Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag amerudi nyumbani, akabidhiwa FC Twente

TEN Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa zamani wa Manchester United alitimuliwa na klabu hiyo ya Ujerumani, Septemba mwaka jana baada ya mechi mbili tu za Bundesliga.

AMSTERDAM, UHOLANZI: KOCHA, Erik ten Hag amepata kazi mpya katika soka, miezi minne tu baada ya kufukuzwa huko Bayer Leverkusen.

Kocha huyo wa zamani wa Manchester United alitimuliwa na klabu hiyo ya Ujerumani, Septemba mwaka jana baada ya mechi mbili tu za Bundesliga.

Ten Hag, ambaye alishinda mechi yake ya kwanza katika Kombe la Ujerumani dhidi ya timu ya Daraja la Nne, alishindwa kushinda mechi zake zote mbili za ligi akiwa na Leverkusen, na akaingia haraka katika migogoro na viongozi wa klabu, wachezaji pamoja na wafanyakazi wa benchi la ufundi.

Baadaye, Mdachi huyo alihusishwa na Wolves, Novemba na pia alionekana kuwa karibu kurejea Ajax kabla ya mwisho wa mwaka.

TE 01

Hata hivyo, Ten Hag, ambaye alifutwa kazi na Man United, Oktoba 2024 baada ya kushinda mechi 70 kati ya 128 katika kipindi cha miaka miwili na nusu, sasa amerejea rasmi katika ulimwengu wa soka.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 amepata nafasi mpya ya kushangaza kama Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu ya FC Twente, inayoshiriki Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), klabu ambayo aliichezea mara mbili katika maisha yake ya soka.

Ten Hag amesaini mkataba hadi mwaka 2028 na atamrithi mkuu wa sasa Jan Streuer kuanzia mwanzo wa msimu wa 2026/27. Kwa sasa, atafanya kazi katika nafasi nyingine ndani ya klabu yake ya utotoni kuanzia Februari 1.

TE 02

Mshindi huyo wa Kombe la FA, ambaye pia aliiongoza Man United kutwaa Kombe la Carabao, amesema ana hamu kubwa ya kuanza kazi katika klabu ambayo pia ilimpatia hatua zake za kwanza za ukocha.

Ten Hag amesema: “Ninaona ni jambo la kufurahisha na la kipekee kurejea FC Twente, klabu ambayo nimekuwa shabiki wake katika Uwanja wa Het Diekman tangu nikiwa mtoto mdogo. Safari yangu ya soka na ukocha ilianza hapa. Kwa kutumia uzoefu wangu katika kukuza vipaji vya vijana, kujenga timu na utamaduni wa michezo ya kiwango cha juu, nataka kuimarisha msingi wa ufundi wa FC Twente kwa kushirikiana na Bodi ya Usimamizi, uongozi na wafanyakazi, ili klabu iweze kutimiza uwezo wake kwa maendeleo endelevu kama nembo ya fahari ya kanda hii.”

TE 03

REKODI YA UKOCHA YA ERIK TEN HAG

-Go Ahead Eagles (Julai 2010 – Juni 2012):

Mechi 39 | Ushindi 18 | Sare 11 | Kipigo 10

-Bayern Munich II (Juni 2013 – Juni 2015):

Mechi 72 | Ushindi 48 | Sare 10 | Kipigo 14

-Utrecht (Julai 2015 – Desemba 2017):

Mechi 111 | Ushindi 56 | Sare 26 | Kipigo 29

-Ajax (Januari 2018 – Mei 2022):

Mechi 215 | Ushindi 158 | Sare 28 | Kipigo 29

-Man United (Mei 2022 – Oktoba 2024):

Mechi 128 | Ushindi 70 | Sare 23 | Kipigo 35

-Leverkusen (Julai 2025 – Septemba 2025):

Mechi 3 | Ushindi 1 | Sare 1 | Kipigo 1