Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya Haaland, Jude Old Traford yavuja

BACK Pict

Muktasari:

  • Kocha Ole Gunnar Solskjaer, 52, ambaye alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kama kocha wa mpito kabla ya kupewa ajira ya kudumu baada ya kuiongoza vyema timu hiyo, yeye ndiye alipendekeza mastaa hao watatu ambao kwa sasa wanafanya vizuri sana.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United ingeweza kuwasajili wachezaji watatu bora zaidi duniani kwa gharama ndogo, lakini badala yake ilitumia fedha nyingi kuwasajili wachezaji wengine ambao kwa sasa wanaonekana kuwa mizigo.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer, 52, ambaye alichukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kama kocha wa mpito kabla ya kupewa ajira ya kudumu baada ya kuiongoza vyema timu hiyo, yeye ndiye alipendekeza mastaa hao watatu ambao kwa sasa wanafanya vizuri sana.

Kocha huyo alikuwa na mipango mikubwa na ndoto ya kufuata nyayo za kocha wa zamani wa timu hiyo Sir Alex Ferguson na kuirudisha klabu katika zama za makombe.

Kwa mujibu wa tovuti yq Daily Mail, kocha huyo kutoka Norway aliushinikiza uongozi wa Man United kuwahi kuwasajili Erling Haaland, Jude Bellingham na Declan Rice kabla ya wapinzani wao kuanza kuwafuatilia.

Wakati huo Haaland, 25, alikuwa akitamba kwa kutupia mabao akiwa Red Bull Salzburg, Bellingham, 22, alikuwa aking’ara Birmingham City, huku Rice, 26, akifanya yake West Ham.

Hata hivyo, uongozi wa Man United ulipuuza na ukatumia Pauni 39 milioni kumsajili Donny van de Beek mwaka 2020, Pauni 73 milioni kumsajili Jadon Sancho mwaka 2021, na Pauni 13  milioni kumsajili Cristiano Ronaldo.

BAC 01

Solskjaer alishuhudia wachezaji wawili aliowapendekeza wasajiliwe wakinyakuliwa na timu nyingine kubwa barani Ulaya mwaka 2020 pale Haaland na Bellingham walipojiunga na Borussia Dortmund wakati Rice naye akisajiliwa na Arsenal miaka miwili baada ya Solskjaer kufukuzwa kazi na Man United.

Van de Beek, 28, alishindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa na akatolewa kwa mkopo kwenda Everton pamoja na Eintracht Frankfurt mwaka 2022 na 2024, kabla ya kuuzwa jumla kwenda Girona mwaka jana.

Sancho, 25, naye hakuwahi kuonyesha kiwango kilichotarajiwa akiandamwa na majeraha na migogoro na mrithi wa Solskjaer, Erik ten Hag, mwishowe akaishia kutolewa kwa mkopo kwenda Chelsea, Borussia Dortmund na sasa Aston Villa.

Kwa sasa akiwa Villa winga huyo bado hajaonekana kung’ara, na anatarajiwa kuondoka Old Trafford katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa Pauni 250,000 kwa wiki kumalizika.

Ronaldo alirejea Old Trafford miaka 12 tangu aondoke kwenda Real Madrid, baada ya wakala wake Jorge Mendes kuiambia Man United kwamba staa huyo alikuwa karibu kujiunga na Man City.

BAC 02

Hata hivyo, mambo hayakuwa mazuri kwa upande wake kwani licha ya kufunga baadhi ya mabao muhimu, mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or alionekana kuwa chanzo cha migogoro ndani ya klabu akifanya mahojiano ya kushambulia uongozi na kocha na mwisho mkataba wake ukavunjwa mwaka 2022.

Kwa sasa Haaland ndiye kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu England akiwa na mabao 17 katika mechi 16, Bellingham naye anaonekana kuwa staa tegemeo Madrid kama ilivyo kwa Rice kule Arsenal.