Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabu ya EPL iko pale pale!

TABU Pict

Muktasari:

  • Kwenye dimba la Old Trafford, Manchester United inakabiliana na Chelsea katika mechi yenye mvuto mkubwa. United inahitaji pointi tatu muhimu ili kuimarisha nafasi yake baada ya kuanza vibaya msimu huu.

LONDON, ENGLAND: WIKIENDI hii Ligi Kuu England inatarajiwa kuendelea tena, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu mechi mbalimbali hususani ile ya Manchester United dhidi ya Chelsea.

Kwenye dimba la Old Trafford, Manchester United inakabiliana na Chelsea katika mechi yenye mvuto mkubwa. United inahitaji pointi tatu muhimu ili kuimarisha nafasi yake baada ya kuanza vibaya msimu huu.

Man United ambayo inashika nafasi ya 14 ikiwa na alama nne ilizokusanya kwa kushinda mechi moja, sare moja na vipigo viwili katika mechi zao nne za mwanzo wa ligi, ipo katika presha ya kusaka matokeo ili walau kurudi katika nafasi za juu.

Kwa sasa ina tofauti ya alama moja tu dhidi ya timu inayoshika nafasi ya kushuka daraja na pointi nane dhidi ya vinara wa ligi.

Kuanza kwao vibaya ligi msimu huu ni mara ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya mwaka 1992.

Kwa upande wa Chelsea, licha ya kuanza vizuri msimu huu, mabingwa hawa wa Kombe la Dunia kwa Klabu wanahitaji kurudi tena katika mstari kwani hawajapata ushindi katika mechi mbili za mwisho za michuano yote.

Chelsea ilitoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Brentford katika ligi kabla ya kuchapika mabao 3-1 na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tangu mwaka 1995 timu hizi zimekutana mara 77,  Man United ikashinda mechi 22, Chelsea 25 na 30 zikamalizika kwa sare.

Hata hivyo, katika mechi zao mbili za mwisho kukutana katika michuano yote mashetani wekundu hawajaambulia chochote wakifungwa mbili. Mechi hii itaanza saa 1:30 usiku.

Pale jijini Liverpool kutakuwa na dabi ya mitaa ya ambapo Liverpool itawakaribisha majirani zao Everton kwenye dimba la Anfield.

Dabi hii ambayo ndio itakuwa mechi ya mapema kuchezwa kesho, itaanza saa 8:30 mchana na Everton inaingia katika mechi hiyo ikiwa na hali mbaya tofauti na Liverpool ambayo imeshinda mechi zote nne za msimu huu.

Everton imeshinda mbili na inashika nafasi ya sita katika msimamo.

Kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur,  Tottenham itawaikaribisha Brighton & Hove Albion katika mechi yenye umuhimu kwa pande zote.

Spurs inataka kushinda mechi hii ili kupanda katika nafasi za juu zaidi kutoka ile ya tatu ambayo inaishikilia kwa sasa, wakati Brighton ambayo msimu huu imeanza vibaya katika ligi, itakuwa inaangalia nafasi ya kurudi katika mstari na kuonyesha makali ambayo imezoeleka kuonekana ikiyatoa.

Sehemu nyingine kwenye dimba la Turf Moor, Burnley  itakutana na Nottingham Forest katika mechi itakayoanza saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Wolves ikiwa nyumbani itaikaribisha Leeds, vilevile West Ham ikiwa pale London Studium itaikaribisha Crystal Palace ambapo mechi zote zitapigwa kuanzia saa 11:00 jioni.