkubwa wa Ligi Kuu England unaweza kuifanya timu yoyote inayopoteza mwelekeo kupata wakati mgumu.

Wakati huohuo, Manchester United jana ilikuwa inajiandaa kukabiliana na Roma katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya kuikaribisha Aston Villa katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu England wikiendi ijayo.

Kwa upande wa uwezekano wa Carrick kuondoka, aliyekuwa kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer, amekiri kuwa asingekataa kurejea Old Trafford endapo angeombwa, ingawa amempa sapoti Carrick akiamini bado anaweza kuigeuza hali ya timu hiyo.